Seif amsindikiza Rais Karume kutunukiwa shahada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Seif amsindikiza Rais Karume kutunukiwa shahada

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Nov 15, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,770
  Trophy Points: 280
  Seif amsindikiza Rais Karume kutunukiwa shahada[​IMG]Waandishi wetu

  UHUSIANO kati ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Dk Amani Karume na Chama cha Wananchi (CUF), unaonekana kuendelea kuimarika baada ya viongozi wa chama hicho jana kumsindikiza rais huyo katika hafla ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu.

  Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu Maalim Seif jana walimsindikiza Karume katika kutunukiwa shahada hiyo iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki.

  Baada ya rais huyo wa Zanzibar kutunukiwa shahada hiyo, mshereheshaji alitangaza makundi ya picha za pamoja ambapo kundi la kwanza lilikuwa la Karume na viongozi wa siasa; Kundi hilo ndilo lililowashirikisha pia viongozi wa CUF.

  Kabla ya kupiga picha Maalim Seif alikwenda kumpa mkono wa kumpongeza Karume akafuatia Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na wakafuatia wengine.

  Hata hivyo, viongozi hao wote jana hawakuwa tayari kuzungumzia kwa undani walichozungumza wakati walipokutana.

  Rais Karume alisema tofauti kubwa iliyokuwepo visiwani humo ni ya kiitikadi za kisiasa hali ambayo alibainisha kuwa sasa imekuwa historia kutokana na CUF, kutangaza kumtambua rais huyo.

  Novemba saba mwaka huu, Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif aliwatangazia mamia ya wafuasi wa chama hicho kisiwani Pemba kwamba chama hicho kimeamua kumtambua rasmi Rais Karume.

  Pamoja na hatua hiyo ya CUF, kupongezwa na watu mbalimbali zikiwamo taasisi za kimataifa na mabalozi, ilikuwa mwiba kwa wanachama wa CUF, ambao wengi wao waliangua vilio baada ya kusikia kauli ya Seif.

  Kauli hiyo mpaka sasa imeibua makundi miongoni mwa wanachama wa CUF, huku baadhi ya wanachama hao wakimuunga mkono Seif na wengine kumpinga.

  Akizungumzia hali hiyo jana, Seif alisema kulikuwa na chuki ya dhahiri miongoni mwa Wazanzibari kwa misingi ya kisiasa na kuwa hali hiyo ndiyo iliyofanya watu wakalia kama watoto wadogo, baada ya kusikia kiongozi wao huyo kutangaza kumtambua Rais Karume.

  “Kwa hatua tuliyofikia tutaiepusha nchi yetu na mambo mengi mabaya, hatua hii imefikiwa kwa maslai ya Zanzibar, tumechoswa na migogoro Zanzibar, nyiye waandhisi simnajua kuwa sisi wazanzibar tuna matatizo yetu wenyewe,… basi hayo ndo tunataka tuyamalize,” alisema Karume.

  Alisema anaamini kuwa yeye na Seif ndio viongozi wakubwa Zanzibar hivyo hatua yao ya kuamua kumaliza tofauti zao za kisiasa itasaidia kuchochea maendeleo ya visiwa hivyo.

  Katika hali ambayo haikuzoeleka hapo awali kwa viongozi hao wa CUF wote kwa pamoja walimpongeza Rais Karume kwa kutunukiwa shahada hiyo ya heshima na kusema kuwa alistahili kutokana na juhudi zake za kuvipatia visiwa hivyo amani na maendeleo.

  Katika siku za nyuma viongozi hao wa CUF, walionekana kupinga na kukejeli kila kitu kilichokuwa kikifanywa na Serikali ya Mapinduzi na wakati mwingine hata vilivyokuwa vikifanywa na Serikali ya Muungano.

  Kwa upande wake Karume alisema kwa sasa wameamua kuachana na siasa ya zamani na kuwa lengo lao ni moja tu la kuipigania Zanzibar na wananchi wake.

  Alisema wameamua kushirikiana ili kuhakikisha kuwa chaguzi mbalimbali zinazo fanyika visiwani humo, haziwi chanzo cha mitafaruku bali kuwaunganisha wazanzibari.

  Chama cha Wananchi CUF kila wakati kimekuwa kikipinga matokeo yatokanayo na chaguzi mbalimbali hali ambayo wakati mwingine ilisababisha umwagikaji wa damu visiwani humo.

  Katika siku za hivi karibuni kulikuwa kunamsuguano mkubwa uliohusu uandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura, hali iliyofanya CFU kutisha umwagikaji mwingine wa damu endapo matakwa yake yasingetekelezwa.

  Kutoka Dodoma, Umoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu Mkoani Dodoma jana walifanya maandamano ya kukipongeza Chama Cha Wananachi (CUF) kwa uamuzi wa kumtambua rais wa Zanzibar huku kukiwa na ulinzi mkali wa Polisi.

  Maandamano hayo yalianzia katika viwanja vya bunge mjini Dodoma
  yalipokelewa na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Hamad Rashid Mohamed katika viwanja wa Mwalimu Nyerere maarufu kama Nyerere Square.

  Hata hivyo tofauti na ilivyotarajiwa wakati maanadamano hayo yalipotangazwa na vyombo vya habari, jana wanafunzi waliojitokeza katika maanadamano hayo walikuwa ni wachache sana idadi ambayo haikuzidi wanafunzi 50.

  Katika maanadamano hayo wabunge wanne chama cha CUF walifika kwa ajili ya kuwaunga mkono wanafuzni hao ambao walikuwa pamoja na wananchi wachache waliojitokeza.

  Wabunge waliokuja mjini hapa jana ni pamoja na Dk Ali Taarabu Ali (Konde),Habibu Juma Mnyaa (Mkanyageni) Salimu Hemedi (Chambani) pamoja na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ambae alikuwa mgeni rasmi.

  Wabunge hao licha ya kuzungumzia mustakabali mzima wa mazungumzo ya Karume na Seif Shalifu Hamadi, walitumia muda mwingi katika kusifia chama  kwa madai kuwa ndicho chama pekee cha upinzani Tanzania.

  “Tangu kuingia kwa mfumo wa siasa za vyama vingi CUF tumekuwa tukiongeza idadi ya wakilishi pamoja na kuibuka na ushindi mkubwa katika uchaguziwa serikali za Mitaa katika ameneo mbalimbali nchini hiyo ni dalili kuwa sisi ndio wapinzani pekee hapa Tanzania,” alisema Dk Taarabu.

  Kwa upande wake Mnyaa alisema kuwa chama hicho kinachohitaji siasa safi na sio siasa za kuibiana kura kila unapofika uchaguzi.

  Mnyaa pia alikosoa mapungufu ya vyama vyote ikiwemo CCM na Cuf kwa kusema kuwa hayana tija kwa wananchi wan chi masikini kama Tanzania.

  Kwa ccm alisema kosa lao kubwa ni kitendo cha chama hicho kuamini kuwa kinaweza kila kitu na kwamba hakuna chama kingine kinachoweza kufanya jambo lolote isipokuwa wao hali ambayo alisema inatokana na mawazo finyu.

  Aliyataja mapungufu ya cuf kuwa ni pamoja na imani kuwa hakuna kilichofanyika ndani ya ccm wakati yapo mambo mazuri ambayo chama hicho tawala kilishayafanya na hivyo akaomba hayo yaliyofanywa mazuri ni budi yaheshimiwe na kuenziwa.

  Akizungumza katika mkutano huo kioongozi wa kabi ya upinzani bungeni aliwataka wanafunzi kutumia elimu yao na maarifa kwa ajili ya kudai mabadiliko ya katiba.

  “Tanzania tunahitaji mabadiliko makubwa sana na kusema kweli ninyi wasomi ndio mtakaoleta mabadiliko hayo hivi inawaingia akilini kweli uchaguzi kama huu uliofanyika hivi karibuni kusimamiwa na ofisi ya Waziri Mkuu katiba hii inamapungufu makubwa sana,” alisema Mohamed.

  Alitumia muda huo pia kuwataka wanafunzi pamoja na Watanzania kuendelea kumpigia debe mwenyekiti wa chama hicho Prof Ibrahim Lipumba kuwa bado anazo sifa za kugombea urais wa nchi. Kiongozi huyo alisema kuwa Lipumba ameshaanza kufahamika na wananchi hivi sasa na hivyo wawapuuze wale wanaosema kuwa asigombee urais kwa kisingizio cha kuwa ameishiwa sera jambo alilosema kuwa hata Viongozi wengi barani Afrika huingia kwa kutambulika kwanza.
   
 2. Jerome

  Jerome Senior Member

  #2
  Nov 16, 2009
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mambo ya mshiko hayo achana nayo,Seif kawa laini kama wali wa nazi na atamsindikiza hata kuchukua form ya uchaguzi nadhani safari ya kurudi CCM imeiva au anataka nyongeza ya mafao?
   
Loading...