Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ilitangaza kukamilisha kuchakata majina ya waombaji wa awamu ya pili tarehe 23/09/2018 na kuwa majina hayo yamekwisha rudishwa vyuoni kwa ajili ya kutangazwa.
Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo SUA hatujaweza kutangaza majina yote ya waombaji waliochaguliwa katika awamu ya pili. SUA inaendelea kufanyia kazi suala hilo ikishirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania na likikamilika muda wowote majina yatatangazwa.
Tunaomba uvumilivu katika wakati huu mara tutakapo tatua changamoto iliyojitokeza majina yatatangazwa.
Mwisho tunaomba radhi tena kwa usumbufu uliojitokeza
IMETOLEWA NA MKURUGENZI,
KURUGENZI YA MASOMO YA SHAHADA ZA AWALI
Yaan usijaribuu until wakujibu ni wajibu wao and umelipia pesa ya udahili ukiona kimya leoo usijaribu kutuma chochote kesho necta TCU uwaeleze then kitafahamika maana kila chuo lazima kitoe majina Leo hili Wanafunzi waweze kujuwa hatima yao
# sua wametoa tangazo kwamba kunashida ya kimtandao imejitokeza but wamefny utaratibu wa kuwasiliana na tcu kwaivo starting now second round wanaweza wakatoa majina
Kwa waliofanikiwa kudownlod majina ya waliokosea loanboard washee hapa. Nina madogo wawili wote wote hawakumbuki credentials za acc zao loanboard na nimejaribu kuyadowload tangu jana bado download in progress.