Sehemu ambayo haikupi uhuru sio sehemu sahihi

Mr George Francis

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2022
Posts
274
Reaction score
486
SEHEMU AMBAYO HAIKUPI UHURU SIO SEHEMU SAHIHI.

Maisha mazuri ni yale yanayokupa uhuru wa kuishi vile unavyotaka bila shinikizo kutoka upande wowote wa dunia.

Ikiwa katika mahusiano, kazi/ajira au katika maisha ya kila siku kama vile urafiki na familia unapoona hakuna uhuru using'ang'anie kubaki hapo.

Ifuatayo ni mifano mitatu ya mazingira ambayo hupaswi kubaki hapo kama hupati uhuru wa kufurahia maisha yako.

1. Katika Mahusiano (Urafiki, Mapenzi, Ndoa)
Ikiwa mtu au uhusiano wako unakunyima uhuru wa kufikiri, kutenda, kuamua na kutumia utashi elimu na maarifa uliyonayo hapo sio sehemu sahihi, ondoka haraka.

Mfano:
●Ikiwa kila wakati unahitaji "ruhusa" kufanya mambo ya kawaida.

●Ikiwa unaogopa kujieleza kwa hofu ya kugombana au kuachwa.

●Ikiwa inakulazimu kubadilika sana mara kwa mara ili kumridhisha mtu mwingine hadi unapoteza utambulisho wako.

●Ikiwa anatumia hadi uchawi au nguvu za giza ili uzidishe mapenzi kwake au vinginevyo nk.

Nikushauri tu kuwa hapo ndugu yangu sio sehemu sahihi kabisa.

Mahusiano mazuri ni yale yanayokupa amani ya moyo na uhuru wa kuwa wewe, sio kuwa mtumwa wa hisia za mtu mwingine.

Usikae kwenye mahusiano ya utumwa kwa sababu ya "tumetoka mbali" au "tuna mtoto/watoto" pekee.

Amani yako ya moyo inastahili zaidi kuliko hizo adithi za "tumetoka mbali" "nimemzoea" au "tuna mtoto/watoto."
Kama mtoto mtalea hata mkiwa mmeachana.

2. Katika Kazi au Biashara
Ikiwa kazi inakunyima uhuru wa kufikiri, kuwa mbunifu, kuendelea kujifunza, au hata kuwa na maisha nje ya ofisi bila kuteswa, basi sio sehemu inayokufaa kwa muda mrefu.

Mfano:
●Ikiwa unafanya kazi kwa hofu tu, sio kwa hamasa.
●Ikiwa mshahara haukidhi, lakini hata maendeleo au heshima haipatikani.
●Ikiwa unahisi kama "mfanyakazi tu", sio mtu mwenye thamani.

Nikushauri tu kwamba tafuta "exit plan" polepole. Jifunze skill mpya, weka akiba, anza side hustle, au tafuta kazi nyingine inayokupa nafasi ya kukua na uhuru wa kupambania ndoto zako.

Watu wengi baada ya kuacha kazi isiyowapa uhuru ndipo maisha yao yalipobadilika kweli to the next level na sasa wanaingiza kipato kikubwa pia wana amani na furaha ya moyo.

3. Katik Maisha kwa Ujumla
Sehemu inaweza kuwa mazingira, jamii, au hata tabia zako mwenyewe.

Ikiwa unahisi kama umefungwa, unanyanyasika au hauwezi kuishi katika uhalisia wako basi hapo sio sehemu sahihi kwako.

Nakushauri kwamba pendelea kujiuliza mara kwa mara: "Je, hapa ninapata amani, furaha na uhuru wa kuwa mimi?"

Ikiwa jibu ni "hapana" kwa muda mrefu basi anza hatua za kuondoka au kubadilisha mazingira.

Usiogope mabadiliko.

Maumivu ya kuondoka ni makali kwa muda mfupi lakini maumivu ya kukaa mahali pasipokufaa ni maumivu ya maisha yako yote.

NB: Sehemu sahihi = uhuru + amani + ukuaji.

Usikubali kuishi kwa "nusu uhuru" au "amani ya bandia."
Ukiachia sehemu isiyokufaa, utafungua nafasi kwa ile inayokustahili kweli.

Je, unahisi upande gani kati ya haya niliyokueleza hapa unakunyima uhuru wako?

Tuandikie kwenye comments, sote tujifunze.
AHSANTE.

#No_learnig_No_earning
So We Have To Learn.

Content By Mr. George Francis
 
Ukishazaliwa tu jua umeingia jela tayari huwezi kuwa huruma mpaka inaingia kaburini tena 😂 😅 😅 😅
 
Back
Top Bottom