Sekondari kongwe za umma kurejeshewa makali yake

nsekwa

JF-Expert Member
Dec 18, 2015
938
1,399
Serikali imeeleza mkakati wa kuzirudisha shule 33 maarufu katika ubora wake ili ziweze kufanya vizuri kama ilivyokuwa zamani.

Mkakati huo ulielezwa jana na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alipokuwa akiwasilisha hotuba ya bajeti yake bungeni.

Alisema shule hizo zilipokuwa nzuri zikitoa elimu bora, zilizalisha vipaji vingi, akiwamo yeye aliyesoma katika mojawapo.Alisema katika awamu ya kwanza, shule 33 zitakarabatiwa.

Alizitaja shule hizo kuwa ni Ihungo, Ilboru, Kilakala, Mwenge, Msalato, Mzumbe, Ngaza, Pugu, Same, Tabora Boys na Tabora Girls.

Nyingine ni Azania, Jangwani, Kantalamba, Mpwapwa, Tosamaganga, Malangali, Milambo, Nangwa, Kibiti, Minaki, Ifakara, Songea Boys, Ndanda, Kigoma, Kibaha na shule za ufundi za Bwiru Boys, Ifunda, Iyunga, Moshi, Mtwara, Musoma na Tanga.

TUMWOMBE MUNGU MAMBO YAWE HIVYO, MAANA HALI ILIKUWA MBAYA SANA.
 
Bora ukaokoe jahazi mama...
Shule za ufund ndo lovulovu kabsa...
Nikianza na shule yangu kipenz Tanga technical
Mi yangu Iyunga imechakaa kupitiliza.ilikuwa inatoa one za kutosha na ilikuwa ni pure science
 
Utaratibu wa kuwateua wanafunzi wanaofaulu urekebishwe!,ili shule zipokee wanafunzi waliofaulu kwa alama stahili.
Mfumo wa utungaji mitihani uboreshwe(si hizi hata wasio jua kusoma na kuandika wanafaulu).
Wanasiasa waache kulazimisha ufaulu(huwa wanatoa kauli 'ole wake mwalimu ambaye hatafaulisha wanafunzi').
 
Mbona pacha wa Nganza yaani Nsumba haipo?
The best government school in Mwanza
nadhani katika shule 33 basi na nsumba imo mkuu, kataja chache tu na hazijafika 33, ila kweli zamani ulikuwa ukisoma shule za serikali unaonekana genious, baadae mambo yakawa vice versa, sasa hivi ukionekana unasoma shule za serikali we ni bongo lala, nitafurahi sana mama ndalichako ukirudisha hadhi ya shule za serikali, mie nilikuwa milambo secondary tabora
 
Itarudisha heshima ya shule za umma kama vilivyo vyuo vikuu vya umma. Inawezekana kama serikali na wizara zitachukua hatua hiyo kama waziri alivyosema. I will pat her back when she implements the plan!
 
Back
Top Bottom