Sehemu ya maelezo ya dereva wa Lissu yanazidi kuibua maswali mengi. Polisi wamhoji hata kwa nguvu

Nimesoma kwa makini taarifa hiyo ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii huku chanzo chake kikitajwa kuwa ni gazeti ambalo hata hivyo jina lake halikubainishwa. Taarifa hii inaibua maswali mengi machache ni haya:

1. Maelezo ya awali kutoka viongozi wakuu wa CHADEMA walisema gari ni moja aina ya Nissan Patrol na kwamba namba zake hazikujulikana. Leo dereva Simon anasema ni magari mawili tena akibainisha kuwa namba za Nissan Patrol ni T 932 AKN. Dereva Simon aliwadanganya Viongozi wake? Alifanya hivyo ili iweje? Namba za Land Cruiser ni zipi?

2. Kwanini alichelewa kumpa Mh. Lisssu taarifa ya kufuatiliwa na magari hayo kuanzia Bungeni na kusubiri mpaka wafike nyumbani wakati wa kushuka jambo ambalo pengine lingesaidia bosi wake kuwa na mawazo mbadala juu ya hatua za kuchukua? Kwanini aliegesha gari kwa namna ambayo ilisaidia kurushiwa risasi Mhe. Lissu kirahisi wakati angeweza kuegesha vinginevyo na hivyo wahalifu wakashindwa kutekeleza lengo lao?
3. Eti akashuka mtu akijifanya kuongea na mtu kwa njia ya mikono, baada ya muda mfupi akarudi kwenye gari , gari la watu hao likiwa limegeuzwa kuangalia lilikotoka ndipo akashuka mtu huyo na silaha aina ya SMG. Muda wote huyo amemzuia Mhe. Lissu ashishuke, kwanini? , kulikuwa na nini hapo? Kulikuwa na umbali gani kutoka kwenye gari kuingia ndani ya nyumbani mpaka washindwe kuondoka?

4. Kwanini amlaze bosi wake kwenye kiti chake lakini yeye ajifiche uvunguni mwa gari lingine lililokuwa limeegeshwa pembeni? Lissu alikuwa anaendeshwa na Dereva kama roboti? Yeye hakutaka kujiongeza? Siyo kwamba huyu Dereva aliandaliwa kitaalam namna ya kumjengea hofu Lissu ili ashindwe kuchukua maamuzi sahihi ya kujiokoa?

5. Eti mmoja wa watu waliomshambulia Lissu walikutana Rose Garden, kwamba aliwatambua kwa vile walishuka kwenye gari lililokuwa linawafuatilia. Je baada ya kuwaona huko Rose Garden alichukua hatua yoyote kuweza kuwatambua , kutoa taarifa yoyote au hata kumjulisha Mhe. Lissu kuwa amewaona watu waliokuwa wakitumia gari lililokuwa likiwafuatilia? Kama jibu ni hapana, siyo kwamba alikutana na watu hao kupanga njama za yeye kusaidia kudhuriwa kwa Bosi wake?

6. Dereva Simon anasema gari lililokuwa na wahalifu lilikuwa limepaki pembeni mwa gari lao(maana yake ni karibu sana) na kwamba silaha iliyotumika ni SMG. Kwa mujibu wa wataalam wa silaha, SMG ina uwezo wa kujeruhi umbali wa mita 1000, Kwa umbali kati ya gari la Lissu na wahalifu ni wazi kama silaha ilikuwa SMG, risasi zingine zingeweza kupita tumboni mwa Lissu na kutoka nje na hata kutoboa gari , je zipo risasi za aina hiyo zilionekana kupenya tumboni na kwenda nje?

Maswali ni mengi sana. Lakini jambo muhimu kwa jinsi huyu Dereva anavyojichanganya, alitakiwa ajieleze Polisi kwa amri tena akiwa ametiwa pingu.
Nyie watetezi wa wauaji mnaingiza siasa bure tu!
Nape kaongea hivyo hivyo kwa nini police hawamhoji?

Double standard
 
Waliochangia uzi huu weengi wao wanaendeshwa na mihemko . ......binafsi najiuliza hilo swali namba mbili sipati jibu
 
Ukweli huyu dereva kaandaliwa hayo maelezo. Na ni suspect namba moja pamoja na Mh. Mbowe. Inabidi wawakamate kupitia interpol ili warudi watoe maelezo vizuri. Nadhani Mh. Mbowe na Mh. Lowasa huu mchezo wanaujua vizuri. Serikali yetu haiwezi kuua mtu kwa kiwango cha namna hii, na hawana rekodi huko nyuma za uharifu.
We ni fifiemu?!
 
Hawa wanafanya ujanja watajiumbu wao tu..

Huyo dereva alibeba nguo inazodaiwa ni damu ya Lissu
Ila yeye hama damu sehemu ambazo lazima zingekuwepo.. kama alimsaidia kumtoa kwenye gari au sijui alimshika kama takataka kumtoa asimguse mwili wake!!! sijui aliita watu wambebe na yeye kusubiri avuliwe nguo apewe halafu zinguse kidogo chini kwa shati..alipata muda wa kubadili nguo wapi au nani alimpa shati au alifikiria kubadili shati awe msafi aende hospitali.. kashika nguo wanazodai ni damu ya Lissu!!!! Maana hii kitu inamengi shaaaa

View attachment 590007
tapatalk_1505313730274.png

Mimi unanichanganya kabisa sielewi hata kidogo
 
kati ya watu ambao hawakutakiwa kuachwa wakizululazulula ni huyu Dereva yeye alitakiwa awepo kwenye chumba maalumu cha mahojiano tangu siku ile ya tukio maana Kwa anavyo toatoa taarifa hovyo bila kuchukua tahadhali ni mbaya sana Kwa usalama wake maana wauaji wanaweza kuhisi huyu Dereva anawafahamu nafikiri wakishajua hilo mnafahamu nini kinafuata!! again ni weakness ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kumuacha Dereva huyu atoe taarifa nyeti kiasi hicho mwenye mitandao ya kijamii wahusika plz mka mu interrogate huyu jamaa kuna kitu anakijua huyu....
 
Ukweli huyu dereva kaandaliwa hayo maelezo. Na ni suspect namba moja pamoja na Mh. Mbowe. Inabidi wawakamate kupitia interpol ili warudi watoe maelezo vizuri. Nadhani Mh. Mbowe na Mh. Lowasa huu mchezo wanaujua vizuri. Serikali yetu haiwezi kuua mtu kwa kiwango cha namna hii, na hawana rekodi huko nyuma za uharifu.
Nani alikwambia hao watu wasiojulikana ni watu was kitengo cha serikali huo ni wasi wasi wako tu.
 
Nimesoma kwa makini taarifa hiyo ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii huku chanzo chake kikitajwa kuwa ni gazeti ambalo hata hivyo jina lake halikubainishwa. Taarifa hii inaibua maswali mengi machache ni haya:

1. Maelezo ya awali kutoka viongozi wakuu wa CHADEMA walisema gari ni moja aina ya Nissan Patrol na kwamba namba zake hazikujulikana. Leo dereva Simon anasema ni magari mawili tena akibainisha kuwa namba za Nissan Patrol ni T 932 AKN. Dereva Simon aliwadanganya Viongozi wake? Alifanya hivyo ili iweje? Namba za Land Cruiser ni zipi?

2. Kwanini alichelewa kumpa Mh. Lisssu taarifa ya kufuatiliwa na magari hayo kuanzia Bungeni na kusubiri mpaka wafike nyumbani wakati wa kushuka jambo ambalo pengine lingesaidia bosi wake kuwa na mawazo mbadala juu ya hatua za kuchukua? Kwanini aliegesha gari kwa namna ambayo ilisaidia kurushiwa risasi Mhe. Lissu kirahisi wakati angeweza kuegesha vinginevyo na hivyo wahalifu wakashindwa kutekeleza lengo lao?
3. Eti akashuka mtu akijifanya kuongea na mtu kwa njia ya mikono, baada ya muda mfupi akarudi kwenye gari , gari la watu hao likiwa limegeuzwa kuangalia lilikotoka ndipo akashuka mtu huyo na silaha aina ya SMG. Muda wote huyo amemzuia Mhe. Lissu ashishuke, kwanini? , kulikuwa na nini hapo? Kulikuwa na umbali gani kutoka kwenye gari kuingia ndani ya nyumbani mpaka washindwe kuondoka?

4. Kwanini amlaze bosi wake kwenye kiti chake lakini yeye ajifiche uvunguni mwa gari lingine lililokuwa limeegeshwa pembeni? Lissu alikuwa anaendeshwa na Dereva kama roboti? Yeye hakutaka kujiongeza? Siyo kwamba huyu Dereva aliandaliwa kitaalam namna ya kumjengea hofu Lissu ili ashindwe kuchukua maamuzi sahihi ya kujiokoa?

5. Eti mmoja wa watu waliomshambulia Lissu walikutana Rose Garden, kwamba aliwatambua kwa vile walishuka kwenye gari lililokuwa linawafuatilia. Je baada ya kuwaona huko Rose Garden alichukua hatua yoyote kuweza kuwatambua , kutoa taarifa yoyote au hata kumjulisha Mhe. Lissu kuwa amewaona watu waliokuwa wakitumia gari lililokuwa likiwafuatilia? Kama jibu ni hapana, siyo kwamba alikutana na watu hao kupanga njama za yeye kusaidia kudhuriwa kwa Bosi wake?

6. Dereva Simon anasema gari lililokuwa na wahalifu lilikuwa limepaki pembeni mwa gari lao(maana yake ni karibu sana) na kwamba silaha iliyotumika ni SMG. Kwa mujibu wa wataalam wa silaha, SMG ina uwezo wa kujeruhi umbali wa mita 1000, Kwa umbali kati ya gari la Lissu na wahalifu ni wazi kama silaha ilikuwa SMG, risasi zingine zingeweza kupita tumboni mwa Lissu na kutoka nje na hata kutoboa gari , je zipo risasi za aina hiyo zilionekana kupenya tumboni na kwenda nje?

Maswali ni mengi sana. Lakini jambo muhimu kwa jinsi huyu Dereva anavyojichanganya, alitakiwa ajieleze Polisi kwa amri tena akiwa ametiwa pingu.
Kwa mfano Kama ingekuwa wewe ungefanyaje
 
Ukweli huyu dereva kaandaliwa hayo maelezo. Na ni suspect namba moja pamoja na Mh. Mbowe. Inabidi wawakamate kupitia interpol ili warudi watoe maelezo vizuri. Nadhani Mh. Mbowe na Mh. Lowasa huu mchezo wanaujua vizuri. Serikali yetu haiwezi kuua mtu kwa kiwango cha namna hii, na hawana rekodi huko nyuma za uharifu.
Ha! ha! Just ha! ha!

Kama kweli mnajua Serikali haihusiki.

Kwa nini mumeshindwa kukamata hiyo Nissan nyeupe?

Kwa nini mlishindwa kuchukua maelezo ya dereva siku ya tukio?

Walinzi wa eneo la area D mumewahoji? Wametoa majibu gani?

Kwa nini mnakataa kuruhusu uchunguzi huru wa kimataifa(Scotland)?

Kwa nini mnakataza watu kusoma dua za maombi?
 
mbona uko ``so deffensive`` ...wewe ndo mmiliki wa hiyo gari?

Hata mimi ananishangaza kuwashwawashwa huku anakutoa wapi. Acha vyombo vifanye kazi yake. Kama wanashida na maelezo yake watumie hata interpol kumhoji hukohuko nairobi au watume mtu.

Tatizo kwetu upelelezi huwa ni kutisha na kitupwa ndani.
 
Back
Top Bottom