Sawa nauli zimepanda lakini zinaendana na ubora wa huduma?

Kinoamiguu

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
10,526
13,015
Shime wanajanvi,

Tarehe nane inakaribia, tutaanza kulipa nauli mpya za daladala na mabasi ya mikoani. Tumeambiwa wadau walitoa maoni yao nchi nzima mimi sikuhojiwa. Ningehojiwa nisingeafiki hata kidogo, sababu ninazo lukuki tena zenye mashiko hasa kwa daladala; huduma ni mbovu mnoo, mbovu sana tena za kutia kinyaa na kukera kama siyo kuudhi.

Pitia standi ya makumbusho usiku kuanzia saa 2 uone watu wa Bunju na Tegeta wanavyodhalilika na kuyumbishwa kama wanyama {wanaswagwa}.

Daladala zinakuja na kupaki anatokea kichaa mmoja anasema hatupakii, tunaenda kulala au gari mbovu au hiki cha kijinga kabisa kabisa.

Watu wa daladala za Bunju na Tegeta mfano wanataka kupata faida mara mbili hawataki watu wanaoenda mpaka mwisho Bunju, wanawaita MAWE kisa hawashuki njiani, kweli? Mamlaka ziko wapi? Trafic wapo wapi? Nani awasemee wananchi hawa wanaoteseka?

Daladala lililosajiliwa kufanya safari zake Bunju-Makumbusho linafika makumbusho wanasema hawaendi, wakifika barabaarani wanasema wanaenda Bunju ili wapakie mara yaani wengi wakashuke Tegeta kisha waanze kupakia tena?

Ndugu zangu, vipato vya Watanzania waliowengi ni vya chini sana, hizi nauli za kulipa mara mbilimbili wanazipata wapi? Kwanini ukate TLB ya Bunju-Tegeta mathalani kisha ukatishe safari? Nani anamiliki magari haya? Asubuhi inakuwa hivyohivyo, watu wanajazana standi ili waende mjini wakiwa wamejazana kama kondoo wanaoenda kuuzwa mnadani, tena wa Pugu.

Nauli mpya zimetangazwa je, wapandishaji nauli upandishaji huu utaenda sawa na ubora wa huduma au Walevi wa ugoro na Double Kiki/Wapiga debe watendelea kupanga ruti na nauli?

Tuamke!
 
Wamesema zinaendana na gharama za mafuta.....kuhusu ubora bongo nunua gari lako
 
Shime wanajanvi,
Tarehe nane inakaribia, tutaanza kulipa nauli mpya za daladala na mabasi ya mikoani. tumeambiwa wadau walitoa maoni yao nchi nzima mimi sikuhojiwa. ningehojiwa nisingeafiki hata kidogo, sababu ninazo lukuki tena zwnye mashiko hasa kwa daladala. huduma ni mbovu mnoo, mbovu sana tena za kutia kinyaa na kukera kama siyo kuudhi.
Pitia standi ya makumbusho usiku kuanzia saa 2 uone watu wa Bunju na Tegeta wanavyodhalilika na kuyumbishwa kama wanyama {wanaswagwa}.
Daladala zinakuja na kupaki anatokea kichaa mmoja anasema Hatupakii, tunaenda kulala au gari mbovu au hiki cha kijinga kabisa kabisa.
watu wa daladala za BUNJU na TEGETA mfano wanataka kupata faida mara mbili hawataki watu wanaoenda mpaka mwisho BUNJU wanawaita MAWE Kisa hawashuki njianikweli? mamlaka ziko wapi? trafic wapo wapi?nani awasemee wananchi hawa wanaoteseka
Daladala lililosajiliwa kufanya safari zake BUNJU MAKUMBUSHO linafika makumbusho wanasema hawaendi wakifika barabaarani wanasema wanaenda Bunju ili wapakie mara yaani wengi wakashuke Tegeta kisha waanze kupakia tena?
Ndugu zangu, vipato vya watanzania waliowengi ni vya chini sana, hizi nauli za kulipa mara mbilimbili wanazipata wapi? kwanini ukate TLB ya BUNJU TEGETA mathalani kisha ukatishe safari? nani anamiliki magari haya? asubuhi inakuwa hivyohivyo watu wanajazana standi ili waende mjini wakiwa wamejazana kama kondoo wanaoenda kuuzwa mnadani, tena wa pugu.
Nauli mpya zimetangazwa je wapandishaji nauli upandishaji huu utaenda sawa na ubora wa huduma au WALEVI WA UGORO NA DOUBLE KIKI/WAPIGA DEBE WATAENDELEA KUPANGA ROOT NA NAULI?
TUAMKE
Kinachotolewa ni "Bora Huduma" na wala siyo "Huduma Bora."
 
Back
Top Bottom