Sehemu za kutembelea hapa Dar

Kama unaweza jaribu camping siku 1 utaenjoy. Fanya na marafiki cost sharing, haizidi elfu 80 hapo hadi kula, hiking, camping, boat, yaani alot utaenjoy madam.
Hebu anaetaka camping aje PM twende sio lazima awe KE hata mkiwa ME fresh tu

tuwe mtu 4 twendeni hii coming weekend Jumapili, Mad Max hebu nielekeze

mgeni ninaetokea Hapa Mbezi Mwisho,nielekeze napita njia ipi hadi nifike nipe idea idea

halafu ntajazia jazia nyama na Google Map,Last sunday niliboeka kinoma ikabd nifanye tour ya kuzunguka Dar nzima kuhakikisha tu ule mshale wa mafuta unatoka kwenye full unainama kidogo,ndio ikawa mwisho wa tour yangu.

Jumapili ijayo nataka nijaribu tena huko...
 
Bei zao nzuri sana and very fair.
Napenda sana adventure za hivyo
Nimependa option ya kwenda na msosi wako as najifungashia wa kutosha
Kuna kuogelea?

Lavit njoo uone mambo yako
 
Wale wanaoenda ushoroba nakumbusha msisahau kubeba camping mattress ya dharula, pod tent wanazo, unaweza beba camping stove ndogo maana unaweza andaa chakula mwenyewe hukohuko vile simple, anyway pametulia sana nililala mara moja nilitoka akili ikiwa mpya,
 
Zifuatazo ni Beach Safi,maji Safi na privacy kubwa katika visiwa vya Dar

-Sinda -kigamboni,panda boti kutokea barakuda au Kipepeo hotel Nauli
20,000(go return) msipungue wanne.

-Bongoyo- Nauli boti 30000 (go-return)
Misitu na sauti za ndege na fukwe za zisizo na watu wengi (pandia boti Msasani Slipway)

-Mbudya-Nauli 10000 ( go+return)
(Beach zote hizo utalipa 10000 kiingilio)/mwanafunzi 5000)
uzuri wake hizo fukwe hiyo pesa utaona ndogo(Hiki ni kisiwa wanakopenda kutembelea wasanii,Wafanyakazi wa kampuni za kimataifa,wanafunzi wa vyuo)
-ukiwa na hema lako unalala huko 54,000

Funguyasini - Hiki kisiwa ambacho unaweza kusema "mchanga unaelea juu ya maji" Si kwamba unaelea ila ukiipeleka familia yako huku watafurahi na hawatasahau hio trip.-Pandia boti Whitesand hotel utasimulia hutaamini uko Tanzania hii,ni zaidi ya Maldives watoto watacheza na ndege hapo utafurahi mwenyewe,kisiwa kipana sana mchanga tupu maji ya kwenye ugoko,kifua,magoti watoto watacheza bila hofu yeyote

Kumbuka beach dress ili ufurahi zaidi bukta,pensi,T-shirt or beach shirt,vest,sandals ambazo zikiloa maji hazina shida,miwani Kama utapenda kwa sababu ya mchanga mweupe,kofia
 
Mmh uku ndo walishoot MOVIE YA BWAWA LA SHETANI kila la kheri wakuu
Mnh naona unatupia ndoa ki dizian flani hiviiii.... Ila nimekue
Mnnnh naona unatupia ndoano ki dizian flan hivi ii tusiku shtukie.. Ila nimekuelewa
 
Ahaaa unataka kelele?
Nenda Juliana😂
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…