Technology
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 769
- 284
aiseeee tatizo la umeme linakera saana... nimechoshwa na story nyingi
Ni hayo maamuzi magumu ndio ambayo tunadhani yangeweza kuleta suluhu katika yote...Tumsikilize Mhe. Jaji Warioba katika kipindi cha dakika 45 ITV atalonga nini manake katika dondoo tu inaonekana nae analaumu utawala uliopo kwa kudhani bado upo katika kipindi cha kufanya kampeni badala ya kutekeleza mikakati ya kuwaletea wananchi maendeleo...
Kumsafisha Lowassa haihitaji hata dodoki, si mda mrefu mr. White atang'ara ile mbaya. Watanzania tuna vipaji vya kusahau. 2015 Lowassa ndani ya ikulu.
Mkuu ulichoongea ni sawa kabisa na ndiyo ukweli wenyewe huo.Ila tatizo ni kwamba Lowassa amechafuka sana na hawezi kusafishika hata
kwa dodoki la chuma.....but the guy is so good
mkuu umenena vema, LOWASSA alikuwa anachapa kazi si mchezo eg alihangaika ili kupata artificial rain, alipita hata sehemu mbovu kama LUMAGE huko Makete kuangalia chanzo cha UMEME wanachotumia wao nk Ndiyo maana watu wanasema 2015 the BEST present from CCM is EDWARD LOWASSA kimsingi huyu MBUNGE ni mchapa kazi ila basi tu
Mkuu Ngoshwe,...Tumsikilize Mhe. Jaji Warioba katika kipindi cha dakika 45 ITV atalonga nini manake katika dondoo tu inaonekana nae analaumu utawala uliopo kwa kudhani bado upo katika kipindi cha kufanya kampeni badala ya kutekeleza mikakati ya kuwaletea wananchi maendeleo...
Warioba alishazibwa mdomo kwa kashfa ya Mwananchi Gold. Akithubutu kuchonga tu kesho utasikia ametinga Kisutu. Hakuna aliye msafi huko
hahaha, unaona, watu walikuwa wanachapa kazi kinguvu, kama hawataki kuchapa kazi walikuwa wanalazimishwa...sasa ona mwendo wa kibagamoyo tulionao sasa na huyu ******...hamna lolote. kama tatizo lilikuwa ni lowasa, mbona hadi leo hii wakati issue ya richmond imeshapotea na haihusiani na kinachoendelea sasaivi, umeme umekuwa tabu kuliko hata kipindi cha lowasa, kwani kipindi kile cha lowasa tulikuwa kwenye wakati mgumu kama tulivyo sasaivi? this is a worse staff aisee kwasasa, watu mara ngereja, mara kikwete etc....tujifunze kutokwenda mbaali kwa jambo kawaida kama ilivyokuwa kwenye richmond....lowasa kwa urais 2015 oyeeeeee. na atapita.That time nakumbuka mkuu siku moja nilikua na appointment na Mkurugenzi mmoja wa Halmashauri nilimkuta ofisini akitetemeka na aliahirisha appointment yangu kisa next week kulikua na ziara ya Lowasa wilayani mwake.
katika hayo yote hapo juu sijaona hata moja lilofanikiwa zaidi ya kuongezeka kwa gharama za umeme ( sababu kuu ikiwa ni ufisadi/fursa ya kufanya biashara), kuongeza kwa ajali barabarani, Kuongezeka kwa rushwa na wizi ( kwenye suala la ruzuku kwenye pembejeo). Kutoa maamuzi ya kukurupuka na hatima yake serikali kushindwa kesi za madai. hayo yote uliyoorodhesha hapo ni mambo ya kitaalam na si ya kisiasa na tanzania kuna wataalamu wengi sana wa nishati, ujenzi nk> tatizo la wanasiasa ni kutaka kutatua matatizo huku wakiangalia kama watapata fursa ya kufanya biashara au ufisadi kwenye kila tatizo letu. Kwenye suala la uraisi nadhani kila mtanzania ana haki ya kikatiba kugombea nafasi yeyote... Ila kwa EL itabidi ajibu swali aliloulizwa na Mwalimu JKN....mali zote kazipata wapi????Nia si klumtetea Lowasa wala Mtu yeyeote ambae anatuhumiwa kwa kuchangia kurejesha nyuma maendeleo ya nchi hii. Ila kwa hali ilivyo sasa hata kama huwezi kushawishika unaweza kuona jinsi ilivyotofauti kuwa na Kiongozi wa mfano wa Lowasa katika mfumo wa utawala wetu...ni mangapi tumekuwa tukielezwa kwa nadharia na hakuna vitendo?
Lowasa pamoja na ufisadi wake lakini aliweza kuthibutu katika mambo mengi magumu:
(i) alidiriki kulitafutia ufumbuzi tatizo la umeme hafi likamchafua kisiasa:
(ii) alibuni mipango mbadala ya kuzuia foleni jiji la Dar ikiwemo njia tatu na kutambua barabara za pembeni ya mjini ambazo sasa zimeshindwa kuendeklezwa;
(iii) alisimamia mpango wa ujenzi wa shule za kata na zahanati japo hazikuwa na mtizamo wa muda mrefu ikiwemo kuandaa wauguzi na waalimu;
(iii) Ndie aliesaidia kwa kiasi kikubwa kuleta ufumbuzi wa tatizo la maji kwa baadhi ya miji japo hali bado inasuasua;
(iv) aliwezesha mpango wa ruzuku za pembejeo kwa wakulima japo uzalishaji katika sekta ya kilimo haukjakaa vizuri;
(v) aliweza kuchukua maamuzi magumu ya papo hapo ikliwemo kuwafukuza watendaji wabovu pasipo kujali ni nani mwenye dhamana ya kuwachukulia hatua za nidhamu (juzi mmesikia wenyewe Mwenzake akitamba i hadharani "kama yeye angekuwa Rais angemfukuza kazi Jairo) lakini baadae tunatangaziwa amesimamishwa ili kuchunguzwa kwanza....na wanaomchunguza ni wale wale wanaoendelea kutuhumiwa kuhusika katika kashfa nyingine ikiwemo kushindwa kushauri ipasavyo kwenye suala la Richmond...
Kumtetemekea mtu si kwamba ndio ishara ya kwamba huyo mtu anafanyakazi sana. nadhani alitetemeka kwa sababu hakujua atakuja na maamuzi gani (ya kukurupuka bila utafiti wa kutosha ) Hata chizi akiwa anakuja ofisini kwako lazima utatemeka piaThat time nakumbuka mkuu siku moja nilikua na appointment na Mkurugenzi mmoja wa Halmashauri nilimkuta ofisini akitetemeka na aliahirisha appointment yangu kisa next week kulikua na ziara ya Lowasa wilayani mwake.