SAUTI: Sikiliza nondo za Godbless Lema Bungeni

SAUTI: Sikiliza nondo za Godbless Lema Bungeni

Ila hii ya kusema wabunge waende na herikopta DODOMA [emoji848] mbunge hapo kachemka
 


Wakuu kumbe tunamis vitu vingi sana kwa hili bunge la gizani!

Lema ameponda swala la bunge kutooneshwa live.

Serikali kubana matumizi huku wakurugenzi wakienda bungeni Dodoma kwa mabasi na kusema hii dhana ya kuturudisha kwenye umaskini.

Anaongeza kuwa kama rais ana nia ya kupambana na ufisadi angeacha bunge liwe live.

Mawaziri waoga hawana maamuzi.

Amemuuliza naibu Spika kurudisha fedha kwa rais bila kumshirikisha Spika wake. Amemtetea yule mama wa Oiljet aliyefukuzwa wakati kamtaja aliyemtuma kwa jina, yaani Muhongo lakini hakuchukuliwa hatua.

Amesema Uchaguzi wa Zanzibar umeisha lakini kesi haijaisha, msifikiri mpo salama.

kanjanja tu. sasa hapo ndio kaongea nini?
 
Ila hii ya kusema wabunge waende na herikopta DODOMA [emoji848] mbunge hapo kachemka
kaka hii nchi haitafika iendelee kama tuna wabunge wanadhani maendeleo ni kwenda bungeni na helkopta na sisi tunawaita majembe. Ila kuna baadhi ya vitu kavisema vizuri kwa asilimia 65 kwa mia kaborongo tu. Huko kwa matajiri sasa hivi kunawaka moto kwaajili hizi class anazizungumzia. Kuweka makundi ya watu kwa class siyo maendeleo ya jamii, mwishowe hua yanaishia pabaya.
 
Mara nyingi ukisikiliza bunge huwezi kujua ni hoja gani inaongelewa? Sijui nini kimetoa lakini naamini kuna tatizo sana, wabunge hawaelewi wako bungeni kufanya nini? Ni nadra kusikia wakichambua miswadwa/hoja kisheria badala yake wanaongea story utafikiri ni watu wako bar wanakunywa pombe.

Ni hizi kelele za kutaka bunge lioneshwe live, nadhani wabunge wenyewe kwa umoja wao wanatakiwa wawekane sawa, bunge lilifikia mahali huwezi kuangalia na watoto, limegeuka kuwa sehemu ya mipasho na lugha za kihuni. Kabla ya kudai bunge liwe live wabunge wakae chini na kuwekana sawa ili liwe bunge lenye staha. vingenevyo, wahurumie watoto wetu.
 
Lema kaongea vizur sana na maneno ameyapangilia kama vile anasoma mahali...Hakika namfaninisha sana Martin Luther King Jr katika kuongea kwa mpangilio mzuri wa maneno wakati wa kutetea wanyonge..Kudos..
 
Nilikuwa nimejaribu kuweka hii clip lakini bila mafanikio.
Lena kawapa ukweli dhahiri, na nadhani sasa itumike njia hiyo hiyo wa bunge wachukue clip za wasemacho bungeni na kurusha mitandao ya jamii tuwasikie.
Pia wasiache kurekodi na zile pumba za wabunge wa ccm, ile watakayo iona ina ujinga ulio pitiliza waturushie na isambae nchi nzima. Baada ya hapo watajihoji kama kwa ulimwengu huu unaweza kuficha ujinga?
Nyie mlisha rogwa kiukweli hamfai
Sijui ni usahaulifu
Au ni ujuha!!
a82664effba7f6e369882b98c5ef7c00.jpg

Poleni sana
Hamna hamu tena
 
Lema kaongea vizur sana na maneno ameyapangilia kama vile anasoma mahali...Hakika namfaninisha sana Martin Luther King Jr katika kuongea kwa mpangilio mzuri wa maneno wakati wa kutetea wanyonge..Kudos..
Lema ni tegemeo la nchi .
 
Hivi Huyu wanae muonea huruma kutumbuliwa na Magufuli Bungeni si walimsema sana tena ovyo ovyo na kina lema wakapiga Makofi tena walimsema huku wameshika makaratasi Eti Leo wanamuonea huruma nakusema Magufuli kamuonea Jamani hawa Wapinzani ni waswahili sana! Leo makonda kusema madudu yake basi ni tatizo madudu waseme wao tuu

Kweli kusafiri asafiri mwarabu akisafiri mzaramo shida
Hawa watu Unaitaji kuwa Zuzu kuwa fuata na upuzi wao
Kwamwenye Akili look lazima ashindwe kuwaelewa hawa

Nivigeugeu sana
d619db3f942b320edc3f9d0f90dc5b45.jpg
b23594ae7509b5ec8062ec8a54129443.jpg
b0668cef628edc01937b6f381f6ea5c9.jpg
 
lema ni hasara tu kwa wana arusha hajafanya lolote pale mjini zaidi ya kuropoka ropoka tu bungeni kama hivi.
 
lema ni mwana siasa shujaa ni mfano wa kuigwa huwa kauli zake na mfananisha na mugabe
 
Back
Top Bottom