Satanic verses

Satanic verses

Hichi kitabu ni kama Hadithi za ndumilakuwili, ni Fiction Novel Based on Magic Realism, nothing special.
Hakuna Hoja wala Facts bali ni mawazo au Idea za kutunga na Opinions za mtu mmoja juu ya kitu fulani ni defamation na mockery sababu hakuna hoja wala facts zozote na hiyo inafanya kitabu kizima kuwa matusi tu.

Ni kama Novel za StarWars, StarTreck na Marvel au DC comicbooks lakini kuchukua mtu halisi kutoka kwenye maisha ya kweli na kumuandika unavyotaka.

Unaweza kuita ni defamation, slander, libel au mockery kwenye level za juu kabisa za kutoa na kitabu kabisa kwa nia ya entertainment. ni kama mtu akutukane tu na akudharirishe hadharani bila sababu za msingi ni lazima ukasirike.
Ndo kazi ya Fasihi Simulizi kuweka mazingira ya kufikirika.

Ila hizi kazi huleta tabu khasa kwa tawala zetu kama Tanzania kitabu cha "Animal Farm" kilipigwa marufuku enzi za Hayati mwalimu Nyerere.

Na hichi kitabu mwandishi wake George Orwell ameandika kuhusu mkulima mwenye shamba ambae aliwatelekeza wanyama hao ambao mwishoe wakaja na mgomo. Mwishoe wanyama hao wakafanya kikao kizito ambacho kilikuja na azimio la kuweka amri saba au "seven commandments", amri ya kwanza ikisema Wanyama wote ni sawa yaani "All animals are equal".

Fasihi Simulizi nyingi zikiwemo "Room 101", "Thought police" "Big brother" na vingine zilikuwa zikitoa elimu tosha ya kukufanay msomaji ufikwe na fikra pevu.

Ni hichi cha Big Brother ndicho kilichompatia umaarufu Orwell kwa kubashiri raia kuwa wanachunguzwa na kufuatiliwa kwa kutumia njia mbalimbali zikiwemo Kamera maarufu kwa jina la CCTV na akaita hio itakuwa ni Big Brother State.
 
Kwa utandawazi wa sasa naona wamempa kiki kubwa yeye na kitabu chake kita zagaa mtaani ,sita shangaa kukiona kinondoni meza ya magazeti,

Sent from my SM-S920L using JamiiForums mobile app
 
Sartanic Verses au Aya za shetani ni kitabu cha Fasihi Simulizi ambacho kimetungwa kwa kuzingatia uhalisia maisha na matukio lakini kwa kumtumia mtume Muhammad na maisha yake.

Kitabu hichi kilitoka mwaka 1988 na TATIZO kubwa ni matumizi ya lugha ya kashfa inayokufuru dini ya kiislam na ambayo mwandishi Salman Rushdie aeleza kuwa ni chanzo cha ghasia, mauaji na misimamo mikali (Islamic fundamentalism).

Moja ya sifa kuu ya mwandishi wa Fasihi Simulizi ni uwezo wa matumizi ya lugha, upangaji wa wahusika katika simulizi hiyo , mazingira, hisia na hali. Hivyo Rushdie atumia lugha inoonekana (kwa wasomaji wa kijujuu) kama ya mzaha hivi na ndo hapo aonekana ametumia lugha ya kashfa.

Kitabu hichi kilipotoka tu waislamu duniani walilaani na hata kufikia kutishia maisha ya Rushdie na wale wote walokuwa wakisaidiana nae kutayarisha kitabu hichi na hata kufikia kupigwa marufuku kuingizwa nchini India.

Mwaka mmoja baadae yaani 1989 kiongozi wa Iran Ruhollah Khomeini ndie alieamuru Salman Rushdie auawe popote alipo agizo liloitwa Fatwa ambalo lilisababisha majaribio kadha wa kadha ya kuondoa uhai wa mwandishi huyo.

Katika simulkizi ya kitabu hichi Rushdie amewatumia wahusika wawili wakuu mwanamme aitwae Gibreel na mkewe aitwae Saladin.

Sasa, katika vitabu vya kiislam hususan Quran Gibreel ni malaika mkuu ambae yu karibu na mtume Muhammad, hivyo huwezi kumfananisha au kuhusisha na matukio ambayo hayamo katika misingi ya dini ya kiislam.

Kwa mfano Saladin amfananisha Gibreel na shetani kwamba amesababisha uokovu kutoka katika anguko la ndege walokuwa wakisafiria pale ilipotekwa nyara ikiwa angani na kuanguka lakini wao wawili kupona.

Saladin nae akakamatwa na askari wa uhamiaji ambao walinyanyasa kijinsia na kipelekea yeye kupata ukichaa. Hali hiyo ni tofauti kabisa na hali halisi kwamba Gibreel alikuwa ameoa mke.

Kosa jingine ni kumbadilisha jina Mtume Muhammad na kumwita Mahound au mjumbe na kuwa ana wapinzani wawili Hind na Baal na pia kuhusisha mtume Muhammad na danguro ambalo pia humo wamo wanawake malaya ambao watumia majina ya wake za mtume.

Na kosa la tatu linopigilia msumari kwenye jeneza ni pale Salman Rushdie katika kitabu chake anapomtumia Ayesha mwanamke wa kihindi ambae hudai kuwa apewa maono ya malaika Gibreel na kisha kwenda kuwaambia wanakijiji wote waende Mecca kuhiji lakini kwa kutembea juu ya bahari ya Arabia kitendo kilichopelekea wanakijiji wote kuingia baharini na kupotea.

Huo ndo mwongozo wa makosa yanosemwa ya mwandishi Salman Rushdie na kitabu chake cha Aya za Shetani.
Je ni kwa nini sasa Ayatollah Khomeini alitengua FATWA na kumsamehe Rushdie?
 
Back
Top Bottom