Sasa nimeanza kumuelewa mh. Zitto Kabwe

Sasa nimeanza kumuelewa mh. Zitto Kabwe

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,697
Reaction score
164,971
Sikuu chache zilizopita(haizidi week), mh.Zitto,alisema kuwa kashifa ya Tegeta Escrow account inaweza kumuangusha "tembo mkubwa".

Baada ya kauli ile,nilijiuliza swali moja tu,huyu tembo mkubwa ni nani?Baade nikajisemea(kwa uzoefu wa siku za nyuma) atakuwa ni PM wetu ingawa nilibaki na duku duku moyoni mwangu.

Hat hivyo,nashukuru leo nimepata jibu na dukuduku langu ambalo nilikuwa nalo, sasa limeisha, kwani leo nimepata jibu sahihi zaidi kuhusu huyu "tembo mkubwa" ni nani.

Kweli hakuna siri chini ya jua na siri ni ya mtu mmoja na si zaidi.

Ahsante Zitto japo uliniboa sana kuwaita viongozi wa UKAWA wasaka tonge.

Pia,shukrani @Yericko nyerere

Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.
 
Last edited by a moderator:
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.[/QUOTE]Yericko kasema wamiliki wa 50% PAP ni Salma na Miraji. Huyo PM akidondoshwa atakuwa kaonewa tu.
 
Ngoja waje akina mjepo, lizaboni na wenzao mukione cha moto...
 
Hii post haijaonwa na Nguluvi3 na Mchambuzi wake. Wao na Zitto tu masuala mengine hawajui. Dah! Eti ndo GT wa humu
 
Ngoja waje akina mjepo, lizaboni na wenzao mukione cha moto...
Mkuu, hizi ni porojo tu. kwa taarifa yako ni kwamba huyu Salary Slip ni Kambi Zitto. Slip aliasi chama wakati wa sakata la Zitto ndani ya chama chao. Sishangai leo kuanzisha uzi kumsifu Zitto.
 
Mkuu, hizi ni porojo tu. kwa taarifa yako ni kwamba huyu Salary Slip ni Kambi Zitto. Slip aliasi chama wakati wa sakata la Zitto ndani ya chama chao. Sishangai leo kuanzisha uzi kumsifu Zitto.

Kinachoniburudisha sana humu ndani ni kwamba mnafahamiana sana...
 
Hii post haijaonwa na Nguluvi3 na Mchambuzi wake. Wao na Zitto tu masuala mengine hawajui. Dah! Eti ndo GT wa humu

kwanini uwasakame wao tu? kwani wewe sio GT? kama ndiyo, mbona wewe umeiona? kunaulazima gani wa wao kuiona
 
Hii post haijaonwa na Nguluvi3 na Mchambuzi wake. Wao na Zitto tu masuala mengine hawajui. Dah! Eti ndo GT wa humu

Mbona kijana inakuwa mgumu kuelewa?

Usichojua kuhusu Zitto ni nini?

Zitto ni fisadi na hana uadilifu na uaminifu
 
naanza kuamini tetesi zinazodai kuwa kuna mpango wa kuinusuru CCM isimeguke uchaguzi ujao kwa kutenegeneza mazingira ya kumteua mtu ambaye ni neutral (PINDA) na kuwapiga chini wgombea wenye makundi yaani EL,MEMBE,SITTA.

kwa maana hiyo basi kwa sasa kuna uwili mtakatifu kati ya JK na PINDA, ambao umejificha katika utendaji wa serikali,

ndo maana ukiangalia sakata la Escrow limekaa ki mtandao JK-PINDA kwamba JK anaonekana kumuhusisha pinda ili ipatikane hela ya kampeni 2015, wakati huo jk atapiga mihela ya capacity charge kupitia PAP & SIMBa TRUST,

kuna issue nyingine imeibuka muda sio mrefu kwamba uwili huu unahusika na mpango wa kifisadi wa kuiuza TTCL kwa kampuni ya VIETEL ya vietenam kumbuka ziara ya juzi ya mkulu vietenamu

ukichunguza kwa jicho la kiinteligensia utaona kwamba JK amemshawish PINDA agombee uraisi 2015 ili alinde maslahi ya dili zake ambazo Pinda amehusika ili kubalance mambo,

inabidi pinda ajiulize mara 2,2 je anamwamini huyu kigeugeu, kama ameisha wageuka maswahiba zake karibu wote, je issue ikisanuka si yatakuwa kama ya richmond??? Tusubiri muda utaongea
Sikuu chache zilizopita(haizidi week), mh.Zitto,alisema kuwa kashifa ya Tegeta Escrow account inaweza kumuangusha "tembo mkubwa".

Baada ya kauli ile,nilijiuliza swali moja tu,huyu tembo mkubwa ni nani?Baade nikajisemea(kwa uzoefu wa siku za nyuma) atakuwa ni PM wetu ingawa nilibaki na duku duku moyoni mwangu.

Hat hivyo,nashukuru leo nimepata jibu na dukuduku langu ambalo nilikuwa nalo, sasa limeisha, kwani leo nimepata jibu sahihi zaidi kuhusu huyu "tembo mkubwa" ni nani.

Kweli hakuna siri chini ya jua na siri ni ya mtu mmoja na si zaidi.

Ahsante Zitto japo uliniboa sana kuwaita viongozi wa UKAWA wasaka tonge.

Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom