Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 16,310
- 33,784
UPOTOSHAJI KUHUSU KILICHOJIRI SCOTLAND
KURA NI ‘NO' MABADILIKO NI ‘YES'
UK KUBADILI MUUNDO WA MUUNGANO
TANZANIA, ULAGHAI, UBABAISHAJI NA UHUNI
Wanajamvi, Niwatake radhi kwa mabandiko marefu
Nyakati tulizo nazo haziruhusu kuacha vitu hewani
Wababaishaji, wapotoshaji na mashabiki hutumi mwanya huo kwa azama zao
Tangu matokeo ya kura ya maoni Scotland kutolewa, yamekuwepo maelezo ya kupotosha wananchi kwa kuficha ukweli wa kilichotokea
Kura ya maoni ya Uingereza imekuwa kielelezo cha mabadiliko katika tawala za dunia. Imechukuliwa kama kipimo ''yard stick''
Mfan, kuna nchi zinaiangalia Scotland kama mfano, Tanzania ikiwemo
Historia ya Uingereza ni ndefu, ikihusisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, muungano wa falme na mabadiliko yaliyofuata.
Hatutaweza kueleza kwa ukamilifu, tutachukua ya muhimu kwa ufahamu tu,wakati huu mazingira yetu yanapowiana na yaliyotokea.
Tuifahamu Uingereza kwa uchache.
Hili ni taifa kubwa lililomiliki makoloni mengi na hadi sasa.
Idadi ya watu ni Milioni 64, ikiwa na uchumi namba 6 duniani
Uingereza ni muungano wa falme kutoka nchi za England na Wale na Scotland zinazotengeneza Great Britain na North Ireland.
Muungano ni wa takribani miaka 300, ukiwa umepitia hatua za mageuzi na mabadiliko. Uingereza haina katiba, hutawali kwa constitutional monarchy.
Mfumo unaotawala ni Unitary system,serikali kuu yenye mamlaka.
Mfumo wao hujulikana kama Westminster
Pamoja na ufalme, Uingereza inaendeshwa kidemokrasia kwa mabunge 2(bicameral).
Bunge la Makabwela (House of common) na bunge la Mamwinyi(House of lords)
Unitary system huongoza nchi kama kituo kimoja(single unit), serikali kuu ikiwa imeshika hatamu
Mfumo wa Unitary unatumika na nchi nyingi duniani, nao pia umegawanyika
Uingereza ina Monarch unitary system malikia akiwa na mamlaka makuu.
Bunge la Mamwinyi limepunguziwa nguvu na sasa hudurusu sharia zitokazo katika bunge la Makabwela(House of Common) na kasha kuridhiwa na Malikia
Uteuzi wa house of lords hufanywa na malikia kwa ushauri wa waziri mkuu, au kamisheni maalumu inayomshauri malikia.
Mtindo wa uteuzi kwa urithi ‘herditary' umeondelewa.
Mageuzi hayo yalianzishwa na chama cha Labor wakati wa Tonny Blair
Kuna nchi zenye mfumo wa Unitary kama Uingereza, nyingine hufuata mfumo huo kama Repulic na hapa zipo nchi nyingi za common wealth ikiwemo Tanzania
Tofauti na unitary,mfumo wa confederation una malengo maalumu kama ulinzi ukiacha mamlaka kwa nchi husika, wakati Federal ni shirikisho litoalo mamlaka kwa washirika
Devolution ni mfumo unaotoa mamlaka kwa maeneo kama mikoa, serikali za mitaa au vinchi washirika kwa maana ya decentralization.
Hata hivyo serikali kuu inabaki kuwa na nguvu za kupangua sharia katika ngazi za chini.
Federalism ni mfumo ambao nguvu za washirika zipo kikatiba, na hapa tunasisitiza
Inaendelea…….
cc MwanaDiwani Nape Nnauye Alinda Mag3 Anna Tibaijuka HKigwangalla Dr.F.Ndugulile John Mnyika Remote JokaKuu gfsonwin Mwalimu Bongolander Kichuguu Buchanan Mwigulu Nchemba AshaDii Paul Makonda Gwalihenzi Kichuguu Ritz EMT MJINI CHAI Pasco Mkandara Mchambuzi MNYISANZU mohamed Mtoi Ogah Kimweri

- Spain na Catalonia
- Denmark na Feroe Island
- Italia na Vaneto

Last edited by a moderator: