Sasa wewe kijana mwenzangu huna ajira alafu kwenye profile yako umeandika Self Employed ndo nini sas

shonkoso

JF-Expert Member
Mar 13, 2015
590
1,205
Tujifunze kuweka taarifa sasa kwenye mitandao ya kijamii kwani sasa Hivi,tunapitia kwenye mitandao ya watu kutafuta vijana ambao wameandika unemployed ni wachache sana almost. ni kama hakuna
 
Tujifunze kuweka taarifa sasa kwenye mitandao ya kijamii kwani sasa Hivi,tunapitia kwenye mitandao ya watu kutafuta vijana ambao wameandika unemployed ni wachache sana almost. ni kama hakuna
Tatizo vijana wengi hawajitambui wanaishi kinadharia zaidi..na ndio maana wanaficha uhalisia wao
 
Sasa kujiajir kwenyewe si ndo huku, ww ulitaka aandike self-employed akiwa amefungua kampuni yake, hata ukiwa unabeba mizigo stand, unakoroga zege hiyo ni self emloyed,
 
Yaaani hatari watu wote wamesoma UDSM hukuti SAUTI,SUA,UDOM,TEOFILI,ECKENFORD,IIRD,MOTC,KILOSA,DAKAWA TTC
Mkuu hivi vyuo ni vya TZ? sii maarufu hata kidogo...mbaya zaidi nusu ya watumiaji wa fb na Insta ndiko watokako.
 
Tatizo vijana wengi hawajitambui wanaishi kinadharia zaidi..na ndio maana wanaficha uhalisia wao

Thats correct Mkuu,Arl.

Ukiingia Fb wengi wetu tumeandika details za uongo kuhusu ajira,Employed/Self employed.Binafsi nafikiri ni kutokujitambua,Ulimbukeni pamoja na uzwaza wa kiwango kikubwa mno kwakuwa naweza kuita huko ni kutafuta "Kiki" kama vijana wa mjini wasemavyo.

Utakuta mtu ni Mwanafunzi lakini anaandika kuwa kajiajiri.Mtu hajawahi hata kwenda shule ila ataandika kasoma UDSM.Huu ni upuuzi.

Ningekuwa HR,ningekuwa nawaangalia waomba kazi katika mitandao ya kijamii kabla ya usaili.Nadhani huko kungenisaidia kumfahamu nitakayemuajiri kiundani kuliko kuagiza CV zilizojaa uongo pamoja na mataizi ya ajabu.

In-short waafrika wengi tunapenda ku-faking reality.Hatuishi uhalisia wetu.Tunaigiza maisha.Ndiyo maana ni rahisi sana mtu kwenda mjini na kuishi maisha tofauti na aliyokuwa anayaishi akiwa nyumbani/kabla ya kwenda mjini.
 
Sasa kujiajir kwenyewe si ndo huku, ww ulitaka aandike self-employed akiwa amefungua kampuni yake, hata ukiwa unabeba mizigo stand, unakoroga zege hiyo ni self emloyed,

Ndiyo wapi tena Mkuu??

Nadhani mtoa mada kawalenga wale wote ambao hawana ajira ya aina yeyote ila katika mitandao ya kijamii wanaandika kuwa waweajiriwa/wamejiajiri na siyo kama ulivyomaanisha wewe.

Anamzungumzia zaidi mtu amabaye ndiyo kwanza yupo Form two,hana ajira yeyote,anakula kwa wazazi,kulala nk then flash back katika mitandao anajiandika kuwa kajiajiri.

Anamzungumzia zaidi Mtu ambaye hana elimu yeyote ila anaandika kuwa kamaliza UDSM,tena Bachelor ya Civil Eng wakati ni uongo mtupu.

Nadhani mtoa mada alikuwa na mlengo huu.
 
Back
Top Bottom