Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 18,016
- 24,964
Kama kura za hapana hazijaja kwa urahisi, je una uhakika gani kuwa kura za ndiyo zilikuja kwa urahisi? Fahamu kuwa hata Gordon Brown aliyewahi kuwa Chancellor of the exchequer na baadaye kuwa prime minister wa UK ni Msikotchi pia na ni kati ya waliopinga utengano. Tamaa ya madaraka ya huyu Bwana Alex Salmond ilileta gharama zisizokuwa za lazima kwa taifa lake kwani hiyo 45% za ndiyo zilipatikana kwa kampeini ya gharama kubwa sana. Nadhani ndiyo maana aliona aibu na kuamua kujiuzulu mara moja kuogopa asijekabiliwa na maswali ya kujibu huko mbeleni .