Sasa vita mpya CHADEMA, CCM
ΒHuu ni ukweli usiopingika. Sasa kama yasemwayo siyo ya kweli mbona Mheshimiwa Rais wetu JK anakaa kimya? Inabidi ayatolee majibu.
Maswali muhimu ambayo anapaswa kuyajibu ni haya
1. Je ni kweli kuwa CCM ina Green Guard?
2. Wana maana gani kukataa miiko ya viongozi kwenye katiba?
3. Hawa wananchi wanaouwawa au walioumizwa na vyombo vya dola kwake ni sherehe ya Arusi?
4. Je, ni lini watu watakuwa huru kujieleza na kutoa mawazo yao bila kuonekana wasaliti?
5. Je anafikri CCM ITAKUWA MADARAKANI MILELE?
6. Mikataba inayotolewa kwa ubinafsi au kwa maslahi ya waziri fulani anachukua hatua gani?
7. Kauli zinazotolewa na mawaziri wake zinamfurahisha kwa kaisi gani? Mbona hawachukuliwi hatua za kinidhamu?
8. Kweli haoni jinsi Speaker ( ambaye ameshapoteza sifa yake na wengine kumwita Bibi Kiroboto) anavyoharibu chombo hiki chenye hadhi kubwa nchini? Uonevu wa wazi wazi kwa wanaopinga interest zake na hatua za kuwafukuza wapinzani kwenye vikao eti kwa sababu ya kusema ukweli bila kutafuna maneno hayaoni? Ushauri wa bure Mheshimiwa Rais, hatuna Speaker Tanzania, chukua hatua anakuabisha sana anaposhindwa kusimamia sheria. Labda ungemwomba Mzee Sita arudi amalizie kipindi hiki kigumu ili kurudisha matuamini ya WAtanzania.
9. Waziri mkuu kusema polisi wapige raia ana maana gani? Tuonaomba umtume nchi zilizoendelea aone jinsi police wanavyofanya hatakama kuna maandamano ya kuipinga serikali. Natumaini umeona huko Brazil kwa mwezi huu uliopita ilivyokuwa. Police wamemwua nani? Nenda nchi kama Italia ambako kuna migomo kila mwezi na maandamano unasikia yanayotoke Tanzania, police kuua raia?
10. Tunakuomba ukae chini na wazee wenye hekima ujadili hali halisi ya nchi yetu. Tunaangamia tukitazama kwa macho. Hiyo ya chadema kusema wanataka kuanzisha Red yao, ilikuwa chanzo cha kuibua haya yote. Mbona kuna Sungusungu ya Mrema, ilikuwa tishiyo. Yote ni kwa sababu polisi wako wameshindwa kufanyakazi yao ipasavyo
tafakari