AUGUSTINO CHIWINGA
JF-Expert Member
- Apr 23, 2017
- 220
- 689
Augustino Chiwinga
Mtama-Lindi.
0659438889
Nimepata bahati ya kutembelea katika Hospitali kadhaa za umma hapa nchini.Kiukweli mabadiliko.niliyoyakuta huko ni makubwa kuanzia kwenye miundombinu kwa maaana ya majengo, madawa , vifaa tiba pamoja na gharama za chini za matibabu.
Nadiriki kusema Watanzania wapo salama na wana uhakika wa kupata matibabu kwa haraka. Kwanza kupitia mfumo wa matibabu ya kuchangia ( Cost Sharing ) ilinilazimu kutumia shilingi elfu mbili tu (2,000) kufungua file, kumuona Daktari,vipimo na kupata dawa zote nilizoandikiwa mpaka nikaona ni miujiza na nikajiuliza maswali labda huenda nipo nje ya nchi na si Tanzania.
Nikawadadisi baadhi ya wagonjwa ili kujua kama huduma hizi zinatolewa kila siku nao wakaniambia kwamba tangu Rais Magufuli aingie madarakani mambo yamebadilika na wao kama wananchi wanyonge wa hali ya chini wanaotegemea Hospitali za umma kupata matibabu wanashukuru sana kwa mabadiliko haya makubwa.
Kwa haya niliyoyashuhudia niseme nini zaidi ya kumshukuru Rais Magufuli kwa kuongeza Bajeti ya Afya mpaka Bilioni 270. Sasa hivi katika vituo vya afya nchi nzima Serikali inapanua miundombinu kwa kujenga wodi mpya na theatre kwa ajili ya operation ndogo ndogo zikiwemo za uzazi.Bila kusahau jumla ya Halmashauri 68 Tanzania nzima zimepewa shilingi Bilion 1.5 kwa ajili ya kujenga Hospitali kubwa za kisasa za Wilaya.
Serikali ya Magufuli imedhamiria kuifanya Tanzania kama Ulaya hakika inawezekana ,hakika Rais Magufuli ni kiongozi makini.
Rais Magufuli tutakukumbuka!