Tatizo watu hawapendi kupata taarifa sahihi kabla ya kuingia kwenye biashara.
iko hivi biashara ya commision bases inafaida ndogo sana kutokana na nature yake ilivyo kwani imekaa kihuduma zaidi na ina middle mens kadhaa kabla ya kumfikia mlaji.
Hivyo basi ni vema unayetaka kufanya biashara hii ukautazama kwa jicho la kama ni bidhaa ndani ya biashara nyingine mfano una duka la kuuza vyakula zaidi ya bidhaa nyingine unazouza weka hiyo maxmalipo? tigo pesa, mpesa, airtel money,mashine ya beeting na wakala wa bank kama equty nakadhalika hapo itaifurahia hiyo biashara.
Mfano mimi binafsi ndivyo ni biashara ya stationery natoa huduma hizo pamoja na uwakala wa equity bank nikichanganya commision zote kwa mwezi hazipungui 600,000 faida kwa mwezi nikijumlisha na mauzo ya stationery najikuta pato langu kwa mwezi ni around 1m. hivi.
Changamoto inahitaji mtaji wa kutosha ili upate faida hiyo pili risk upotevu wa hela na wizi ni tatizo.