Wazazi tuwe makini na maisha ya watoto wetu tuko bize kutafuata hela watoto wassome wale vizuri kama hatufuatilii mambo kama hayo ubize wetu hausaidii kitu.Pick-Up hii aina ya Toyota leo mchana imenaswa na askari wa usalama barabara maeneo ya Posta ya zamani jijini Dar es Salaam ikifanya shughuli za kuwapeleka na kuwarudisha majumbani wanafunzi wa shule moja ya awali ikijulikana kama School Bus licha ya kuwa katika hali ya kuhatarisha usalama wa wanafunzi hao. Pichani ni wanafunzi waliokuwa wamebebwa katika gari hilo wakivuja jasho chini ya turubali lililofunika gari hilo kushika joto la jua. Kulia ni msimamizi wa wanafunzi hao.
View attachment 50953
School Bus hilo likipelekwa kituo cha polisi kwa uchunguzi zaidi.
Duh hiii ni balaa
hao wazazi wao wako wapi au walikuwa hawalijui hilo la watoto kubebwa kwenye pick up yenye turubali
Na hao walimu au huyo mwenye shule aliona kabisa hilo ni gari la kubebea wanafunzi
Hii biashara ya mtu anaanzisha shule nyumbani kwake na wazazi wanadanganywa wanapeleka watoto huko matokeo yake ndio haya
Poor kids hata hawajui kinachoendelea
Na mwalimu mwenyewe mbona nguo kama fupi sana kuwakalia wattoto mapaja yako nje anafundisha nini
Au ni kwamba watoto wakitoka hapo wamefuzu kila kitu
Kama wanafika, mbona poa tu.
Kuliko kukatiza na miguu town ni rahisi kugongwa.
Wabongo wanapenda sana makuu na ufahari...
Hapo sana sana police wameshafanya bonge la deal, na lazima wamevuta hela,
Angalia wenzetu wanatumia usafiri gani??
View attachment 51004
hii kali aiseeePick-Up hii aina ya Toyota leo mchana imenaswa na askari wa usalama barabara maeneo ya Posta ya zamani jijini Dar es Salaam ikifanya shughuli za kuwapeleka na kuwarudisha majumbani wanafunzi wa shule moja ya awali ikijulikana kama School Bus licha ya kuwa katika hali ya kuhatarisha usalama wa wanafunzi hao. Pichani ni wanafunzi waliokuwa wamebebwa katika gari hilo wakivuja jasho chini ya turubali lililofunika gari hilo kushika joto la jua. Kulia ni msimamizi wa wanafunzi hao.
View attachment 50953
School Bus hilo likipelekwa kituo cha polisi kwa uchunguzi zaidi.