Selelii aandaa mkutano mkubwa kumpongeza Mpendazoe!

Zyansiku

Member
Joined
Jul 27, 2009
Posts
49
Reaction score
10
Mbunge wa jimbo la Nzega na mmoja kati ya wale walioitwa wapambanaji wa ufisadi Lucas Lumambo Selelii kesho saa nane mchana atahutubia wakazi wa mji wa Nzega kuonyeshwa kufurahishwa kwake na kitendo cha ujasili cha aliyekuwa mpambanaji mwenzie wa ufisadi na mbunge wa kishapu mpendazoe cha kujitoa CCm na kuhamia CCj akisema kitendo hicho hakipaswi kupita bila kupongezwa.
Selelii aliyasema hayo mara baada ya mkutano wa kumsimika kamanda wa vijana wa nzega Ndg mbozu kijijini kwa ke Isanzu! akiwa amezungungukwa na baadhi ya wasaidizi wake akiwemo katibu wake ambaye pia ni katibu mwenezi wa nzega bwana Mayunga Selelii alisema" najua kuna watu watataka kujua nini msimamo wangu juu ya alichokifanya Mpendazoe nasema hivi yule bwana Mwanaume, haogopi cha nini wala nini na zaidi ametumia haki yake ya kikatiba na kesho nitakuwa na mkutano mkuwa wa kutangaza nia yangu ya kugombea tena jimbo la nzega lakini muda ukiruhusu sitasita kumzungumzia mwanaume wa Mbegu Mpendazoe"
Mkutano huo ambao utafanyika katika viwanja vya "Parking Nzega' utahudhuriwa na wana CCM kadha wa jimbo la nzega ambao Selelii hakutaka kuwataja zaidi ya kusema utakuwa mkutano wa kihistoria!
Nitawajuza kila litalojiri kwani nitakuwepo Nzega.
 
Haya sasa!
Mambo taratibu yananoga!
Hao waliomlaani Mpendazoe leo wakae mkao wa kula kumlaani mtu mwingine very soon!
Na trend hiyo itaendelea saana mwaka huu!
 
Watasema nae mzigo mwishoe wao ndo watakuwa vifurushi
 
Huyu si ndiye gazeti la Uhuru la leo limemquote akisema kwamba Mpendazoe amejichimbia kaburi? Au Uhuru lilimtafuta makusudi kumuhoji na kisha kupotosha? Nani mkweli, Selelii au gazeti la Uhuru la leo?
 
Haya sasa!
Mambo taratibu yananoga!
Hao waliomlaani Mpendazoe leo wakae mkao wa kula kumlaani mtu mwingine very soon!
Na trend hiyo itaendelea saana mwaka huu!

kajisemea Mpendazoe the list is long

Selelii hata wewe big up
kwa nini usimpongeze Mpendazoe kama anastahili......
 
Huyu naye akichomoa na kuondoka huko kwenye chama cha maf.... labda ndiyo utakuwa mwanzo wa trend ya kukimbia chama hicho. Only time will tell.
 
Na mm natangaza nia yangu ya kuondoka ssm na kukaa bila kuwa mwanachama kwanza.......(nangoja waje kunigombea, atakayepanda dau najiunga na chama hicho)
 
Hatimaye karudi nyumbani kwa wapiga kura, dakika za majeruhi!!!!!. Hajafanya kitu kwa wapiga kura wake, katumia muda mwingi na vita ya mafisadi ambayo haijazaa matunda yoyote. Wananchi wake walikuwa wanategemea maendeleo, sijui atawambia nini? Nzega inazidi kurudi nyuma kimaendeleo kila uchwao.
 
Mie hapo ndo politic ya bongo inaponiacha hoi, uchaguzi unakaribia ni mbinu gani watu watafanya kupunguza viti vya CCM bungeni au kumiliki bunge tunabaki na habari ya mpendazoe, tuliona wengi walitoka na wakarudi vichwa chini suruali za mikanda zikiwa hazifungi eg. Lamwai, hebu watu wa concentrate CCM inatia kichefu chefu, haitaki kubadilika!
 
Huyu naye akichomoa na kuondoka huko kwenye chama cha maf.... labda ndiyo utakuwa mwanzo wa trend ya kukimbia chama hicho. Only time will tell.

BAK I cant wait for that wave, natamani ningeamka kesho nikakutana na habari njema!!
 
Mmh Sijui nitawahi uchaguzi wa mwaka huu?

Annina
 
Saa sita dk moja usiku bado - usilete mambo ya 1st of April wakati muda haujafika Mkuu.
 
Mbunge wa jimbo la Nzega na mmoja kati ya wale walioitwa wapambanaji wa ufisadi Lucas Lumambo Selelii kesho saa nane mchana atahutubia wakazi wa mji wa Nzega kuonyeshwa kufurahishwa kwake na kitendo cha ujasili cha aliyekuwa mpambanaji mwenzie wa ufisadi na mbunge wa kishapu mpendazoe cha kujitoa CCm na kuhamia CCj akisema kitendo hicho hakipaswi kupita bila kupongezwa.
Selelii aliyasema hayo mara baada ya mkutano wa kumsimika kamanda wa vijana wa nzega Ndg mbozu kijijini kwa ke Isanzu! akiwa amezungungukwa na baadhi ya wasaidizi wake akiwemo katibu wake ambaye pia ni katibu mwenezi wa nzega bwana Mayunga Selelii alisema" najua kuna watu watataka kujua nini msimamo wangu juu ya alichokifanya Mpendazoe nasema hivi yule bwana Mwanaume, haogopi cha nini wala nini na zaidi ametumia haki yake ya kikatiba na kesho nitakuwa na mkutano mkuwa wa kutangaza nia yangu ya kugombea tena jimbo la nzega lakini muda ukiruhusu sitasita kumzungumzia mwanaume wa Mbegu Mpendazoe"
Mkutano huo ambao utafanyika katika viwanja vya "Parking Nzega' utahudhuriwa na wana CCM kadha wa jimbo la nzega ambao Selelii hakutaka kuwataja zaidi ya kusema utakuwa mkutano wa kihistoria!
Nitawajuza kila litalojiri kwani nitakuwepo Nzega.

Mbona huyu ndugu yuko Dar katika kamati za bunge? Na waandishi wa magazeti walimhoji kutoa na msimamo wake, tuache kutunga vitu vya kufikirika! JF is a big thing.
 
Huyu nae anatafunwa na mdudu mtu aliyemtafuna mpendazoe, muda wote alikuwa kamanda wa ufisadi sasa anatapatapa,hana jeuli kwa kijana husein bashe naona sasa kaanza ku bwatabwata hiyo yote ni kujiami kwa chaguo la wana nzega jipya.
Huu ni wakati wa vijana wazee watuachio ccm yetu wamfuate mpendazoe.
 
Haya sasa!
Mambo taratibu yananoga!
Hao waliomlaani Mpendazoe leo wakae mkao wa kula kumlaani mtu mwingine very soon!
Na trend hiyo itaendelea saana mwaka huu!
PJ cousin, kabla hujaenda mbali fikiria kwanza huyuhuyu selelii amesema hakupata muda wa kumshauri mpendazoe kuhusu kuondoka ccm... na ni huyuhuyu selelii aliyesema hawezi kuhama ccm...

tusubiri ukweli uje na pia tujue source ya hii habari kabla ya kutoa matawi yetu guys

hiki ni kipindi cha dawasco na dssd maji taka plus
 
Saa sita dk moja usiku bado - usilete mambo ya 1st of April wakati muda haujafika Mkuu.

Yaani na mimi nimeshtukizia. Huyu huyu Selelii ambaye leo magazeti yamemnukuu akisema rafiki yake Mpendazoe ni msiri sana na amefanya kosa kuhama?

Na amefika saa ngapi Nzega, si alikuwa kwenye kikao cha kamati gani sijui, Dar?

Aisee hii ishu imeshika watu wengi, naomba tuwekeane mkataba kuwa "no April Fool's pranks on this issue!!"
 
Back
Top Bottom