Sasa nimeamini ni kwanini nchi tajiri kama Tanzania haina maendeleo

GedsellianTz

JF-Expert Member
Jul 5, 2016
1,335
1,778
Katika uchunguzi wangu niliofanya nimegundua tatizo kubwa la nchi yetu kuwa nyuma kiuchumi na maendeleo ni sababu tulikuwa tunaongozwa na watu walio na elimu feki na vyeti feki, siasa na undugu vilitawala, watu wasio kuwa na sifa stahiki waliweza kukamata nyazifa mbalimbali katika serikali yetu na kuwaacha watu wenye ujuzi na waliosomea wakihangaika na kutafuta ajira kila kukicha, naimani kubwa toka mwanzo watu sahihi wangekamata nafasi sahihi walizotakiwa kushika tanzania ingekuwa ni nchi moja yenye utajiri wa hali ya juu.
 
huo uchumguzi utakua feki tu..............maana wanao/waliotuongoza hawajawah kaguliwa vyeti...........cc maskin kwakuwa wanaotuongoza wanatakiwa wajue kusoma na kuabndika tu
Sio feki mkuu, maana hata hao ambao hawakaguliwi vyeti wamejaa uozo tupu, ndio maana hatuwezi kuendelea wametanguliza matumbo kwanza kuliko utaifa
 
Katika uchunguzi wangu niliofanya nimegundua tatizo kubwa la nchi yetu kuwa nyuma kiuchumi na maendeleo ni sababu tulikuwa tunaongozwa na watu walio na elimu feki na vyeti feki, siasa na undugu vilitawala, watu wasio kuwa na sifa stahiki waliweza kukamata nyazifa mbalimbali katika serikali yetu na kuwaacha watu wenye ujuzi na waliosomea wakihangaika na kutafuta ajira kila kukicha, naimani kubwa toka mwanzo watu sahihi wangekamata nafasi sahihi walizotakiwa kushika tanzania ingekuwa ni nchi moja yenye utajiri wa hali ya juu.
naomba mods waunde kamati uchunguzwe uwezo wako wa kufikiri
 
Katika uchunguzi wangu niliofanya nimegundua tatizo kubwa la nchi yetu kuwa nyuma kiuchumi na maendeleo ni sababu tulikuwa tunaongozwa na watu walio na elimu feki na vyeti feki, siasa na undugu vilitawala, watu wasio kuwa na sifa stahiki waliweza kukamata nyazifa mbalimbali katika serikali yetu na kuwaacha watu wenye ujuzi na waliosomea wakihangaika na kutafuta ajira kila kukicha, naimani kubwa toka mwanzo watu sahihi wangekamata nafasi sahihi walizotakiwa kushika tanzania ingekuwa ni nchi moja yenye utajiri wa hali ya juu.
Hata nchi zilizo endelea hufoji vyeti......
 
Well lingine linatudidimiza ni kwamba people of the same circle ndio wanapewa nafasi.

Mfano Snr Mgimwa kafa mwane kapewa jimbo. Kigoda, celina kombani,rizmoko,mama rizmoko hii ina multiply effect kwenye jamii yote
Ukienda polisi na jeshini,mabenk,sekta binafsi ,serikalini,utakuta wengi baba zao walikuwa huko wakawachomeka watendaji wa sampuli hii huwa hawajitumi, hawana uchungu sababu baba yupo na amekulia kwenye maisha ya raha sababu baba aligharamia hawezi kulitumikia taifa.

Na ukute na vyeti navyo labda alifoji na kusoma chuo alibebwa mfano DAB alivyobebwa Muccobs. Nchi haiwezi kuendelea hata siku moja
 
Well said to broo, umenena ukweli mtupu kwa namna hii nchi haiwezi kuendelea hata kidogo
 
Kwani vyeti feki vimetokana na serikali ya chama gani..?
Umeanza uchochezi, ila nina imani ni ile ya kijani.....kuna watu walifojiwa vyeti ili waingizqe kwenye system sasa system hiyo hiyo imegeuka.
 
umasikini wetu unatokana na Mimi kwanza wengine watajijulia. Na hata wanaoingia kwa nia ya dhati kuleta maendeleo anapambana na vizingiti vya wapigaji.Uzalendo wa Tanzania kwanza haupo sikuizi. N.k
 
Badili heading yako
Dunia inatambua tz ni nchi maskini tofauti na ulivyoandika.
Nikija kwenye mada.
Tatizo kubwa ni kuongozwa na watu wasio na uwezo wa kuongoza kwani wenye uwezo hawapewi nafasi, sera za ujamaa yulushindwa lakini bado voingozi wanasema ni sera ya chama dola
Ufisadi na mikataba mibovu inayosainiwa na viongozi walioko madarakani
Kutokuheshimu sheria, miongozo na katiba ya nchi, Na kutokuwa na vipaumbele vyenye tija kwa taifa,yani bajeti yetu ni ya kugusa gusa afya kidogo elimu kidogo, ndege kidogo kilimo hamna kitu.
La muhimu kabisa ni kuwa hatuna sera shirikishi ya taifa ni hili ndiyo janga.
 
Aisee nimefungua huu udhi nikijua nakuta mafacts ya hatari kumbe ni vifacts vyepesi kabisa visivyo na uzito wowote
mkuu. utajiri hauletwi na vyeti original wala fake. tatizo ni mipango na ufatiliaji wa mipango ya maendeleo.
 
Kisu kimegonga mfupa.

Watu walikua wanapeleka CV zao zinapokelewa na watu wasio na sifa na ndio wanaotoa maamuzi. Matokeo barua zinawekwa kapuni wanaita ndugu zao wasio na sifa wanapewa ajira mezani.

Hata vyuoni unakuta kuna baadhi ya wahadhiri feki walikua wanaroho mbaya na kufelisha watu hovyo na kufaulisha mabinti machangudoa na kuacha wale wanaojituma na kusoma kwa juhudi kisa wanauwezo wa kujidhalilisha kingono.
Yote haya ni matokeo ya kuwa na watumishi feki.
 
Back
Top Bottom