Sasa nimemwelewa Mh Lowassa!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa nimemwelewa Mh Lowassa!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ngoshwe, Jul 23, 2011.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  [​IMG]


  Wakati ule alipochukua uamuzi mgumu wa kujiuzulu, alisema, " ETI KISA NI UWAZIRI MKUU" ni kama vile alikuwa mtu aliyekuwa ameshinikizwa na mtu fulani kujiuzulu ili kupisha kelele za watanzania baada ya kubaini nae alihusika katika kashfa ya Richmond.......lakini wakati ule nilidhani Lowasa alikuwa hajui analofanya kwa kukubali kwake kuwajibika hadharani akasema, ...."najiuzulu".

  Wengi tulidhani baada ya kujiuzulu Mhe. Lowasa mambo ya Nishati ya Umeme katika nchi hii yata kaa vizuri kwani ni kipindi kile kile ambapo tulitangaziwa mikakati kibao Bungeni na Kwenye hotuba ya Mhe. Rais ile ambayo sasa hatuisikii ya kila mwezi kuwa tatizo la umeme litakuwa historia...

  Kumbe sasa kwa fikra za wazi mnaweza kubaini tatizo halikuwa na wala sio Lowasa..., Lowasa alijitahidi kadiri ya uwezo wake kutimiza maagizo ya mkuu..haya tunayaona sasa ni yale yale yaliyomtokea Lowasa, yamemgusa Mhe. Waziri Mkuu mwingine Pinda, sasa kwa staili nyingine ya posho za kuwahonga wapitisha bajeti kwa kutaka wafunike kombe ili bajeti ya nishati ipite mabo yaendelee kama kawaida.., Awali Mhe. Waziri Mkuu alionyesha kughazabika eti haya mambo ya "posho za kulainisha maamuzi" hayapo Serikalini.

  Safari hii kupitia Mtendaji Mkuu wa Wizara ile ile ya Nishati Bw. David Jairo..huyu ambae alikuwa ni Mtumishi muadilifu, mtaalamu wa Sheria, ambaye alipata kufanya kazi kwa karibu sana na Mkuu wa nchi kule IKULU akiwa ni msaidizi wa Mkuu wa Nchi chini ya Katibu Mkuu Kiongozi wa sasa (aliyetoka Wizara ya Mambo ya Nje na Mkuu wa Nchini) ambaye ametangaza kuanza hatua za kumwajibisha Jairo ili hali nafasi yake ya Ukatibu Mkuu Nishati inatangazwa kupangiwa mtumishi mwingine (Eliakim Maswi).

  Hapo napo tena ni funika kombe mwaharamu apite kama ilivyokuwa kwa wale watendaji waliotajwa kuhusika na kashfa ya Richmond...(Jairo atapangiwa kazi nyingine) http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=31495

  .Eti Jairo sasa anaonekana kikwazo cha upatikanaji wa UMEME, kama ilivyokuwa kwa Mhe. Lowasa, Je, ni wapi Jairo alipata ujasiri na kiburi cha wa kuandika yale aliyoandika kuziagiza taasisi anazozisimamia kama haikuwa mazoea au hakupata maagizo yoyote toka kwa mtu fulani wa juu yake?

  (Waziri wake, Waziri Mkuu na Mkuu wa Nchi hawakujua haya ambayo yaliandikwa,
  kutumwa na kuhifadhiwa kwenye majalada ya umma kwa lengo la kuomba fedha amazo zinaingia kwenye akanuti ya taasisi nyingine ya umma kwa lengo la kuhonga watendaji)? .....Mhe, Msabaha wakati ule nae aliponzwa kwa kuandika madokezo ya kuagiza wa chini yake...lakini alipokuwa akichomoka akitoa kauli ambayo iliashiria kuwa nae aliagizwa na mkubwa wake wa kazi kufanya yale aliyofanya na wakati ule tukasema ni "Lowasa tu huyo...'

  Lakini kauli za kujiuzulu kwa Lowasa nazo zilionyesha kana kwamba nae aliagizwa kufanya vile na mtu mwingine wa juu yake ...ni nani? hatukujua! (LOwasa akachafuka)!...... Sasa tumefumba macho kabisa, hatuna mjadala tena juu ya kulipa sdeni la Mrithi wa RICHMOND yaani DOWAS hasa baada ya Wakuu wa Dunia hii (Marekani) kuingilia kati kwa staili ya
  Symbion Power, ...........tunamjadili Jairo.....

  Hatujui kumbe hapa tulipo, tunachohitaji ni umeme, umeme kwa gharama zotote zile (hayo ndio maamuzi magumu ambayo Lowasa aliyasimamia na yakamfanya aonekane hafai). Tulidhani Lowasa ndio kikwazo cha maendeleo ya nchi hii, eti kumbe hata baada ya kujiuzulu kwake bado matatatizo ni yale yale tena sasa ni mazito zaidi..tumeona bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini imeashindwa kupita kwa kile kinachodaiwa kukosa mikakati ya kuondoa tatizo la Umeme na wakati huo Katibu wake Mkuu kung'olewa kwa kashfa ya kutaka kuiwezesha bajeti hiyo ipite kimya kimya...eti sasa si Waziri Msabaha, Karamagi wala Lowasa wameshiriki katika hili sakata....
   
 2. BABA JUNJO

  BABA JUNJO JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uko sawa kabisa brother.
   
 3. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu ulichoongea ni sawa kabisa na ndiyo ukweli wenyewe huo.Ila tatizo ni kwamba Lowassa amechafuka sana na hawezi kusafishika hata
  kwa dodoki la chuma.....but the guy is so good
   
 4. M

  Mlugaluga Member

  #4
  Jul 23, 2011
  Joined: Jun 6, 2006
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu, history is a good judge.
   
 5. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu ni kama unataka kusema kwamba Lowasa hakuwa tatizo kwasababu walifuata baada yake hawajatatua matatizo? Unataka kutuambia kwamba aking'olewa kiongozi fisadi na nafasi yake ikachukuliwa na kiongozi mwingine ambae baadae akaonekana ni fisadi pia basi inatosha kusema yule wa kwanza kung'olewa sio fisadi.

  Binafsi ninaamini matatizo yaliyopo sasa hivi kwa kiasi kikubwa ni mfumo mbovu uliopo. Inawezekana kweli suala ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kupitisha bajeti ni utaratibu wa kawaida kabisa ila Jairo anang'olewa kwasababu story zime-leak kwa umma. Lakini, kwa nini mtu akipewa nafasi basi akubali kufuata mazoea mabaya badala ya kufanya kazi kwa uadilifu? Bora kung'olewa kisa umekataa kufuata mazoea mabovu kuliko kung'olewa kisa umefuata utaratibu mbovu ulio zoeleka halafu uanze kulalama eti umetolewa kafara.

  Kila mtu ajipange kwa kufanya kazi kwa uadilifu kwasababu sifagilii kujifanya kwamba umetolewa kafara ... tutaangalia kwanza, ulifanya kosa au la?
   
 6. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kama lowassa alijiuzulu huku akijua makosa yalitokea ngazi ya juu yake(Jk) kwa nini hakushtaki kwa wananchi ili wasimpe kura JK?
  Lowassa alishachafuka,ccm pamechafuka na hakuna wa kumyooshea kidole mwenzake.tunahitaji mabadiliko(system overhaul) siamini kama mabadiliko haya yatatoka ccm.
   
 7. H

  Hute JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,053
  Likes Received: 3,920
  Trophy Points: 280
  tatizo halikuwa lowasa, lowasa ni safi ndo maana atakuwa rais wa nchi/inji hii mwaka 2015. period.
  ona alivyokuwa anachapa kazi, tungeendelea na kasi ile, tungekuwa mbali pamoja na kwamba wengi wangekuwa wameumia, napenda rais wa aina ya lowasa kuliko rais wa aina ya kikwete......it hasn't been proven kwamba lowasa alikula rushwa hadi leo, rushwa hiyo haionekani, wala fungu hilo la kumbi halionekani.....which means jamaa walimwonea tu, ndo maana hata anavyoondoka alisema naachia ngazi, tena kwa majonzi akijua hakufanya kitu kwa nia mbaya....kama yalitokea matatizo yalitokea kwasababu tu kiutendaji na haikuwa necessary kwenda mbaliiii kiasi kile kwa kina mwakyembe na wengine....
   
 8. F

  Ferds JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  hizi mbio za urais 2015 zitgawanya watanzania hasa ndani ya CCM, makala nyingi hivi sasa ni za kusafisha walio wachafu, historia ya lowassa ni mbovi na wizi tangu aanze AICC, uwaziri wake ktk wizara mbalimbali, hadi uwaziri mkuu, hakuna asiyejua kuwa Lowassa hakupaswa kuwa waziri mkuu ila ni mkono wa playmaker Rostam Azizi, maamuzi magumu ili kuficha ufisadi hatuyataki....................................
   
 9. k

  kamimbi Senior Member

  #9
  Jul 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu tusidandanyane, Lowasa, Rostam pamoja na Jairo wamechemsha kwa sababu tofauti tofauti, hakuna wa kutetewa hata mmoja, yaliyo wapata ni halali yao, wao wanajua vizuri mipaka ya kazi zao, hawakushinikizwa na mtu yeyote ktk kutekeleza yaliyo sababisha wakachafuka kama walivyo.
  kidogo naweza kumtetea Msabaha, huyu alitolewa kama kondoo wa kafara, hawa wengine mkuu naomba tusiwasafishe kwa njia kama hii, but im sorry mkuu kama nitakuwa nimekukwaza, ukweli ndo huo.
   
 10. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  mkuu umenena vema, LOWASSA alikuwa anachapa kazi si mchezo eg alihangaika ili kupata artificial rain, alipita hata sehemu mbovu kama LUMAGE huko Makete kuangalia chanzo cha UMEME wanachotumia wao nk Ndiyo maana watu wanasema 2015 the BEST present from CCM is EDWARD LOWASSA kimsingi huyu MBUNGE ni mchapa kazi ila basi tu
   
 11. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Naona umemtizama kwa jicho la tatu.
   
 12. Cheche Mtungi

  Cheche Mtungi JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,487
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  .................but the guy is so good.
  MH! MPAKA 2015 MAJIBU YATAPATIKANA TU!
   
 13. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #13
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nia si klumtetea Lowasa wala Mtu yeyeote ambae anatuhumiwa kwa kuchangia kurejesha nyuma maendeleo ya nchi hii. Ila kwa hali ilivyo sasa hata kama huwezi kushawishika unaweza kuona jinsi ilivyotofauti kuwa na Kiongozi wa mfano wa Lowasa katika mfumo wa utawala wetu...ni mangapi tumekuwa tukielezwa kwa nadharia na hakuna vitendo?
  Lowasa pamoja na ufisadi wake lakini aliweza kuthibutu katika mambo mengi magumu:

  (i) alidiriki kulitafutia ufumbuzi tatizo la umeme hafi likamchafua kisiasa:
  (ii) alibuni mipango mbadala ya kuzuia foleni jiji la Dar ikiwemo njia tatu na kutambua barabara za pembeni ya mjini ambazo sasa zimeshindwa kuendeklezwa;
  (iii) alisimamia mpango wa ujenzi wa shule za kata na zahanati japo hazikuwa na mtizamo wa muda mrefu ikiwemo kuandaa wauguzi na waalimu;
  (iii) Ndie aliesaidia kwa kiasi kikubwa kuleta ufumbuzi wa tatizo la maji kwa baadhi ya miji japo hali bado inasuasua;
  (iv) aliwezesha mpango wa ruzuku za pembejeo kwa wakulima japo uzalishaji katika sekta ya kilimo haukjakaa vizuri;
  (v) aliweza kuchukua maamuzi magumu ya papo hapo ikliwemo kuwafukuza watendaji wabovu pasipo kujali ni nani mwenye dhamana ya kuwachukulia hatua za nidhamu (juzi mmesikia wenyewe Mwenzake akitamba i hadharani "kama yeye angekuwa Rais angemfukuza kazi Jairo) lakini baadae tunatangaziwa amesimamishwa ili kuchunguzwa kwanza....na wanaomchunguza ni wale wale wanaoendelea kutuhumiwa kuhusika katika kashfa nyingine ikiwemo kushindwa kushauri ipasavyo kwenye suala la Richmond...
   
 14. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Ngoshwe, kama hakufanikiwa katika yote hayo uliyoainisha juu tena iweje mtu huyo awe ni msafi? Ina maana mipango yake ni ya kukurupuka na alikuwa hasikilizi ushauri, mambo ambayo yalimgharimu na yanendelea kumgharimu.

  Kufukuza watu bila ya kufuata utaratibu inadhihirisha wazi kwamba alikuwa hafahamu vipi serikali ilitakiwa ishughulikie issue kama ile. Itakuwaje yeye Waziri Mkuu amfukuze engineer wakati kuna viongozi wa kati wengi tu ambao wangeweza kufanya hiyo shughuli? Sasa WAziri Mkuu akianza kupita njiani na kufukuza watu ovyo ovyo unadhani hiyo ndiyo ingekuwa bora?

  Si umeona matokeo ya kufanya vitu bila ya kufuata sheria? Matokeo yake ni Serikali ndiyo inalipa tena fidia kubwa zaidi ..... mfano yale majumba ya masaki yaliyovunjwa imefikia wapi?
   
 15. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Hivi huyu Jairo kama ni mchafu hivi na alikuwa shoga yake huyu Jamaa msafiri, haina maana kuwa hata huyu msafiri ni hao hao!
   
 16. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  MAJI ziwa Victoria mpaka KAHAMA pamoja na kuwepo mkataba wa kikoloni kuzuia watz wasitumie maji yale
   
 17. M

  Major JF-Expert Member

  #17
  Jul 23, 2011
  Joined: Dec 20, 2007
  Messages: 1,425
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  Mkuu jaribu kutumia kichwa kufikiri na siyo "marufi"
   
 18. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #18
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Jamani tuenzi maneno ya mwalimu juu ya Lowasa tusije pata laana ya baba wa taifa uko aliko.
  Nasikia alimwambia kijana utajiri wote huu umeutoa wapi?
   
 19. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #19
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  wakati mwingine najiuliza hapa,,inshu ni huyu bwana kuwa tajiri ama ufisadi. na kama ni ufisadi ni upi na upi aliofanya specifically? kiutendaje huyu nywele nyeupe alikuwa zaidi,zaidi sana ya wengi watumishi wa serikali waliomfuata including Pinda
   
 20. kabila01

  kabila01 JF-Expert Member

  #20
  Jul 23, 2011
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 3,014
  Likes Received: 1,823
  Trophy Points: 280
  That time nakumbuka mkuu siku moja nilikua na appointment na Mkurugenzi mmoja wa Halmashauri nilimkuta ofisini akitetemeka na aliahirisha appointment yangu kisa next week kulikua na ziara ya Lowasa wilayani mwake.
   
Loading...