Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,883
- 2,763
Jioni ya leo katika radio ya pashen fm huwa kunakuwa na kipindi nimekisahau jina. Wapo watangazaji watatu; wa kiume mmoja na mabinti wawili wenye sauti nyororo. Kilichoniboa kuhusu wote watatu ni ufaham wao mdogo wa mambo na kutokujua kiswahili kwa ufasaha. Kiukweli nimewakosoa kimoyomoyo mpaka basi. Mfano kuna habari moja toka kenya kuwa bwana mmoja-ochieng kawaua watoto wake watatu wa kufikia pamoja na mama yao. Wao wakajichanganya wasijue wanasoma nini na kufikia uamuzi kuwa ile familia ndo imemuua huyo bwana. Imenifanya kununua gazeti hilo la dar leo na kuisoma habari hiyo. Kingine ni habari iliyohusu majambazi ambapo wanasema majambazi 'waliweza' kuuawa. Hii inasikitisha