By Farrel Jnr Foum
Kura za hapana zilizoshinda leo hazijaja kwa urahisi maana ahadi za kurejesha mamlaka makubwa Scotland yataifanya nchi hii kuwa na mfumo mpya wa muungano wao. Bwana Alex Salmond namuona ni mwenye kipaji kikubwa na mwenye kujiamini, anajuwa anachokifanya na nina hakika hii ilikuwa ni one man war against vyama vyote vikuu, hata wakubwa waliostaafu na kubezwa katika siasa za nchi kama Gordon Brown naye pia alijitumbukiza kuhakiksha hawajitengi na umoja wao. Dunia nzima ilihamia Scotland kuhakikisha no vote inapatikana. Nakumbuka hata Bill clinton nae aliwasihi kutojitenga kwa vile madhara yake ni makubwa zaidi kwa alliance wa marekani wanaemtegemea.
Kura za asilimia 45 ni nyingi ukitazama namna gani alivyoshinda na establishment ya miaka 300 ya umoja wao. Lakini naamini hakufanya tu bila ya plan maalum ya kuhakikisha madai ya Scotland yanasikika vizuri upande wa pili na pia mabadilko makubwa zaidi ya matarajio ya wengi ya kimamlaka kwao yanapewa nguvu hasa pale wataposhindwa kujitenga. Kwa waskotish leo ni ushindi juu yao kwa vile miezi minane inayokuja tutaona namna gani mamlaka makubwa yakielekea North kuanzia masula ya fedha, kodi, na hata uwezo wa kupanga fiscal policy zao. Chancelor wa fedha anaporwa mamlaka makubwa ya maamuzi kuelekea devolution ya bunge la scotland huku hata mgao wa fedha kwa scotland ukiengezeka maradufu kuliko kwa waingereza wenyewe. Hio ndio cost ya umoja wao.
Projects kubwa kubwa kama za welfare na hata pension zitawanufaisha zaidi waskotish kutokana na mamlaka waliokubaliwa kupewa. Lakini kuna possibility kubwa kwa England nayo kupewa devolution ya bunge lake. Hili halina mjadala, ninaamini katika miezi minane ijayo kilio cha waingereza kitazidi kukuwa hasa baada ya UKIP kulivalia njuga suala zima la mamlaka makubwa kwa Scotland wakiwa si wapingaji bali wakidai nao usawa kwa bunge lao mahsusi kwa yale yaliokuwa hayamo katika umoja wao. Kwa sasa mamlaka waliopewa waskotish yatazidisha kelele za devolution kwa england ili kuepusha wabunge waskotland kuchangia masuala wasio yahusu ambayo kwa sasa yatazidi kuwa makubwa zaidi.
Wanaomdharau Alex Salmond hawajui strategies zake na za SNP walizozipanga, kwanza wataendelea kuwa madarakani kwa muda mrefu zaidi, kwa vile asilimia kubwa ya kura walizopata zinaonyesha wataweza kuunda serikali hasa kutokana na ukweli wa kutoiva kwa Labour na Tory katika uundaji wa serikali ya pamoja.
Pili wataendelea kuyatumia mamlaka watakayoongozewa kwa faida ya watu wao na zaidi kwamba wameweza kukidhi ahadi walioitoa ya kuleta referendum baada ya kuchaguliwa. Hili kwa upande wa uingereza chini ya uongozi wa Cameron linawaumiza kichwa kwa vile ahadi yao ya referendum kwa EU wameshindwa kuitekeleza kwa woga wa kushindwa na hata Labour pia anafahamu challenge zinazowakabili mbele yao.
Nilioyasoma kwa wenzetu:-
Kwanza ustaarabu walioutumia kuhakisha kampeni zao zinakwenda kisheria na kuheshimiana.
Pili uhuru wa maoni ya kila mmoja bila ya kufukuzana, kupandikiziana kesi na kutishana kwa uingiaji wa msituni kupinga ukuwaji wa maoni ya wananchi.
Tatu hakukuwa na matusi yalioelekezwa kwa aliekuja na kura ya maoni kwa sababu uhuru wa kusikiliza maoni ya wananchi unaheshimiwa na demokrasia ni nguzo ya utawala wenye nguvu.
Nne umoja umelindwa kwa kusikilizwa malalamiko yao na kuhakikisha unalindwa kwa kuwapa mamlaka yao waskotish wanayoyadai.
Tano kwa lolote lenye mashaka, njia bora ni kurejea kwa wananchi na kuweza kupata kauli moja kubwa ya kuondosha utata.
Sita wingi wa wabunge wa SNP katika scotland haukuwafanya kupindisha taratibu au kupandikiza maoni yao kwa jambo lenye nguvu ya wananchi, walikubali kulirejesha moja kwa moja kwa wananchi kusikiliza maoni yao.
Saba umoja wa kweli ni wa kuheshimiana, wa kufuata haki na usawa kwa kila upande.
Nane hata katika miungano mikubwa yenye faida kwa pande zote ikiwa hakuna haki, usawa, heshima na kusikilizwa kwa maoni ya wananchi hakuna guarantee ya kudumu kwa miungano hio.
Tisa tunapojadili faida za miungano tujikite katika uzito wa hoja si kelele za mchele wa mbeya na tashtiti za dharau kwa wengine. Khofu ya jeshi kuchukuwa nchi na tashtiti za kutuita wauza vitunguu haitasaidia kurejesha umoja tunaoutamani.
Kumi tunapopima faida za kuwepo kwa muungano tusidharau mchango wa sehemu nyengine kwa sababu ya udogo wake na udogo wa population yake. Uingereza inapopulation ya watu milio sitini, scotland milioni sita, ratio ya 6:1. Na kwetu pia milioni arobaini kwa milioni moja haiwapi haki walio,wengi na kuzima kwa wachache.
Nimalizie kwa waliofurahia referendum ya No vote kwa Scotland, wafahamu kwanza faida ya referendum ambayo kwa upande wetu imekuwa ikichezewa chezewa kisiasa.
Pili ikiwa referndum ya no vote ya 55% ni ya kupigiwa makofi na kupongezana, wakumbuke pia mabadiliko ya zanzibar ya katiba ya 2010 yalikuja na ushindi wa asilimia 66. Imagine kama No vote wangelipata ukubwa wa majority ya asilimia 66.
Wito wangu ni kwa wenye mamlaka kutuuliza nasi wananchi wa nchi hizi mfumo gani wa serikali tunaoutaka katika muungano na mabadiliko tunayoyatarajia. Tunahitaji kura ya maoni kutuuliza kwa uwazi muelekeo wetu sio vyama kubeba hatamu na matashi ya wananchi.