Sato na Sangara kutoka China

Sato na Sangara kutoka China

uvugaji wa samaki ni soko kubwa sana duniani kama walivyo kuku wa kisasa, uvugaji wa samaki utatoa ajira kubwa zaidi. Pia kuna soko kubwa sana nje ya nchi. Ni sawa na Greenhouse farming, muda si mrefu watu watalima nyanya kwenye eneo dogo mjini na kupeleka sokoni.
Kilimo na ufugaji wa kisasa utawavutia vijana kupenda kilimo, bila ya hivyo hawawezi kupenda kilimo cha jembe la mkono
 
Kuna sato na sangara hai na waliogandishwa wanauzwa mwananyamala na Wachina. Bei yake ni poa kuliko Sato na Sangara tika Mwanza. Hao samaki ni zao la vifaranga waliochukuliwa Lake victoria kijanja na kuoteshwa kwenye bwawa kubwa huko Gwanzhu. Sera za Serikali yetu zinatoa fursa kwa wachina/wageni na kudidimiza wavuvi na viwanda vya ndani. Jadili kwa hoja. Hatua thabiti zichukuliwe haswa kuhakikisha Wachina hawa wamefuata taratibu na wanalipa kodi kuwaingiza tz.

Na serikali yetu ichukue vifaranga ipeleke Bwawa la Mtera na Kidatu
 
Hizo ni fursa kwani walaji ni wengi kuliko uzalishaji. Tuchangamkie fursa na TFDA nao wafuatilie kuona ubora wa samaki wenyewe maana wachina waangalia fedha mno.
 
Kuna sato na sangara hai na waliogandishwa wanauzwa mwananyamala na Wachina. Bei yake ni poa kuliko Sato na Sangara tika Mwanza. Hao samaki ni zao la vifaranga waliochukuliwa Lake victoria kijanja na kuoteshwa kwenye bwawa kubwa huko Gwanzhu. Sera za Serikali yetu zinatoa fursa kwa wachina/wageni na kudidimiza wavuvi na viwanda vya ndani. Jadili kwa hoja. Hatua thabiti zichukuliwe haswa kuhakikisha Wachina hawa wamefuata taratibu na wanalipa kodi kuwaingiza tz.

Inawezekana samaki akatoka china tena Gwanzhu akafika bongo akiwa hai? basi atakuwa sio samaki wa kawaida,
 
Sioni tatizo kwa wachina kuuza sato na sangara kwa bei nafuu,maana inamsaidia mtanzania wa kawaida kupata hao samaki kwa beo rahisi,sio wote wana afford kununua sato kilo kwa 10,000 na sangara kwa 8,000 kama wanauza chini ya hapo sio mbaya.

Watanzania achana nao bana,wakiletewa vitu pei utasikia oh tunakosa kodi hao tu wa Mwanza na Mara nao hawlipikodi na bei ipo juu,kwanza hiyo kodi inawanufaisha akina nonino,wacha wauze bei poa na sisi tupate protein bana au anataka tule mapanki,sijuihaowachina wapo wapi bana namimi nipate Sato,sijui bei yake kiasi gani,Sato wa Mwanza wanaliwa Masaki na O'bay.
 
Back
Top Bottom