Sehemu ya maelezo ya dereva wa Lissu yanazidi kuibua maswali mengi. Polisi wamhoji hata kwa nguvu

Nimesoma kwa makini taarifa hiyo ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii huku chanzo chake kikitajwa kuwa ni gazeti ambalo hata hivyo jina lake halikubainishwa. Taarifa hii inaibua maswali mengi machache ni haya:

1. Maelezo ya awali kutoka viongozi wakuu wa CHADEMA walisema gari ni moja aina ya Nissan Patrol na kwamba namba zake hazikujulikana. Leo dereva Simon anasema ni magari mawili tena akibainisha kuwa namba za Nissan Patrol ni T 932 AKN. Dereva Simon aliwadanganya Viongozi wake? Alifanya hivyo ili iweje? Namba za Land Cruiser ni zipi?

2. Kwanini alichelewa kumpa Mh. Lisssu taarifa ya kufuatiliwa na magari hayo kuanzia Bungeni na kusubiri mpaka wafike nyumbani wakati wa kushuka jambo ambalo pengine lingesaidia bosi wake kuwa na mawazo mbadala juu ya hatua za kuchukua? Kwanini aliegesha gari kwa namna ambayo ilisaidia kurushiwa risasi Mhe. Lissu kirahisi wakati angeweza kuegesha vinginevyo na hivyo wahalifu wakashindwa kutekeleza lengo lao?
3. Eti akashuka mtu akijifanya kuongea na mtu kwa njia ya mikono, baada ya muda mfupi akarudi kwenye gari , gari la watu hao likiwa limegeuzwa kuangalia lilikotoka ndipo akashuka mtu huyo na silaha aina ya SMG. Muda wote huyo amemzuia Mhe. Lissu ashishuke, kwanini? , kulikuwa na nini hapo? Kulikuwa na umbali gani kutoka kwenye gari kuingia ndani ya nyumbani mpaka washindwe kuondoka?

4. Kwanini amlaze bosi wake kwenye kiti chake lakini yeye ajifiche uvunguni mwa gari lingine lililokuwa limeegeshwa pembeni? Lissu alikuwa anaendeshwa na Dereva kama roboti? Yeye hakutaka kujiongeza? Siyo kwamba huyu Dereva aliandaliwa kitaalam namna ya kumjengea hofu Lissu ili ashindwe kuchukua maamuzi sahihi ya kujiokoa?

5. Eti mmoja wa watu waliomshambulia Lissu walikutana Rose Garden, kwamba aliwatambua kwa vile walishuka kwenye gari lililokuwa linawafuatilia. Je baada ya kuwaona huko Rose Garden alichukua hatua yoyote kuweza kuwatambua , kutoa taarifa yoyote au hata kumjulisha Mhe. Lissu kuwa amewaona watu waliokuwa wakitumia gari lililokuwa likiwafuatilia? Kama jibu ni hapana, siyo kwamba alikutana na watu hao kupanga njama za yeye kusaidia kudhuriwa kwa Bosi wake?

6. Dereva Simon anasema gari lililokuwa na wahalifu lilikuwa limepaki pembeni mwa gari lao(maana yake ni karibu sana) na kwamba silaha iliyotumika ni SMG. Kwa mujibu wa wataalam wa silaha, SMG ina uwezo wa kujeruhi umbali wa mita 1000, Kwa umbali kati ya gari la Lissu na wahalifu ni wazi kama silaha ilikuwa SMG, risasi zingine zingeweza kupita tumboni mwa Lissu na kutoka nje na hata kutoboa gari , je zipo risasi za aina hiyo zilionekana kupenya tumboni na kwenda nje?

Maswali ni mengi sana. Lakini jambo muhimu kwa jinsi huyu Dereva anavyojichanganya, alitakiwa ajieleze Polisi kwa amri tena akiwa ametiwa pingu.

Hizi habar umesaidiwa kuandika au?
Swala la kufuatiliwa halikuanza siku hiyo, hiyo Hali walishakutana nayo mara nyingi sana na hata kwenye hotuba ya lisu alitaja mpaka namba ya hilo gari je polisi walichukua hatua gan? Kama bavicha waliandika barua polisi wewe ulitaka hiyo siku Dereva na lisu Watoe taarifa mbinguni? Wapi angekuwa salama zaidi ni ndani ya gari au nje ya gari? Uhai wake umesaidiwa na gari angetoka tu ungekuta mazishi yake tayari.
Sijaona sababu ya wewe kuandika haya! Ni vema basi kama hujui kinachoendelea ukae kimya kabisa .
 
Nimesoma kwa makini taarifa hiyo ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii huku chanzo chake kikitajwa kuwa ni gazeti ambalo hata hivyo jina lake halikubainishwa. Taarifa hii inaibua maswali mengi machache ni haya:

1. Maelezo ya awali kutoka viongozi wakuu wa CHADEMA walisema gari ni moja aina ya Nissan Patrol na kwamba namba zake hazikujulikana. Leo dereva Simon anasema ni magari mawili tena akibainisha kuwa namba za Nissan Patrol ni T 932 AKN. Dereva Simon aliwadanganya Viongozi wake? Alifanya hivyo ili iweje? Namba za Land Cruiser ni zipi?

2. Kwanini alichelewa kumpa Mh. Lisssu taarifa ya kufuatiliwa na magari hayo kuanzia Bungeni na kusubiri mpaka wafike nyumbani wakati wa kushuka jambo ambalo pengine lingesaidia bosi wake kuwa na mawazo mbadala juu ya hatua za kuchukua? Kwanini aliegesha gari kwa namna ambayo ilisaidia kurushiwa risasi Mhe. Lissu kirahisi wakati angeweza kuegesha vinginevyo na hivyo wahalifu wakashindwa kutekeleza lengo lao?
3. Eti akashuka mtu akijifanya kuongea na mtu kwa njia ya mikono, baada ya muda mfupi akarudi kwenye gari , gari la watu hao likiwa limegeuzwa kuangalia lilikotoka ndipo akashuka mtu huyo na silaha aina ya SMG. Muda wote huyo amemzuia Mhe. Lissu ashishuke, kwanini? , kulikuwa na nini hapo? Kulikuwa na umbali gani kutoka kwenye gari kuingia ndani ya nyumbani mpaka washindwe kuondoka?

4. Kwanini amlaze bosi wake kwenye kiti chake lakini yeye ajifiche uvunguni mwa gari lingine lililokuwa limeegeshwa pembeni? Lissu alikuwa anaendeshwa na Dereva kama roboti? Yeye hakutaka kujiongeza? Siyo kwamba huyu Dereva aliandaliwa kitaalam namna ya kumjengea hofu Lissu ili ashindwe kuchukua maamuzi sahihi ya kujiokoa?

5. Eti mmoja wa watu waliomshambulia Lissu walikutana Rose Garden, kwamba aliwatambua kwa vile walishuka kwenye gari lililokuwa linawafuatilia. Je baada ya kuwaona huko Rose Garden alichukua hatua yoyote kuweza kuwatambua , kutoa taarifa yoyote au hata kumjulisha Mhe. Lissu kuwa amewaona watu waliokuwa wakitumia gari lililokuwa likiwafuatilia? Kama jibu ni hapana, siyo kwamba alikutana na watu hao kupanga njama za yeye kusaidia kudhuriwa kwa Bosi wake?

6. Dereva Simon anasema gari lililokuwa na wahalifu lilikuwa limepaki pembeni mwa gari lao(maana yake ni karibu sana) na kwamba silaha iliyotumika ni SMG. Kwa mujibu wa wataalam wa silaha, SMG ina uwezo wa kujeruhi umbali wa mita 1000, Kwa umbali kati ya gari la Lissu na wahalifu ni wazi kama silaha ilikuwa SMG, risasi zingine zingeweza kupita tumboni mwa Lissu na kutoka nje na hata kutoboa gari , je zipo risasi za aina hiyo zilionekana kupenya tumboni na kwenda nje?

Maswali ni mengi sana. Lakini jambo muhimu kwa jinsi huyu Dereva anavyojichanganya, alitakiwa ajieleze Polisi kwa amri tena akiwa ametiwa pingu.
Sijakuelewa tena aswa hapo ulipozungumzia smg ndo kabisa hujui kitu umekalili tu kuwa inaweza kuzuru kuanzia mita 100 huhuhuhuhuu kama hujui kaa kimya hoji mengine tu... smg sio fani yako u better stay shut na sio kukimbia kuandika uzi.. unajua gari lina body ya bati ya aina gani?? Ingekuwa walikuwa mita 100 isingeweza kuingia tumboni mwa lissu hzo risasi!! Kwa taarifa yako hata upepo unaweza punguza makali na kasi ya risasi itakuwa body ya gari???... ulianza vizuri mwishoni ukaonyesha muemko wa ki lumumba
 
Acha kudandia habari,umesema habari hii imeenea ktk mitandao ya jamii,lakini ukasema habari hii IPO ktk gazeti ambalo wewe hulijuwi.Mambo haya hufanywa na watoto au wagonjwa wa akili maana sitarajii kwa mtu anayejitambua akaandika kitu ambacho chanzo chake hakijuwi.
 
Ukweli huyu dereva kaandaliwa hayo maelezo. Na ni suspect namba moja pamoja na Mh. Mbowe. Inabidi wawakamate kupitia interpol ili warudi watoe maelezo vizuri. Nadhani Mh. Mbowe na Mh. Lowasa huu mchezo wanaujua vizuri. Serikali yetu haiwezi kuua mtu kwa kiwango cha namna hii, na hawana rekodi huko nyuma za uharifu.
Kweli kabisa,hata Nape alitshiwa bastola na mtu asiyejulikana,clouds pia wasiojulikana.Wasichafuwe serikali yetu,maana haiwezi kufanya haya,bali haya hufanywa na watu wasiojulika ambao haitakiwi kusomewa albadiri.
 
Waungwana tuwe na subira katika kipindi hiki.......

Kitu pekee cha muhimu kwa sasa ni kuombea hali ya Lissu itengemae......

Kitu muhimu kwa sasa ni uhai wa Lissu......
 
Nimesoma kwa makini taarifa hiyo ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii huku chanzo chake kikitajwa kuwa ni gazeti ambalo hata hivyo jina lake halikubainishwa. Taarifa hii inaibua maswali mengi machache ni haya:

1. Maelezo ya awali kutoka viongozi wakuu wa CHADEMA walisema gari ni moja aina ya Nissan Patrol na kwamba namba zake hazikujulikana. Leo dereva Simon anasema ni magari mawili tena akibainisha kuwa namba za Nissan Patrol ni T 932 AKN. Dereva Simon aliwadanganya Viongozi wake? Alifanya hivyo ili iweje? Namba za Land Cruiser ni zipi?

2. Kwanini alichelewa kumpa Mh. Lisssu taarifa ya kufuatiliwa na magari hayo kuanzia Bungeni na kusubiri mpaka wafike nyumbani wakati wa kushuka jambo ambalo pengine lingesaidia bosi wake kuwa na mawazo mbadala juu ya hatua za kuchukua? Kwanini aliegesha gari kwa namna ambayo ilisaidia kurushiwa risasi Mhe. Lissu kirahisi wakati angeweza kuegesha vinginevyo na hivyo wahalifu wakashindwa kutekeleza lengo lao?
3. Eti akashuka mtu akijifanya kuongea na mtu kwa njia ya mikono, baada ya muda mfupi akarudi kwenye gari , gari la watu hao likiwa limegeuzwa kuangalia lilikotoka ndipo akashuka mtu huyo na silaha aina ya SMG. Muda wote huyo amemzuia Mhe. Lissu ashishuke, kwanini? , kulikuwa na nini hapo? Kulikuwa na umbali gani kutoka kwenye gari kuingia ndani ya nyumbani mpaka washindwe kuondoka?

4. Kwanini amlaze bosi wake kwenye kiti chake lakini yeye ajifiche uvunguni mwa gari lingine lililokuwa limeegeshwa pembeni? Lissu alikuwa anaendeshwa na Dereva kama roboti? Yeye hakutaka kujiongeza? Siyo kwamba huyu Dereva aliandaliwa kitaalam namna ya kumjengea hofu Lissu ili ashindwe kuchukua maamuzi sahihi ya kujiokoa?

5. Eti mmoja wa watu waliomshambulia Lissu walikutana Rose Garden, kwamba aliwatambua kwa vile walishuka kwenye gari lililokuwa linawafuatilia. Je baada ya kuwaona huko Rose Garden alichukua hatua yoyote kuweza kuwatambua , kutoa taarifa yoyote au hata kumjulisha Mhe. Lissu kuwa amewaona watu waliokuwa wakitumia gari lililokuwa likiwafuatilia? Kama jibu ni hapana, siyo kwamba alikutana na watu hao kupanga njama za yeye kusaidia kudhuriwa kwa Bosi wake?

6. Dereva Simon anasema gari lililokuwa na wahalifu lilikuwa limepaki pembeni mwa gari lao(maana yake ni karibu sana) na kwamba silaha iliyotumika ni SMG. Kwa mujibu wa wataalam wa silaha, SMG ina uwezo wa kujeruhi umbali wa mita 1000, Kwa umbali kati ya gari la Lissu na wahalifu ni wazi kama silaha ilikuwa SMG, risasi zingine zingeweza kupita tumboni mwa Lissu na kutoka nje na hata kutoboa gari , je zipo risasi za aina hiyo zilionekana kupenya tumboni na kwenda nje?

Maswali ni mengi sana. Lakini jambo muhimu kwa jinsi huyu Dereva anavyojichanganya, alitakiwa ajieleze Polisi kwa amri tena akiwa ametiwa pingu.
Hiyo point ya mwisho hata mimi ndiyo nimeingiwa shaka, nilivyokuwa jeshini nillisoma hilo la umbali wa SMG kujeruhi maana yake risasi zote zisingebaki mwili hadi zije kutolewa mwilini. Umbali chini ya KM 1 inapita

Ila tusiongee sana juu ya hili wote tumesikia na hatukuona dhahiri
 
Kuna namna mbili za huyu Dereva kuwa Nairobi.........

Ni aidha kweli anapata tiba ya kisaikolojia baada ya kulishuhudia tukio hilo baya na la kutisha la kutaka kuwawa kwa boss wake....

Ama, CHADEMA nao wanafanya uchunguzi wao kabla ya "suspect number one - serikali" haijamchukua huyu bwana na ndiyo maana wamem retain Nairobi kwa kigezo kuwa naye anapata matibabu lakini wakikusanya data muhimu through him....

All in all, hata mimi kwa maelezo haya (kama kweli ni halisi na ni yake), ni wazi sana kuwa kuna maeneo mengi anajichanganya na kuleta mashaka makubwa kuwa inawezekana naye ni part of this deadly deal...!!
 
Waungwana tuwe na subira katika kipindi hiki.......

Kitu pekee cha muhimu kwa sasa ni kuombea hali ya Lissu itengemae......

Kitu muhimu kwa sasa ni uhai wa Lissu......

Yeah, muhimu ni uhai wa Tundu Lissu at least for now..

Lakini kuwapata wauaji hawa is also equally important kwa sbb kutokupatikana kwao sasa hawa wauaji hatutakuwa tunatatua tatizo..

Mwisho wataendelea kukamilisha orodha yao ya wale watu waliopanga kuwaua...

Scenario hii ni sawa tu na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu...

Una wagonjwa upande huu ukiwatibu na wakati huohuo ukidhibiti kuenea zaidi kwa ugonjwa huo!!
 
Coco chanel hata ukiangalia kwa macho ya kijani na mahaba ya kuongopa utaona damu kwenye seruali ya Dereva..angalia imeviliana sana tu kwa suruali. Jitahidi kuwa subjective japo hatuwapendi hawa wapinzani wetu
 
Wachangiaji wengi wa hii post wanachangia bila kuwa na "open mind"! Kifupi wengi wameshafikia conclusion ya tukio zima jambo ambalo nadhani sio sahihi sana!

Sisi ni binadamu na hapa duniani kuna changamoto nyingi sana zinazoweza kusababisha lolote kutokea hata ambalo kwa akili ya kawaida huwezi kudhani hata kwa asilimia chache kwamba lingewezekana!

Fikiria kuhusu haya yanayosemwa semwa kuhusu mzazi kumtoa kafara mwanaye au mtoto kumtoa kafara mzazi wake!! Unadhani hii kwa akili ya kawaida ya binadamu wa kawaida ni jambo la kuwezekanika kirahisi rahisi!?! Lakini je, haya hayatokei katika jamii zetu!? Wanaoyafanya mkipanda nao daladala utaona alama zao usoni!?!

Kwenye huu uso wa dunia lolote la weza kutokea hivyo kutazama jambo ukiwa na "open mind" ni vizuri zaidi kwani utaruhusu ubongo wako kuwaza ambayo hukuyategemea kuyaona kirahisi sana bila kuwa na tafakuri ya kina
 
Ukweli huyu dereva kaandaliwa hayo maelezo. Na ni suspect namba moja pamoja na Mh. Mbowe. Inabidi wawakamate kupitia interpol ili warudi watoe maelezo vizuri. Nadhani Mh. Mbowe na Mh. Lowasa huu mchezo wanaujua vizuri. Serikali yetu haiwezi kuua mtu kwa kiwango cha namna hii, na hawana rekodi huko nyuma za uharifu.
huwa mnaua kwa kiwango gan?
 
Back
Top Bottom