Ngaliba Dume
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,710
- 3,675
Leo Rais amehutubia Wakuu Wilaya na Wakurugenzi wa Wilaya,Miji na Majiji ndani ya Ikulu Dsm.Kabla ya kula kiapo na kupata semina toka Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma,viongozi hao wateule walipata wasaa wa kuhutubiwa na Waziri Mkuu,Makamu wa Rais,Rais,Kamishna wa Tume ya Maadili na baadae kabisa Waziri wa TAMISEMI.
Rais amesisitiza kuwa ataendelea kuchaguwa watu ambao ni "watii" kwa chama na serikali,amesisistiza kuwa hawezi kuchaguwa watu katika uongozi wa utumishi wa umma kwa hawaamini juu ya Chama cha Mapinduzi na sera ya chama hicho,kwani Serikali iliyopo ni ya chama cha Mapinduzi na wananchi walichaguwa chama hivho kushika dola.Hivyo mtu anayetaka kufanya kazi na utawala huu ajuwe anafanya kazi ya kutekeleza sera ya chama tawala iliyokabishiwa serikali.Ufafanuzi huu wa Rais umekuja baada ya malalamiko kuwa nafasi za U-DAS na DED zimejazwa na makada wa CCM,hivyo Rais alikuwa anasisitiza kuwa ni lazima achaguwe makada sababu ndio wanaoamini juu ya sera na ilani ya CCM.
Akijibu hoja ya uzoefu na maswala ya "Strategic Succesion Plan",Rais JPM amesema mambo ya "kurithishana" uongozi katika utumishi wa umma katika kipindi chake hayapo.Kwamba umekaa ofisini unajuwa kabisa akitoka fulani unafuata wewe hiyo haipo.Hivyo ofisi nyingi zenye mpango mkakati wa "succesion"(?) wauweke kando kwani leo Rais ameahidi kusafisha muundo wote wa watu kuanzia ngazi ya chini mpaka juu,na sasa ameanza juu na anasema atashuka mpaka chini kwenye mizizi kuhakikisha anaweka watu hata kama hawana uzoefu ili mradi wawe wanaendana na kasi yake na kuamini juu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Hakika wale watumishi wa umma wasio na kadi wala muelekeo wa kikada,ambao pengine kutokana na mfumo wa kanuni na taratibu za utumishi wa umma walitegemea "Strategic Succesion Plan" ili kutoka hapo walipo kwenda hatua nyingine,basi wavute subra kidogo.
Naye Waziri Angela Kairuki kapigilia msumari kwa kuwaagiza Wakurugenzi kushirikiana na Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwabaini watu wasioendana na kasi ya Serikali hii na wale wasio na muelekeo wa kutekeleza ilani ya CCM kuwekwa pembeni.Waziri Kairuki anasema huu si wakati wa kuwa "Vuguvugu",ni ama unakuwa Moto au baridi.Watumishi wote wa umma ni lazima wajue wapo pale kufuata matakwa ya ilani ya CCM,kweli mtumishi wa umma hutakiwi kuwa na chama,lkn kwa sasa wanatakiwa wajuwe wanatekeleza ilani na mwatakwa ya CCM,hivyo wawe na mkao wa ki-CCM na kama hawawezi basi wapishe nafasi au wasubiri chama kingine wanachoamani kina sera nzuri waje kuzitekeleza.
Kauli hizi ni kama zinauwa misnigi ya Utumishi wa umma,mipango ya uzoefu,succesion pamoja na Impartiality zinaanza kupotea katika utumishi wa umma.Sasa ni dhahiri wale watu walio "neutral" na wasioeleweka upande wa kisiasa katika utumishi wataisoma namba.
Tunajuwa Rais wetu mpendwa JPM ana nia nzuri juu ya nchi yetu,lakini hili la utumishi wa umma,tunaomba alitazamae upya.Uzoefu katika utumishi wa umma ni zaidi ya elimu,kumtoa mtu moja kwa moja Lumumba na kumkabishi Halmashauri ina mashara yake,kama si leo basi hako mbeleni.Kuudharau mfumo wa "Succesion Plan" katika utumishi wa umma si afya,na si kweli kuwa watumishi wote ni mafisadi.Tusiikatishe tamaa kada ya utumishi wa umma kwa makosa ya watu wachache