Sauti ya dr wilbroad slaa

Kimilidzo

JF-Expert Member
Jan 3, 2011
1,346
613
Sisi wakazi wa vijijini tulikuwa tumemiss sana sauti ya Rais wetu wa moyoni, ambaye akituamuru tuingie mtaani kama Misri na Algeria tunaenda mara moja bila kupinga, Dr Slaa (PhD). Hatimaye jana kupitia luninga ya ITV tumeisikia kutoka mahakamani Arusha. Watu walizizima kwa furaha pale kilabuni tulipokuwa tunaangalia luninga kwa kulipia kutokana na ukosefu wa umeme. Sauti ya Rais wa mioyoni mwetu imekonga nyoyo zetu na tunatamani kesi iwe inasikilizwa kila siku ili tuwe tunamsikia mara kwa mara. Sauti ambayo inaweza kumtoa nyoka pangoni. Tumefarijika kusikia kuwa Rais atatutembelea kwa maandamano kuanzia keshokutwa na atafika hadi wilayani. tunasema Karibu sana Rais wetu mpendwa Dr Slaa (PhD) na Dowans ya JK hailipwi ng'ooooooo
 
du kwa kweli Dr. Slaa nampenda sio siri, kwanza ana akili ya kuchambua mambo na anafaa kuwa rais kwa kuwa alionesha kiwango kikubwa cha uelewa wa matatizo ya wananchi na jinsi ya ufumbuzi wa hayo matatizo. Alimpita Kikwete mara 2000 kwa uelewa na kujibu hoja.
 
Dr anajua nini watanzania wanataka na si kama viongozi wengine tulionao,heshima kwa Dr wa ukweli
 
arushalema.jpg


Akizungumza nje ya Viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, aliwaambia mamia ya wafuasi wa chama hicho baada ya kesi inayomkabili yeye na wafuasi wengine kuahirishwa, akisema katika maandamano hayo pia watazungumzia mauaji wa Arusha.

"Tunawashukuru sana kwa kuja mahakamani kutuunga mkono. Kama tulivyoahidi, yale maandamano ya nchi nzima yataanza Mwanza kesho kutwa (kesho) na baada ya hapo tutaenda mikoa mingine ya Kanda ya Ziwa,"alisema Dk Slaa.

Dk Slaa alisema baada ya kumaliza Mkoa wa Mwanza watakwenda katika mikoa ya Mara, Shinyanga na Kagera huku akibainisha kuwa watakaa Kanda ya Ziwa kwa siku 10.
 
Dar lini jamani na mimi nijoin hayo maandamano....kama wataniua waniue tu...kama walivozoea kupiga watu wasio hatia risasi za moto
 
Aluta continua. Hapa sasa mnaongea nimefurahia sana mipango hii kama mnahitaji rasilimali bunini njia ya kuwachagia kama ile ya mpesa au sms za kulipia kwa kuandika chadema kama bado inatumika
 
Dar lini jamani na mimi nijoin hayo maandamano....kama wataniua waniue tu...kama walivozoea kupiga watu wasio hatia risasi za moto

JK asipokuwa makini, na asipoacha usanii ataondoka madarakani kabla ya muda wake kuisha. Asimwonee Dr. Slaa tumaini jipya kwa watanzania.
 
Dr Hata makada wanamkukubali ila uccm umewazidi uwezo, Dowans hawastahili malipo tutaandama mpaka kieleweke.
 
nilidhani ni mimi tu niliyefurahi kusikia sauti,nilimsikia akisema "polisi tumieni akili za kuzaliwa" baada ya polisi kuwafurumushia wananchi,raia wema waliotoka kusikiliza kesi dhidi ya viongozi na wanachama wa CHADEMA
 
Nyie nadhani mnapenda hata ush*zi na mik*jo ya huyo. Blind supporters!
 
Back
Top Bottom