Sasa Raisi apunguze baraza la mawaziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa Raisi apunguze baraza la mawaziri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Richard, Feb 7, 2008.

 1. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2008
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Baada ya hekaheka ya pale Bungeni Dodoma naona huu ni wakti mzuri wa kukaa kitako na kuunda baraza jipya la mawaziri tena dogo lenye idadi ndogo ya mawaziri na manaibu.

  Halafu pia naona raisi achague mawaziri kutoka mikoa kona zote za Tanzania.

  Pia namshauri mheshimiwa raisi, asipange wabunge aliowachagua yeye kupitia viti maalum kama mama Rwakatare kwani haitaleta haki kwa wapiga kura.

  Sasa mtazamo wa baraza jipya la mawaziri ambalo ni la watu 22 ningependa mheshimiwa raisi aunde ni kama ifuatavo:

  Waziri Mkuu

  Naibu Waziri Mkuu

  Waziri wa Mazingira, Maendeleo Endelevu na Makazi

  Waziri wa Fedha na Uchumi

  Waziri wa Sheria, Katiba na Serikali za Mitaa

  Waziri wa Afya na Huduma za Jamii

  Waziri wa Elimu (kwa ujumla), Watoto na Ujuzi

  Waziri wa Maendeleo Vijijini na Ushirika

  Waziri wa Mambo ya Ndani

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Kimataifa

  Waziri wa Utamaduni na Michezo

  Waziri wa Biashara na Nishati

  Waziri wa Miundombinu na Usafiri

  Waziri wa Kazi

  Waziri wa Utalii na Maliasili

  Waziri wa Habari na Mawasiliano

  Waziri wa Sayansi na Teknolojia

  Waziri wa Uvuvi na mambo ya Baharini

  Waziri wa Kilimo na Chakula

  Waziri wa Uraia na Uhamiaji

  Waziri wa Viwanda

  Waziri wa Usalama wa Raia

  Mwanasheria mkuu wa Serikali

  Na Katibu wa Baraza  Naomba kutoa hoja
   
 2. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Richard,

  Ushauri mzuri sana huo. Lakini pia ukichunguza sana utagundua kuwa nyingi ya wizara hapo zinaweza tu kuwa idara au kurugenzi za serikali na kazi ikafanyika badala ya kuwa na mzigo wa kuweka wanasiasa kuziendesha.

  Wizara kumi ni nyingi sana.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,457
  Likes Received: 81,708
  Trophy Points: 280
  Mawaziri ishirini mpaka ishirini na tano wanatosha kabisa na siyo kila wizara inahitaji kuwa na naibu waziri. Hii itapunguza gharama kubwa za uendeshaji serikalini.
   
Loading...