Ahlan Wasahlan brothers and sisters!
Acheni tuwe wakweli, binafsi nimeanza kumfuatilia Huyu Msanii Muda mrefu lakini zaidi sana Na Kwa undani Ni kuanzia 2007 mpaka Leo.
Kwa kifupi Ni Msanii mzuri mwenye uwezo wa kucheza vizuri Na sauti Yake, sijui Kama hua anatunga mwenyewe Au anatungiwa hizo nyimbo zake Ila Kwa kiasi kikubwa anajitahidi.
Ila Sasa kuna huu wimbo wa kuitwa Unconditionally bae, Alikiba ameshirikishwa, Kwa jinsi ninamvyomjua Na uwezo wake katika huu wimbo hajafanya kazi yeyote, Yaani kaimba vibaya!
Imagine anasema "jina langu Ali Sasa lazima Nile" Sasa hii maana Yake Nini? Alikosa Kabisa cha kuandika hapo? Au Ndio mambo ya mizani? Huo wimbo Ni mzuri sana Anzia vionjo vyake Ktk beat mpaka mpangilio wa sauti za hao wenye wimbo wao lakini Huyu Msanii wetu kapooza sana katika nafasi Yake ingawa upande wa video kafanya vizuri.
Hivyo Kwa maoni yangu Ni kwamba Alikiba KAHARIBU wimbo wa watu, Hebu piga picha ule wimbo wangeimba wenyewe tu Sauti Sol, ungependeza sana!
Ushauri wangu; Next time Alikiba akipata nafasi ajitahidi kuimba serious Na mistari yenye mashiko, unapoleta utani Ktk issue serious haujiangushi wewe tu, unatuangusha mpaka sisi Watanzania wenzio.
NB: Hayo Ni maoni yangu Mimi binafsi Mgibeon, sina team yeyeto ya kushabikia hapa bongo zaidi ya Young Africans Sports Club! Kila mtu anasikio lake la kusikilizia uzuri Na ubaya wa wimbo, hivyo hala hala Na matusi jamani, tafadhari sana!