Sefue: Tumemaliza kumchunguza Maswi

Sefue: Tumemaliza kumchunguza Maswi

MAHORO

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2013
Posts
7,585
Reaction score
2,571
.... Wadau, Ombeni Sefue Amesema Uchunguzi Wa Kamati Ya Maadili Ya Uma Dhidi Ya Kina Maswi Umekamilika. Ripoti Itawekwa Hadharani Mda Si Mrefu. Wasiwasi Wangu Ni Kwamba Watuhumiwa Wengi Kama Maswi Watasafiswa Na Kuonekana Hawakuhusika Kwenye Sakata La Escrow, Hii Ni Kwasababu Werema Alishasema Ahukumiwe Yeye Kwani Ndiye Alisababisha Hao Wengine Waingie Kwenye Kashfa Hiyo.. Yangu Macho, Mtanikumbuka.!
==========================

Takribani miezi minne baada ya kusimamishwa kazi kwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, uchunguzi wa awali kuhusu tuhuma za ushiriki wake katika kashfa ya Kampuni ya IPTL ya uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 200 katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), umekamilika.

Katibu Mkuu Kiongozi ambaye kisheria ndiye mwenye mamlaka ya nidhamu kwa watumishi wa umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwamo makatibu wakuu, Balozi Ombeni Sefue (pichani), alithibitisha jana kukamilika kwa uchunguzi huo.

Uchunguzi huo ulifanywa kwa upande mmoja na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kubaini kama kuna ukiukwaji wowote wa sheria ya maadili ya viongozi wa umma uliofanywa na Maswi katika sakata hilo.

Pia ulifanywa na kamati iliyoundwa na Balozi Sefue kuchunguza iwapo Maswi ametenda kosa la kinidhamu linalostahili hatua za kinidhamu kuchukuliwa dhidi yake.

Akizungumza na NIPASHE jana, Balozi Sefue alisema tayari ripoti zote mbili ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na ya kamati hiyo zimekwishawasilishwa katika ofisi yake baada ya uchunguzi kukamilika.

"Wameshakamilisha uchunguzi na ripoti zote mbili zimeshaandaliwa na zimeshakabidhiwa kwangu, tunaendelea kuzichambua. Tutakapokuwa tayari tutatoa taarifa," alisema Balozi Sefue.

Maswi alisimamishwa kazi kwa muda na Balozi Sefue, Desemba, 23 mwaka jana, ili kupisha uchunguzi huo.

Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo, Ngosi Mwihava, aliteuliwa kukaimu nafasi ya Maswi hadi uchunguzi huo utakapokamilika.

Kipindi anasimamishwa kazi, Maswi alikuwa kiongozi wa tatu kukumbwa na dhoruba inayotokana na sakata la Escrow baada ya kujiuzulu aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema Desemba 16, 2014 na kung'olewa aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka, Desemba 22, mwaka jana.

Baadaye, aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Prof. Sospeter Muhongo, naye alijiuzulu na Rais Jakaya Kikwete akamteua aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Simbachawene, kushika

Chanzo:Nipashe
 
.... Wadau, Ombeni Sefue Amesema Uchunguzi Wa Kamati Ya Maadili Ya Uma Dhidi Ya Kina Maswi Umekamilika. Ripoti Itawekwa Hadharani Mda Si Mrefu. Wasiwasi Wangu Ni Kwamba Watuhumiwa Wengi Kama Maswi Watasafiswa Na Kuonekana Hawakuhusika Kwenye Sakata La Escrow, Hii Ni Kwasababu Werema Alishasema Ahukumiwe Yeye Kwani Ndiye Alisababisha Hao Wengine Waingie Kwenye Kashfa Hiyo.. Yangu Macho, Mtanikumbuka.!

Safi sana ni habari njema kuisikia. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
 
.... Wadau, Ombeni Sefue Amesema Uchunguzi Wa Kamati Ya Maadili Ya Uma Dhidi Ya Kina Maswi Umekamilika. Ripoti Itawekwa Hadharani Mda Si Mrefu. Wasiwasi Wangu Ni Kwamba Watuhumiwa Wengi Kama Maswi Watasafiswa Na Kuonekana Hawakuhusika Kwenye Sakata La Escrow, Hii Ni Kwasababu Werema Alishasema Ahukumiwe Yeye Kwani Ndiye Alisababisha Hao Wengine Waingie Kwenye Kashfa Hiyo.. Yangu Macho, Mtanikumbuka.!
Tatizo la wanyarwanda ni watu wa ajabu sana,

kichwa cha andiko lako na andiko lenyewe wala havishabihiani kabisa,

Wewe unaweza kuonesha ushahidi usioshaka wapi maswi kahusuka,

mambo yenu ya huko Rwanda usituletee bana.
 
Sijawahi kuona alipohusika maswi hata chembe alisukiwa zengwe na wanasiasa tu pamoja na mafisadi.
 
Kwa hiyo wewe uliamini kwamba Maswi alitenda kosa? Hata mtu wa kawaida alikua kwamba Maswi hakutenda kosa. Akiwa kama mtendaji wa serikali aliomba muongozo toka ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali ambaye ndiye mwenye dhamana ya kuishauri serikali kuhusu masuala ya kisheria. Mwanasheria akampa mwongozo tena akamwambia afanye haraka serikali isije ikaingia katika matatizo; haya yapo kimaandishi, sasa Maswi angekaidi?
 
Sijawahi kuona alipohusika maswi hata chembe alisukiwa zengwe na wanasiasa tu pamoja na mafisadi.
Mambo yalivyoenda ilionekana Maswi hakuhusika lakini wajanja wachache waleeee, mafisadi wachache waleeee sijui walikula maharage ya wapi waleee wakamtungia zengwe Maswiiiiiiii ili wamuondoe paleeee wapate kufanya mambo yao kuleeee. Lakini kweli itamuweka huru Maswi.
 
Tatizo la wanyarwanda ni watu wa ajabu sana,

kichwa cha andiko lako na andiko lenyewe wala havishabihiani kabisa,

Wewe unaweza kuonesha ushahidi usioshaka wapi maswi kahusuka,

mambo yenu ya huko Rwanda usituletee bana.

.... Mkuu, Hata Kama Hakuhusika Moja Kwa Moja, Anatakiwa Kuwajibishwa Kwani Yeye Ndo Mtendaji Mkuu Wa Wizara. Alafu Ukome Kuniita Mnyarwanda, Ila Ningekua Mnyarwanda Hasa Mtutsi Ningefurah Sana
 
Sawa Maswi alihisikuna pesa za umma hapo na aliomba ushauri kwa AG Werema aliyesema pesa za Escrow zichotwe tena haraka!

Lakini mbona BoT kama msimamizi wa mabenki haitoi orodha ya waliochota pesa za Escrow kupitia Stanbic bank?
 
.... Wadau, Ombeni Sefue Amesema Uchunguzi Wa Kamati Ya Maadili Ya Uma Dhidi Ya Kina Maswi Umekamilika. Ripoti Itawekwa Hadharani Mda Si Mrefu. Wasiwasi Wangu Ni Kwamba Watuhumiwa Wengi Kama Maswi Watasafiswa Na Kuonekana Hawakuhusika Kwenye Sakata La Escrow, Hii Ni Kwasababu Werema Alishasema Ahukumiwe Yeye Kwani Ndiye Alisababisha Hao Wengine Waingie Kwenye Kashfa Hiyo.. Yangu Macho, Mtanikumbuka.!
Akirudishwa Prof Muhongo naye arudishwe
 
Kama hakuhusika inabidi napo afunguliwe mashitaka ya kutohusika kama mtendaji mkuu wa wizara ya nishati na madini.
hapa ndio huwa tunasema sisi watanzania ni wajinga hv inawezekana vp maswi hasihusike alafu waziri hausike,cha ajabu waziri anahusika alafu naibu waziri hausiki
 
Prof.mhongo na maswi waliwajibika kiutendaji lakn hakuna ushahidi wa kimgao wao kuhusika kama tibaijuka,chenge na ngelej
 
Pambafu mkubwa we mnyarwanda unaandika hisia zako badala ya report!
 
Liliulizwa swali: Fedha za Escrow ni za umma au za watu binafsi?
Jibu lililopatikana: Fedha hizo SIO za umma, ni binafsi.
Likaulizwa jingine: Kama sio za umma mbona alitumwa CAG mtumishi wa umma kuzikagua?
Jibu halikupatikana hadharani.
Likatwangwa swali jingine: Kama sio za umma mbona watumishi wa umma (Werema, Muhongo, Tibaijuka, Maswi na wengine) wanaadhibiwa kwa pesa isiyo ya umma?
Jibu haliwezi kujulikana.
Likaulizwa jingine: Kama waliochukua fedha kule Mkombozi Bank wanajulikana, je ni akina nani waliochukua sehemu ya fedha hizo kutokea Stanbic Bank?
Jibu lake halipo hata kwa ngumi.
Likaulizwa la mwisho: Je kuna hasara yoyote ambayo serikali imeingia kwa kadhia ya Escrow?
Jibu lake likatolewa fasta fasta tu: HAKUNA.

Haya jamani. Jitokezeni kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura siku yoyote likiletwa mitaa yenu.
 
Tatizo la wanyarwanda ni watu wa ajabu sana,

kichwa cha andiko lako na andiko lenyewe wala havishabihiani kabisa,

Wewe unaweza kuonesha ushahidi usioshaka wapi maswi kahusuka,

mambo yenu ya huko Rwanda usituletee bana.

wewe sungura tope chakula cha mafisadi naomba usituharibie majadiliano yetu
 
Tatizo la wanyarwanda ni watu wa ajabu sana,

kichwa cha andiko lako na andiko lenyewe wala havishabihiani kabisa,

Wewe unaweza kuonesha ushahidi usioshaka wapi maswi kahusuka,

mambo yenu ya huko Rwanda usituletee bana.

Haka kajamaa MAHORO nakafananisha na kale kajasusi ka kagame kaliko hamia bbc!
 
Last edited by a moderator:
.... Wadau, Ombeni Sefue Amesema Uchunguzi Wa Kamati Ya Maadili Ya Uma Dhidi Ya Kina Maswi Umekamilika. Ripoti Itawekwa Hadharani Mda Si Mrefu. Wasiwasi Wangu Ni Kwamba Watuhumiwa Wengi Kama Maswi Watasafiswa Na Kuonekana Hawakuhusika Kwenye Sakata La Escrow, Hii Ni Kwasababu Werema Alishasema Ahukumiwe Yeye Kwani Ndiye Alisababisha Hao Wengine Waingie Kwenye Kashfa Hiyo.. Yangu Macho, Mtanikumbuka.!

Hatakama atakuwa alihusika unadhani kipi kitatokea?
 
Back
Top Bottom