Saudi Arabia bans 50 baby names

Saudi Arabia bans 50 baby names

What next after changing your name into tradition one? What will you benefit from that? Mambo mengine ni vyema kufahamu watu wanayafanya kwa mujibu ya iman zao. Hawa waSAUDIA hawajapiga marufuku majina hayo kwakuwa yanaenda kinyume na tamaduni za waarabu bali kwakuwa yanamaana mbaya katika upande wa dini. Kifupi kama unamawazo ya kuwa na majina yako ya kiasili hujakatazwa lakini pia jitahidi ufuate na mila na desturi yako huku ukiachana na kuwa mfuasi wa dini kama uislamu au ukristo ambazo kimsingi hao ndio waliokuja kutufundisha.

Mkuu sijui kama umesoma post vyema, Saudia wamekataza hayo majina kwa sababu kuu mbili, mosi yako kinyume na tamaduni zao, mbili ndio za sababu za kidini

Nitapata faida ya utambulisho wangu kupitia jina na nitakuwa nimetunza asili yangu

Siamini dini ya mtu mweupe yeyote FYI
 
Kumpa mtoto jina la asili kunaweza kuwa kitu cha muhimu sana, ndiyo maana hata mimi nimejiita "Kiranga" na si "Sean".

Kulazimisha mtu asiitwe "Sean" ni kitu tofauti kabisa.

Sikatai majina ya asili, mimi mwenyewe nimekumbatia majina ya asili.

Nakataa kulazimisha majina na kuwanyima watu uhuru wa kuamua watumie majina gani.

Mimi siku zote nasimamia uhuru, na kukataa watu binafsi kupangiwa jinsi ya kuishi maisha yao binafsi na serikali.

Hili nataka lieleweke wazi.

Tuko pamoja mkuu maana hata mimi nimetoa pendekezo tu sio lazima na sidhani kama Saudia kukataza majina hayo officially ni best move

Ni jambo la kheri sana watu kutumia majina yao asilia, majina yanatumika kama utambulisho zaidi ya kitu kingine chochote ulimwenguni
 
sisi wanuakyusa wakina mwaiboro mwakipumbu atufile atufigwegwe wenyeji wa dah mfanyeni sasa babake anaitwa bure ukiunganisha mfanyeni bure.
 
Mnaotaka mbaki na majina ya asili msiishie hapo, muwe mnavaa na kiasili, kwani hata mavazi ya sasa ni amma ya kizungu amma ya kiasia.

Ndiyo maana tunatafuta vazi la taifa tatizo ma ccm huwa hawafanikishi jambo.Kamati ilizunduliwa kwa mbwembwe ilipoishia allah knows
 
Saudi Arabia ni moja ya nchi za kidikteta zilizobakia hapa duniani.
 
Wamezingatia asili yao kwanza, sasa wewe muafrika kumuita mtoto wako Ally Mohamed Ally maana yake nini.. Kuletewa dini na weupe hakumaanishi hata asili yetu haina maana na inabidi kila kitu tufanye kama wao
Sie tuna asili gani wewe!!? Tushukuru kuwa hata hii lugha tunayoelewana humu wametufadhili !! hiyo misemiyati nayo ni yao!! sahau majina ya ny'o nga' nyu' !! tuongee kaBinaadamu na siyo.... kushabikia !! Haki tuseme bhanaa!!
 
Mkuu sijui kama umesoma post vyema, Saudia wamekataza hayo majina kwa sababu kuu mbili, mosi yako kinyume na tamaduni zao, mbili ndio za sababu za kidini

Nitapata faida ya utambulisho wangu kupitia jina na nitakuwa nimetunza asili yangu

Siamini dini ya mtu mweupe yeyote FYI

Unaujua utamaduni wa Saudia Arabia?
 
Unaujua utamaduni wa Saudia Arabia?

Sina sababu ya kujua utamaduni wa Saudia ila wao ndio wamesema sababu ni mbili utamaduni na dini

Mengine unaweza bishana nao au ukaacha
 
Sie tuna asili gani wewe!!? Tushukuru kuwa hata hii lugha tunayoelewana humu wametufadhili !! hiyo misemiyati nayo ni yao!! sahau majina ya ny'o nga' nyu' !! tuongee kaBinaadamu na siyo.... kushabikia !! Haki tuseme bhanaa!!

Hueleweki
 
Majina mengine nayo ukisikia lazima kwanza ugune,Kusudiyao,yashakua,Ntatoloka,Havintishi,Mwandimbo,Avintishi,Nyamkimbo yani uuuuuuuuwiiiiii!..
 
Ndiyo maana tunatafuta vazi la taifa tatizo ma ccm huwa hawafanikishi jambo.Kamati ilizunduliwa kwa mbwembwe ilipoishia allah knows

Hivi hii habari ya "Vazi la taifa kwa kamati, imla iso tamati" bado haijafikia tamati mpaka leo?

Nikiandika kuhusu hii habari hapa chini, January 2012 !

Ndiyo habari hizi hizi za umungumtu wa serikali.

http://www.vijana.fm/2012/01/25/vazi-la-taifa/
 
Saudi Arabia ni moja ya nchi za kidikteta zilizobakia hapa duniani.

Habari nzima ya kukataza majina ni kuwashikia watu akili tu.

Unaambiwa wewe mpaka wako hapa, tunakufungia huko zizini kama ng'ombe.
 
Hueleweki

Samahani Bufa ...wewe ndiyo huelweki kabisa !! maana unashinikiza utamaduni wako kwa wengine.. Wao huru na wao wapendavyo wewe na mengineo humu yanawahusu nini ya wenzenu? badilisheni yenu na murekebishe tamaduni zenu!!
ndo muje waeleze wengine.!
 
Majina mengine nayo ukisikia lazima kwanza ugune,Kusudiyao,yashakua,Ntatoloka,Havintishi,Mwandimbo,Avintishi,Nyamkimbo yani uuuuuuuuwiiiiii!..

hayo unayaona mabaya kwa kuwa umezoea haya ya kizungu Nancy, Elizabeth, Magreth, George, Godfrey n.k lakini kama hayo majina yangekuwa common yasingeonekana mabaya
 
Kwa hiyo kwa sisi vichwa Maji unashauri tuendelee kuita watoto, shida,chozi, siambiliki, mwanambaya, tabu situmai, sijui n.k
 
hayo unayaona mabaya kwa kuwa umezoea haya ya kizungu Nancy, Elizabeth, Magreth, George, Godfrey n.k lakini kama hayo majina yangekuwa common yasingeonekana mabaya

Sijayazowea yakizungu wala ya ki China,ila haielekei kumuitaa mwanao Kusudiyao,au Avintishi...
 
Back
Top Bottom