‘school bus’ la utata lanaswa na polisi dar

‘school bus’ la utata lanaswa na polisi dar

Sad indeed!
BTW jana nilikua mitaa flan ya Kawe, asa ile naingia barabarani na gari yangu, jamaa akanichomekea na-ka vitz kake, kuchungulia hivi, asalaleeeeee! kameshona watoto nyomiiiiiiii! imagine ile siti ya mbele wamepakatana wawili, nyuma ndio usiseme, afu kwa kujidai, gari ina hadi logo za shule, i was like; wat the f word am i seeing?, is it real?, kumbe lile lilikua trela, hii ndio muvi, hakyanan umuweke mwanangu chini ya turubai hilo, ndio utanieleza kwanini Man Utd tunabebwa na marefa EPL.:frusty:
 
Pick-Up hii aina ya Toyota leo mchana imenaswa na askari wa usalama barabara maeneo ya Posta ya zamani jijini Dar es Salaam ikifanya shughuli za kuwapeleka na kuwarudisha majumbani wanafunzi wa shule moja ya awali ikijulikana kama “School Bus” licha ya kuwa katika hali ya kuhatarisha usalama wa wanafunzi hao. Pichani ni wanafunzi waliokuwa wamebebwa katika gari hilo wakivuja jasho chini ya turubali lililofunika gari hilo kushika joto la jua. Kulia ni msimamizi wa wanafunzi hao.

View attachment 50953

“School Bus” hilo likipelekwa kituo cha polisi kwa uchunguzi zaidi.
Wazazi tuwe makini na maisha ya watoto wetu tuko bize kutafuata hela watoto wassome wale vizuri kama hatufuatilii mambo kama hayo ubize wetu hausaidii kitu.
 
Duh hiii ni balaa
hao wazazi wao wako wapi au walikuwa hawalijui hilo la watoto kubebwa kwenye pick up yenye turubali
Na hao walimu au huyo mwenye shule aliona kabisa hilo ni gari la kubebea wanafunzi
Hii biashara ya mtu anaanzisha shule nyumbani kwake na wazazi wanadanganywa wanapeleka watoto huko matokeo yake ndio haya
Poor kids hata hawajui kinachoendelea
Na mwalimu mwenyewe mbona nguo kama fupi sana kuwakalia wattoto mapaja yako nje anafundisha nini
Au ni kwamba watoto wakitoka hapo wamefuzu kila kitu

Thanks
 
Wabongo wanapenda sana makuu na ufahari...

Hapo sana sana police wameshafanya bonge la deal, na lazima wamevuta hela,

Angalia wenzetu wanatumia usafiri gani??

india 2.jpg
 
Just wondering, kama school pickup (sio bus) iko hivi hiyo shule itakuwaje (i.e walimu, majengo etc)...kwani ni lazima kuwe na usafiri???
 
Kaaazi kweli kweli. Ngoja na mimi nitaanzisha school bus langu la mkokoteni.
 
Pick-Up hii aina ya Toyota leo mchana imenaswa na askari wa usalama barabara maeneo ya Posta ya zamani jijini Dar es Salaam ikifanya shughuli za kuwapeleka na kuwarudisha majumbani wanafunzi wa shule moja ya awali ikijulikana kama “School Bus” licha ya kuwa katika hali ya kuhatarisha usalama wa wanafunzi hao. Pichani ni wanafunzi waliokuwa wamebebwa katika gari hilo wakivuja jasho chini ya turubali lililofunika gari hilo kushika joto la jua. Kulia ni msimamizi wa wanafunzi hao.

View attachment 50953

“School Bus” hilo likipelekwa kituo cha polisi kwa uchunguzi zaidi.
hii kali aiseee
 
Wazazi wengine ovyoo kabisa, kwa maana iyo ilo ligari linafika hadi nyumbani kumchukua mtoto???
 
Back
Top Bottom