Seif Khatib aja na lake kuhusu REDET Report

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
Serikali: Matokeo REDET safi




na Ratifa Baranyikwa



SERIKALI imesema ripoti ya utafiti uliofanywa na Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET), imeonyesha kuwa watu wengi wanaridhika na utendaji wa Serikali na Rais Jakaya Kikwete kuliko inavyoelezwa na baadhi ya watu.
Tamko rasmi la serikali kuhusu ripoti hiyo ya Redet lilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Muhammed Seif Khatib mbele ya waandishi wa habari.

Waziri Khatib katika tamko lake hilo alisema, matokeo hayo ya Redet yameonyesha pia kwamba, watu wanaoridhika na utendaji wa kazi wa serikali wanafikia asilimia 79.4, unapochanganya wale waliotengwa katika makundi mawili ya wanaoridhika sana na wanaoridhika kiasi.

Khatib alisema serikali imelazimika kutoa tamko hilo sasa baada ya kuwapo kwa maoni tofauti ya wananchi tangu Redet, walipotoa maoni yao hayo wiki mbili zilizopita.

Akizungumzia juu ya utafiti huo ambao lengo kubwa ni kuboresha utendaji wa shughuli za serikali na kuleta maendeleo kwa watu walio wengi na kuimarisha demokrasia nchini, Khatib alisema kuwa, kwa mujibu wa utafiti huo, serikali ya awamu ya nne imeona imepata mafanikio makubwa katika miaka miwili ya mwanzo ya uongozi wake wa miaka mitano.

Katika hilo, Khatib alisema kuwa katika uchambuzi uliofanywa na serikali, neno ridhika ambalo limetumiwa kuwahoji wananchi kutoa tathimini juu ya utendaji wa serikali ambalo lilitengwa katika vipengele vitatu, ambavyo ni ‘Naridhika sana’, ‘Naridhika kiasi’, na ‘Siridhiki’ lina maana moja.

“Kwa mujibu wa kamusi ya kiswahili sanifu, Toleo la pili mwaka 2004, neno ridhika linamaanisha kutosheka na maelezo au kufurahia kitu fulani, kwa mantiki hiyo basi “kuridhika sana” na “kuridhika kiasi” kote ni kuridhika,” alisema Khatib.

Akitoa mfano, Khatib alisema kuwa matokeo ya utafiti wa Redet juu ya utendaji wa kazi wa Rais Kikwete unaonyesha kuwa asilimia 44.4 walisema ‘naridhika sana’ na asilimia 35.0 wakasema ‘naridhika kiasi’.

Alisema kutokana na matokeo hayo, bila ya kujali maneno ‘sana’ au ‘kiasi’, utabaini kuwa wananchi wanaoridhishwa na utendaji wa serikali kinachoonekana ni kwamba wanaoridhika ni asilimia 79.4.

Pamoja na hilo, Khatib alikiri kuteremka kwa maoni ya watu kuhusu utendaji wa Rais Jakaya Kikwete pamoja na utendaji wa Baraza la Mawaziri kama ilivyoonyeshwa kwenye utafiti ukilinganisha na ilivyokuwa mwaka jana ambako watu waliokuwa wakiridhika na utendaji wa Rais Kikwete ni asilimia 90.1.

Alielezea sababu za kuporomoka huko, kulitokana na kuwapo kwa tuhuma kadhaa dhidi ya serikali wakati utafiti huo ulipokuwa ukifanyika.

Mbali ya hilo, Khatib alisema utafiti huo ulionyesha kuwa idadi ya watu waliokuwa wakiridhishwa na utendaji wa Baraza la Mawaziri walikuwa asilimia 61.2 unapochanganya wale wanaoridhika sana 20.2% na wanaoridhika kiasi 41.4%.

“Kwa upande wa serikali za mitaa wananchi waliosema “Naridhika sana” ni asilimia 32.5 na waliosema “Naridhika kiasi” ni asilimia 47.1 hivyo wananchi walioridhika na utendaji wa serikali za mitaa ni asilimia 79.6.

“ Kuhusu Bunge wananchi waliosema “Naridhika sana” ni asilimia 21.8 na waliosema “ Naridhika kiasi” ni asilimia 42.5 kwa hiyo wananchi walioridhika na utendaji wa kazi za Bunge ni asilimia 64.3,” alisema Khatib.

Hata hivyo alisema kuwa kuhusu Watanzania wengi wasiosoma ambao wameonekana kuunga mkono utendaji wa rais kuliko wasomi, serikali ina wajibu wa kuwahudumia Watanzania wote bila kujali wenye elimu na wasio na elimu.

“Kwanza hao wachache wa chuo kikuu wanaomuunga mkono rais, chuo kikuu idadi yake ni ndogo sana,” alisema.

Aidha, kuhusu mengineyo, tatizo kubwa ambalo utafiti umeonyesha kwa wananchi kutoridhika na mahitaji kama ya afya, elimu, maji na miundombinu, serikali imesema kuwa inakubali sehemu hizo kuwa na matatizo na wananchi kutoridhika, lakini bajeti ya mwaka huu imelenga kuboresha maeneo hayo.

Khatib alisema kuwa kufuatia ufafanuzi huo wa utafiti uliofanywa na Redet, serikali inapenda kusisitiza kuwa imefanya mambo makubwa ya maendeleo ambayo yanaonekana wazi machoni mwa wananchi na Watanzania wanapaswa kuelewa kwamba, mkataba kati ya uongozi wa chama tawala (CCM) na serikali ni wa miaka mitano, na hadi hivi sasa serikali inaamini kuwa utekelezaji wa ilani ya chama hicho unaendelea vizuri na utakamilika kama ilivyokusudiwa.

Khatib alisema kuwa serikali inaipongeza Redet kwa utafiti wake, aidha inaipokea taarifa kama changamoto ya kuendelea kutekeleza ahadi mbalimbali za serikali kwa wananchi.

Aidha, serikali imeishauri Redet izidi kuendelea na tafiti mbalimbali za aina hiyo ambazo zitatoa changamoto kwa serikali iliyoko madarakani.


tanzania daima
 
Hii ni mpya ya kufunga mwaka.
Yaani mawaziri wetu nadhani over 90% ya muda wao wanatumia kufikiria namna ya kuspin badala ya kufikiria mipango ya kuwaletea maendeleo wananchi.Wana-focus kutawala tuu.
 
Muda wote Khatib alikuwa wapi!
Muda wote alikuwa akipanga atoke vipi huyu mtu.
QUOTE 'Mbali ya hilo, Khatib alisema utafiti huo ulionyesha kuwa idadi ya watu waliokuwa wakiridhishwa na utendaji wa Baraza la Mawaziri walikuwa asilimia 61.2 unapochanganya wale wanaoridhika sana 20.2% na wanaoridhika kiasi 41.4%'
Mawe mmepigwa na kuzomewa juu, sasa tujaze magazine ndo mtajua.
usanii kwenda mbele
 
Nimecheka kweli kweli niliposoma hii habari, yaani ni taabu tupu.

Kumbe yule waziri wa Sadaam (Muhammed Saeed al-Sahaf)hayuko peke yake.
 
Kwenye post yangu ya nyuma nilsema exactly aliyosema waziri, ni kwa bahati mbaya sana kwamba asimilimia kubwa ya waandishi hata mashuleni walipita kimkanda mkanda hata interpretation ya statistical data rahisi kama za REDET walishindwa. Well, wengine of course ilikuwa makusudi. Watu hao hao ukiwaambia Umepata maksi daraja A, B, C, D, F. wanakuambia hata aliyepata D. amefaulu Lakini ati kuridhika sana, na kuridhika kiasi maana yake sio kuridhika, ati maana ya kuridhika kiasi maana yake sio kuridhika du!
 
'Mbali ya hilo, Khatib alisema utafiti huo ulionyesha kuwa idadi ya watu waliokuwa wakiridhishwa na utendaji wa Baraza la Mawaziri walikuwa asilimia 61.2 unapochanganya wale wanaoridhika sana 20.2% na wanaoridhika kiasi 41.4%'

Kwa hiyo kwa interpretation ya huyu waziri kama hao wanaoridhika sana wangekuwa say 52% na wale wa kiasi 65% in maana wanaoridhika ni 117% shame on this man jamani kweli nchi itaenda ukiwa na this type of viongozi?
 
....Again, There Goes The Tanzanian 'Comical Ali'!!!

Tukitumia Neno 'VILAZA', Watasema Tumekosa Maadili Ya Kitanzania!!

Hivi Viongozi Wetu Wanapo Bwabwaja na Kutoa Matamshi Kama Haya Yenye Lengo La Kuongopea Wananchi Kwa Kutoa Utitiri wa Takwimu Wanajua Maadili na Kanuni za Uongozi Bora?!



SteveD.
 
Hii ni mpya ya kufunga mwaka.
Yaani mawaziri wetu nadhani over 90% ya muda wao wanatumia kufikiria namna ya kuspin badala ya kufikiria mipango ya kuwaletea maendeleo wananchi.Wana-focus kutawala tuu.

..niliposoma kwamba kamusi imetumika nikasema ngoja nisome simulizi za "ze comedy"!

..usanii mtupu,bila aibu!
 
Kwenye post yangu ya nyuma nilsema exactly aliyosema waziri, ni kwa bahati mbaya sana kwamba asimilimia kubwa ya waandishi hata mashuleni walipita kimkanda mkanda hata interpretation ya statistical data rahisi kama za REDET walishindwa. Well, wengine of course ilikuwa makusudi. Watu hao hao ukiwaambia Umepata maksi daraja A, B, C, D, F. wanakuambia hata aliyepata D. amefaulu Lakini ati kuridhika sana, na kuridhika kiasi maana yake sio kuridhika, ati maana ya kuridhika kiasi maana yake sio kuridhika du!

..kilitime,

..kushiba sana,kushiba kiasi na kushiba....vyote ni kushiba tu?

..kucheka sana,kucheka kiasi na kucheka....vyote ni kucheka tu?

..na hii haina maana kabisa kwenye opinions,sio?
 
..mtu akikwambia amecheka sana[pengine mpaka mbavu kuuma],ina maana amecheka tu?haina maana zaidi?

..mtu akasema amecheka[pengine kukuridhisha,ulipokuwa unachekesha,ili usiwe offended kakuchunia],ina maana amecheka tu?haina maana zaidi?

..sasa,hao watu wawili hawafanani katika opinion zao juu ya kilichowafanya wacheke,mmoja atasema alikuwa amefurahi[amused]kupita kiasi na mwengine atasema hakuchekeshwa na chochote,alitimiza wajibu tu!
 
Exams:
Question No. 8;

Among 100 viewers of TV program surveyed by Kalumanzira Research Insitute, the viewers were asked to rate how they are sastified with "Ze Commedy TV Program..." they were asked to chose one of the following satisfaction level according to their satisfaction.

A. Excellent
B. Very good
C. Good
D. Undecided
D. Bad.

After the research the following results were revealed;
10% said Excelent, 30% very good, 10% good, 5% undecided, and the rest they said program need to be banned in other words bad!

You are asked to advise the TV owner on the percentage of the viewers who are satisfied with the program?

What will be the answer?
 
It is a literal translation:
Very satisfaied
Somewhat satisfied
Not Satisfied

So, is it rational to treat the 'somewhat satisfied' as being satisfied?

REDET have to find a better 'msamiati' katika survey tool yao kama wanataka kupata maoni sahihi ya wananchi.

Kama Khatib hastushwi na maoni ya wasomi, pamoja na kwamba ni wachache, basi na ajiandae kupambana na hali ngumu. Yeye anataka aone kwanza vijijini wanamkataa kabla ya kuamini? Opinion formers ni hao hao wasomi.
 
Supposing Khatib is right for the sake of argument, it is pathetic to see him setting such low standards and expectations for a government that started with so much hoopla.I would expect him to focus on strategies to perform better and convert the "somewhat satisfied" into "very satisfied" instead of claiming the "somewhat satisfied" shamelessly without even asking himself why are they "somewhat" satisfied.

If people call this government "vilaza" it is righly so_One characteristic of a kilaza is to seek just the passmark, not bothering with putting effort for a stellar performance.At the end of the process the people are shortchanged.
 
Huyu Khatib sitakaa nimsahau.He came to our school in the mid 80s.It was close to elections.
Alituambia kuwa wote ni malofa kwenye ile school.
Tulimshangaa sana.Then tukamuuliza why unatuita wote malofa?
Akatuambia msingekuwa malofa mngekuwa mnasoma shule za kifahari (international schools, au shule za Dar).Tukamuuliza zaidi kwanini sisi malofa?? akasema sababu ni watoto wa wakulima na wafanyakazi.

Lakini mpaka nimekuwa mtu mzima-still I have fresh memmories of his utterances na sijaona justification yake. Of course, we created negative perception because some of students had different backgrounds. Among others were a son of 'mzee wa ukweli na uwazi'.

Unfortunately, the ghost is not gone,it is still there.

Really, hatuwezi kuendelea kwa mtindo huu.Why? hata kama issue ni union, ndiyo kusema hamna watu bora zaidi ya Khatib kutoka upande wa pili??
 
Huyu Khatib sitakaa nimsahau.He came to our school in the mid 80s.It was close to elections.
Alituambia kuwa wote ni malofa kwenye ile school.
Tulimshangaa sana.Then tukamuuliza why unatuita wote malofa?
Akatuambia msingekuwa malofa mngekuwa mnasoma shule za kifahari (international schools, au shule za Dar).Tukamuuliza zaidi kwanini sisi malofa?? akasema sababu ni watoto wa wakulima na wafanyakazi.

Lakini mpaka nimekuwa mtu mzima-still I have fresh memmories of his utterances na sijaona justification yake. Of course, we created negative perception because some of students had different backgrounds. Among others were a son of 'mzee wa ukweli na uwazi'.

Unfortunately, the ghost is not gone,it is still there.

Really, hatuwezi kuendelea kwa mtindo huu.Why? hata kama issue ni union, ndiyo kusema hamna watu bora zaidi ya Khatib kutoka upande wa pili??


NINA IMANI KUNA WATU ZAIDI YA 1000 MPAKA MWISHO WA WIKI IJAYO WANAOWEZA KUCHUKUA NAFASI YAKE NA KUFANYA BORA ZAIDI. KUNA WATU ZAIDI YA 10,000 MPAKA MWISHO WA MWEZI UJAO WANAOWEZA KUCHUKUA NAFASI YAKE NA KUFANYA KAZI NA KUTOA MATAMSHI YA KULETA MAANA ZAIDI. PIA NAAMINI KUNA WATU ZAIDI YA 100,000 MPAKA MWAKA KESHO WANAOWEZA KUCHUKUA NAFASI HIYO NA KUTOA MAWAIDHA YENYE LENGO LA KULETA MEMA NCHINI MWETU KULIKO HAYO YALIYOTOLEWA.

TATIZO: KUNA WATU SI ZAIDI YA 2 WANAOFAHAMIANA NA KUELEWANA NA MUUNGWANA KAMA JINSI ALIVYO YEYE!!


SteveD.
 
Exams:
Question No. 8;

Among 100 viewers of TV program surveyed by Kalumanzira Research Insitute, the viewers were asked to rate how they are sastified with "Ze Commedy TV Program..." they were asked to chose one of the following satisfaction level according to their satisfaction.

A. Excellent
B. Very good
C. Good
D. Undecided
D. Bad.

After the research the following results were revealed;
10% said Excelent, 30% very good, 10% good, 5% undecided, and the rest they said program need to be banned in other words bad!

You are asked to advise the TV owner on the percentage of the viewers who are satisfied with the program?


What will be the answer?

Kilitime,

Those are just numbers, they have very little meaning unless you use them to compare with past results or results obtained for other parties, in your case other programs.

The real meaning of REDET poll comes when you compare JK and his government ratings in 2007 to results obtained last year.

Good may be a good mark if your last attempt ended with bad or fail, but it may be a disappointing result if a year ago, you received Excellent.

Important thing here is to establish trends, and from what I saw from REDET poll, trends for all attributes are going down and that is not a good sign for JK and his government.

The only positive thing (for CCM) I can think of is coming from the fact that CCM as a party is still doing well compared to opposition.
 
Kilitime,

The only positive thing (for CCM) I can think of is coming from the fact that CCM as a party is still doing well compared to opposition.

Mwanzo wa safari yoyote ni hatua moja. Hivyo nguvu za CCM zinaendelea kupungua mwaka hadi mwaka. If they will continue to manipulate Tanzanians and "rape" the Economy, believe you me they will soon face a "Free fall".
 
Nilikuwa nimeanza kuandika makala zangu za kufunga mwaka; sikutarajia nitapewa kachumbari ya hoja kama hii ya Khatib; hata kichwa cha habari imenibidi nibadili.. Jumatano ijayo makala ya "Kasungura" na ile ya "ndege ya Lowassa" zitakuwa ni kama preview!! Ee molanipe nafasi niseme nitakachosema!!!! Utani mwingine mbaya.
 
Results za REDET, kwangu mimi zinaonyesha reality kwa CCM na popote pale, ukiwa madarakani kama unafanya kazi lazima uzalishe wasioridhika, especially wakati uki-enfforce sheria mbalimbali! mchezaji wa soka wa substitution wakati anaingia anaona kama vile anenda kufungia timu yake magolo 3, lakini baada ya muda mambo yale yale.
Kwa hiyo katia ku-riew mambo yabidi uwe makini uangalie kwa mapana! Maana kwa jinsi Wapinzani wa CCM, wanavyotutaka twaelewe ni a if Tsh.320Bil ziazokusanywa na TRA haiendi kutekeleza mradi wowote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom