Scientific evidence ya uponyaji wa babu

Scientific evidence ya uponyaji wa babu

Mzee2000

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2009
Posts
528
Reaction score
221
Wengi tumesikia ushuhuda wa baadhi ya watu wanaosema kwamba wametibiwa na babu lakini hizo zote ni hearsay bado sijaona uthibitisho wa kisayansi unaaonyesha uponyaji huo.

Kwa hiyo yoyote mwenye uthibitisho aonyeshe hapa:

1)Uthibitisho wa cheti cha daktari unaoonyesha ugonjwa kabla ya kunywa dawa na uthibitisho unaoonyesha ugonjwa uliopona kwa mfano, mtu aliyekuwa HIV positive na baadae kuonekana hIV positive.

2)Uthibitisho mmoja tu unatosha, katika sayansi, only one proof is enough. Kwa hiyo naomba wenye data wazimwage hapa. Bila proof, at lest moja, basi mambo ya loliondo ni mass halucination.
 
Homa ndugu mbaya sana yani hata uambiwe kula kinye*i chako utapona, utafanya hvyo. Wahenga wanasema "uongo wa mganga nafuu
ya mgonjwa.
 
Hadi sasa utafiti mdogo nilioufanya kwa wagonjwa kama 10 magonjwa mbalimbali hakuna hata mmoja mwenye proof ya kupona na wengine wanasema hawajapona
 
jamani wale watu 200 wako wapi? Mwenye taarifa nao atujuze,
 
Hiyo ni imani, utapona kwa imani. Lakini kisayansi hiyo dawa inaonesha ni antiviral na antidiabetic ambayo labda tuseme ina low potency. Soma report ya NIMR waliyo copy and paste toka tafiti za watu.
 
Mfa maji haachi kutapatapa, wajinga ndio waliwao na huku ni kukosa maarifa ya mambo yalifichika, Mungu tunakuoma utusaidie tuujue ufalme wako ili haya yanayojitokeza tuyakatae na kukutumainia wewe YEHOVA pekee.
 
sina uthibitisho wa wagonjwa wa ukimwi ila wa kisukari. Mjomba wangu aliyekuwa ameteseka sana na kisukari sasa ni mzima na anakunywa na kula vyote alivyokuwa hali kabla ya kutumia kikombe cha babu na vyeti vimethibitisha
 
waliopona kisukari wapo akiwamo mama yangu mzazi
 
Kwi kwi kwi!!nashukuru watanzania wamerealize kuwa babu ni msanii!sasa kabaki na wateja kutoka kenya na kongo ambao wakishtuka watapotea.
 
waliopona kisukari wapo akiwamo mama yangu mzazi

toa scientific evidence!kila siku mnasema watu wanapona bila kuthibitisha.mama yake rafiki yangu amefariki juzi wiki 5 baada ya kikombe cha babu.
 
waliopona kisukari wapo akiwamo mama yangu mzazi

toa scientific evidence!kila siku mnasema watu wanapona bila kuthibitisha.mama yake rafiki yangu amefariki juzi wiki 5 baada ya kikombe cha babu.
 
Back
Top Bottom