Mkakati wa Serikali kuzirudisha shule 33 maaarufu katika ubora wake usiwe wa maneno matupu

Jul 8, 2013
47
65
Mkakati wa Serikali kuzirudisha shule 33 maaarufu katika ubora wake usiwe wa maneno matupu na pia uangalie shule zote za Umma.

Serikali imetangaza rasmi kuanza mkakati wa kuziboresha shule kongwe ili zirudi katika ubora wake.

Shule 33 zilizotajwa ni hizi
Ihungo,Ilboru,Kilakala,Mwenge, msalato,Mzumbe,Nganza,Pugu,Same,Tabora Boys na Tabora Girls.
Zingine ni hizi Azania,Jangwani,Malangali,Kantalamba,Mpwapwa,Tosamaganga,Milambo,Nangwa,Kibiti,Minaki,Ifakara,Songea Boys,Ndanda,Kigoma,Kibaha na shule za ufundi Bwiru BOYS,Ifunda Tech,Iyunga,Moshi Tech,Mtwara,Musoma na Tanga Tech.

Hata hivyo serikali kabla ya kuanza kutekeleza mkakati huu ni lazima zipatikane sababu juu ya ni nini kimeziofikisha shule hizo hapo zilipo? Zikipatikana sababu ndipo ianze kazi ya kusaka majawabuu ya matatizo hayo.

Hizi shule 33 zinazoitwa maarufu kwa sasa yamebaki majina tu ni vyema huu mkakati uanze na kusaka chanzo cha anguko la shule hizi ndipo watu waanze kufikicha bongo zao ili kunusuru elimu yetu ambayo imetufikisha katika hatua ya kupeleka chuo kikuu watu wasio na sifa stahiki.

Pia mkakati huu uanglie shule zingine za umma maana ukifika vijiji kama mapaliji huko wilayani Chunya au Ulefi huko Mufindi na namna huduma za elimu zinavyotolewa ni hatari tupu.

Mama Ndalichako anza kutenda sasa maana hata aliyekuwa mkurugenzi wa Wilaya ya Mufindi mwaka 2011 alihaidi mbele ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Malangali walioandamana kupigani mabadiliko ya kweli katika shule yao kuwa Bunge la Tanzania katika bajeti yake limetenga Milioni 200 ili kuikarabati Shule ya Sekondari Malangali lakini ilikuwa ni ahadi ya uongo ambayo utekelezaji wake haujafanyika mpaka keshokutwa.

Elimu ni uhai wa Taifa lolote
 
Back
Top Bottom