Sasa Tunaanza kuulizana Kwa vipi uwanja huu ni mali ya CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa Tunaanza kuulizana Kwa vipi uwanja huu ni mali ya CCM?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by nngu007, May 14, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora.
  [​IMG]


  Sehemu ya ndani ya uwanja huo.
  • Habari ambazo ninazo kutokana na kuhoji wakazi kadha wa kadha wa mkoa wa Tabora, uwanja wa Ally Hassan Mwinyi ni mali ya chama tawala CCM. Lakini nilipohoji ni nani aliyeujenga uwanja huo nikaambiwa ulijengwa na mkuu wa mkoa huo wa zamani hayati Lawrence Gama ambapo baadhi ya bidhaa ziliongezwa bei kidogo ili kupata fedha za kuujenga uwanja huo mpaka hapo ulipofikia. Sasa kwa maelezo hayo machache inamaanisha uwanja huo ni mali ya wakazi wa mkoa huo na si CCM kama ilivyo sasa, au labda tungeambiwa unamilikiwa na serikali ya mkoa wa Tabora ingeeleweka. Na tatizo hili halipo Tabora tu bali hata Dar es Salaam, ambako pana majengo mengi Chama kimejigawia likiwemo la umoja wa vijana pale mtaa wa Lumumba na Morogoro rd na yale yote ya umoja wa wanawake na taasisi nyingine znazomiliki majengo. Chama kilijigawia rasilimali hizo pale Tanzania ilipoingia katika mfumo wa vyama vingi, lakini sioni pana mantiki gani wajimilikishe huku mali hizo zilikuwa za vijana wa Tanzania sio wa CCM. Na wapiga kelele sijapata kuwasikia wakilizungumzia hili. Wadau anayelijua vizuri suala hili tafadhali anieleweshe pengine wana uhalali wa kumiliki majengo hayo.
   
Loading...