Saudia Arabia yaachana na Petrodollar rasmi

Saudia Arabia yaachana na Petrodollar rasmi

hiyo vita ni mgumu sana sioni mmarekani akishindwa
Mbona kaanza kushindwa Mkuu upo dunia ya ngapi,takwumu zinaonesha kila mwaka transactions kwa USD zinapungua kwa kasi kama upepo.
Kwenye kikao cha G7 kinachoendelea Italy wanataka wataifishe mali za Russia na sababu kubwa zipo kwenye USD kwa mantiki nchi gani itaendelea kuweka akiba yake kwenye USD???
 
Ngumu sana siyo rahisi kiivyo hizi mcho zote unazotaja mwisho wa siku wanaenda kuchukua hela imf na world bank kwa dollar maana taasisi za fedha duniani zote mmarekani anazicontrol yeye kupambana na marekani siyo kitu rahisi hivyo ,hii mifumo ya kuitawala dunia aliijenga tangu mwaka 1600 huko
Mkuu ndio maana siku hizi nchi zinaanzisha Bank za kikanda baada ya kuona WB & IMF lengo Lao ni kuilinda USA na western.sikiliza speech za viongozi wako wa kiafrika wakiongea huko kwenye mikutano ya UN mbona huwa wanalisema hilo jambo.
bank kama New development Bank Home - New Development Bank imeanzishwa ili kuwaondolea nchi kama Tanzania manyanyaso ya IMF & WB
 
Mbona kaanza kushindwa Mkuu upo dunia ya ngapi,takwumu zinaonesha kila mwaka transactions kwa USD zinapungua kwa kasi kama upepo.
Kwenye kikao cha G7 kinachoendelea Italy wanataka wataifishe mali za Russia na sababu kubwa zipo kwenye USD kwa mantiki nchi gani itaendelea kuweka akiba yake kwenye USD???
Ubaya ni kwamba huyu jamaa ana ubabe na ana control vitu vingi duniani, atakubana tu uteme bungo, libya alianzisha mpango huu kabla ya dunia kuzinduka kilichomkuta hata viongozi wetu wa afrika walijifanya kama hawaoni kilichomkuta gafdaffi, iraq alishambuliwa bila sababu
Hapa tatizo jamaa ni mbabe anafanya chochote kukuharibu ukigusa maslahi ya uchumi wake
 
Unajiuliza kwanini tunakopa nje pesa muda huu kwa wingi kwa sababu hatuna dollar za kuwalipa watasha na hao wakorea na wachina wanaojenga SGR, MADARAJA na bwawa la Nyerere. Sasa kama unaona wachina wanapenda pesa yeo basi watukopeshe Yuan then tuwalipe Yuan hiyohiyo kama watakubali. Hao hao Saudia wambie nawapa pesa ya madafu mnipe mafuta uone watakavyomute. Mrusi mwenyewe anahangaika na uchumi baada ya ukosefu wa dollar ya marekani. Very sad
Ndio maana ukaambiwa Hifadhini dhahabu badala ya dollar makaratasi, maana chochote ukitakacho kupitia akiba yako ya dhahabu utakipata duniani
 
Ubaya ni kwamba huyu jamaa ana ubabe na ana control vitu vingi duniani, atakubana tu uteme bungo, libya alianzisha mpango huu kabla ya dunia kuzinduka kilichomkuta hata viongozi wetu wa afrika walijifanya kama hawaoni kilichomkuta gafdaffi, iraq alishambuliwa bila sababu
Hapa tatizo jamaa ni mbabe anafanya chochote kukuharibu ukigusa maslahi ya uchumi wake
Ana contro kitu gani ambacho wengine hawana
 
Binadamu ana akili kuliko mnyama ndio maana akaitwa Bin Adam, aliyekwambia mataifa yameshindwa kuachana na matumizi ya dollar nani, Juzi Urusi katangaza kuachana na dollar kwa Ununuzi au mauzo yoyote ya biashara kutoka Urusi, Mchina teyari yuko mbioni kumalizi swift yake ili utakapo bidhaa yake itakubidi ukaitafute Yuan ilipo ndipo upate kununua, mataifa mengine yatafuata mdogo mdogo, mchakato wa kuingamiza dollar utachukua miaka mingi kidogo lakini hatimaye itakufa, dunia inabadilika kwa kasi huwezi kila siku uwe unatumia dollar kama silaha kuumiza nchi zao wakubali never, Mchina kajifunza mengi sana kutokana na vita vya Ukraine na Urusi hawezi kukubali kufanya makosa hayo, kuitegemea dollar tena kwa kila kitu kwenye bond keshaanza kuiondoa...
China huyo huyo biashara zake nyingi anafanya na haohao wanaomlipa dola sasa unataka kuniambia atawaacha.? Ni kitu ambacho hakiwezekani.

Haya mambo ya kuachana na dola ni porojo tu zinapigwa kwa sisi tunaofanya biashara za kimataifa huwezi kutudanganya labda muendelee kudanganyana huko kwenye vijiwe vyenu na huko masjid ubwabwa.
 
Tuombe Urusi afanikiwe kwenye harakati zake kuifungulia dunia ili kila nchi itumie pesa zake. Just saying.
Urusi au Putin mkuu?
Putin hawezi ishi milele hizo strategy zake ni za muda tu kama za Magu once you are dead and gone trouble in paradise.
 
Nikienda kununua sabufa china watakataa pesa yao?..Korea nao watakataa nikitaka Samsung kwa pesa yao,zamani siyo leo
Na wenyewe wakitaka kununua bidhaa kwenye hayo mataifa yaliyoendelea watafanyaje wakati sasa hawana dola na madeni wanayodaiwa kwa dola watayalipaje.?⁉️

Acheni kudanganyana humu bwana.
 
Acha kujifariji kila kitu huwa kinaenda kwa hatua.
Miaka 30 iliyo pita Marekani alikuwa anamiliki zaidi ya %50 ya uchumi wa dunia lakini leo hii ana miliki %18 tu ya uchumi wa dunia.
Urusi kaondolewa kwenye mfumo wa kifedha wa swift lakini mpaka sasa Urusi anafanya biashara kote duniani zikiwemo hizo nchi zilizo iwekea vikwazo.
Kitendo cha uchumi wa Urusi kuonesha unakuwa chini ya vikwazo vikali vya nchi za Magharibi ni nshala tosha kabisa kuwa nchi za Magharibi zinepoteza utawala wa kiuchumi ulimwenguni.
Zaidi ya asilimia 70 ya biashara za kimataifa bado zinatumia dola kinyume cha hapo mtumie "The Ancient Barter Trade" kitu ambacho ni kigumu sana kwa dunia ya leo.

Mimi niko kwenye International Business hivyo nafahamu ninaongea nini.
 
Binadamu ana akili kuliko mnyama ndio maana akaitwa Bin Adam, aliyekwambia mataifa yameshindwa kuachana na matumizi ya dollar nani, Juzi Urusi katangaza kuachana na dollar kwa Ununuzi au mauzo yoyote ya biashara kutoka Urusi, Mchina teyari yuko mbioni kumalizi swift yake ili utakapo bidhaa yake itakubidi ukaitafute Yuan ilipo ndipo upate kununua, mataifa mengine yatafuata mdogo mdogo, mchakato wa kuingamiza dollar utachukua miaka mingi kidogo lakini hatimaye itakufa, dunia inabadilika kwa kasi huwezi kila siku uwe unatumia dollar kama silaha kuumiza nchi zao wakubali never, Mchina kajifunza mengi sana kutokana na vita vya Ukraine na Urusi hawezi kukubali kufanya makosa hayo, kuitegemea dollar tena kwa kila kitu kwenye bond keshaanza kuiondoa...
Hiyo Russia itatumiaje sarafu ya dola wakati alisha ondolewa kwenye SWIFT 😛😛
 
Wanakiburi Cha mahela ya bure ya watu duniani kote wanaokwenda kulizunguka jiwe na kumtupia mawe shetani
 
Na wenyewe wakitaka kununua bidhaa kwenye hayo mataifa yaliyoendelea watafanyaje wakati sasa hawana dola na madeni wanayodaiwa kwa dola watayalipaje.?⁉️

Acheni kudanganyana humu bwana.
Watanunua kwa pesa ya hayo mataifa,wakati umefuka kutafuta riyali ya Saudi kununua mafuta badala ya kuhaha na dola
 
Urusi hana mchango wowote hapa africa zaidi ya kuuza masiraha yake lakini nchi za magharibi ndizo zinazotoa mikopo na kusaidia nchi zetu ikiongozwa na baba lao Usa .
Sasa hiyo urusi inatusaidia nini? Jaribu kuwaza Tanzania tuna Ng'os ngapi zinazofadhiliwa na Usa na zimeajiri maelfu ya watanzania.
Kwanza sijawai pita na kuona mashirika yanayofadhiliwa na Urusi zaidi ya nchi za magharibi.
Hupaswi kuishi kwa nawazo ya kusaidiwa,bali kujisimamia mwenyewe ni upumbavu kuamini kwamba Urusi anajukumu la kukupa msaada. hizi ndo akili za ngozi nyeusi.
 
Back
Top Bottom