Sasa ni miaka 60 baada ya Uhuru wa Bara letu. What kind of future do African politicians hold for their fellow countrymen in the next 60 years (2080)?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu Watanzania;

Mpaka kufikia sasa (2020) ni miaka 60 imepita baada ya uhuru wa bara letu hili pendwa la Afrika.

Now, what kind of future do African politicians and leaders hold for their fellow countrymen in the next 60 years (2080)?


Nimeamua kuuliza hivi kwa maana kwamba;

Mwaka wa 1960 ulijulikana kama Mwaka wa Afrika (The year of Africa) kwa sababu ya mfululizo wa matukio ambayo yalifanyika wakati wa mwaka huo- haswa uhuru wa mataifa kumi na saba ya Kiafrika - ambayo yalionyesha kuongezeka kwa hisia za ile dhana ya mapenzi mema kwa bara la Afrika (Pan-Africanism). Mwaka huo ulileta kilele cha harakati za uhuru wa Afrika na kuibuka kwa Afrika kama moja ya nguvu kuu katika Umoja wa Mataifa (UN).

images (49).jpg
Maendeleo haya ya haraka ya kisiasa yalisababisha uvumi na matumaini juu ya mustakabali wa Afrika kwa ujumla; lakini wakati huo huo, bara hili lilikuwa linaanza kukabiliana na hali halisi ya vurugu za baada ya ukoloni. Mwaka huu pia ulianza kushuhudia mwanzo wa upinzani wa kutumia silaha kwa serikali ya Ubaguzi wa rangi ya Afrika Kusini (South African apartheid government), na mabadiliko ya kisiasa kote Afrika na ulimwenguni kwa ujumla.

Mnamo mwezi Oktoba mwaka 1960, rais wa Ghana Mh. Kwame Nkrumah alihutubia mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa ambapo alijadili jukumu na nafasi ya bara la Afrika ulimwenguni na nafasi ya baadaye la ulimwengu barani Afrika. Nkrumah alisisitiza juu ya nguvu mpya ya Afrika, akisema kuwa Afrika haitaki wala haina nia ya kulipiza kisasi kwa wakoloni wake wa Ulaya, lakini pia akasisitiza yuu ya uhuru wa mataifa changa.

images (51).jpg

Hii ni sehemu ya speech ya mzee Nkurumah akiwa UN:

Ukweli mmoja mchungu kwa wakati huu ni athari kubwa juu ya muamko wa bara la Afrika katika ulimwengu wa kisasa. Wimbi linalojitokeza la utaifa mingoni mwa waafrika linafagia kila kitu kinachokuta mbele yake na linaleta changamoto kwa mamlaka na serikali za kikoloni kufanya marejesho ya haki kwa miaka kadhaa ya udhalimu na uhalifu uliofanywa dhidi ya bara letu. Lakini sisi waafrika hatutafuti kisasi.

Ni kinyume kabisa na asili yetu kuhifadhi chuki na visasi. Zaidi ya milioni mbili ya watu wetu wanalia kwa sauti moja ya nguvu kubwa. Hatuombei vifo kwa wanyanyasaji na watesi wetu; hatutangazi kutaka kuona hatma mbaya kwa watesi wetu waliotufanya watumwa; tunatoa madai mzuri ya kuhitaji haki; Afrika inataka uhuru wake. Afrika lazima iwe huru.

===========

Ni kipi ambacho wanasiasa na viongozi wa Afrika wanatarajia kuwapa wananchi wao ndani ya miaka mingine 60 mbele mpaka kufikia 2080?

(1) Mauaji mengine ya kimbari kama yale yalitokea nchini Rwanda mnamo mwezi April mwaka 1994 kwa sababu ya kuendekeza siasa za ukabila?

(2) Muendelezo wa vita za wenyewe kwa wenyewe pamoja na kuibuka kwa makundi ya kigaidi kama vile Boko Haram na Al-Shabab?

(3) Jumuiya za kikanda (EAC, SADC, ECOWAS) zinazoundwa na mataifa yanayokosa kauli ya pamoja katika kushughulikia changamoto za kimaendeleo pamoja na magonjwa (COVID-19)?

(4) Jumuiya ya umoja wa Afrika (AU) iliyodhaifu zaidi, inayokosa kauli thabiti na inayoshindwa kutatua changamoto za ndani ya bara? (mzozo wa maji ya mto Nile kati ya Misri na Ethiopia pamoja na dola zilizoanguka (Failed States) kama Libya na Somalia)

WHAT SHOULD AFRICANS EXPECT FROM THEIR LEADERS IN THE NEXT 60 YEARS?

NB: Hii mada inalenga katika kuangazia mustakabali mzima wa mendeleo katika bara la Afrika ndani ya miaka 60 ijayo mpaka mwaka 2080.

Ninaomba tuepuke kabisa matusi, mabishano na malumbano ya CCM, CHADEMA, ACT-WAZALENDO, NCCR, CUF.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Future ya Afrika Bado ni ngumu. Kuna dhana potofu kuwa Uhuru wa bendera tuliopata miaka 60 iliyopita kuwa labda ulitokana na Harakati za kina Nkhruma na Nyerere, ukweli ni kuwa Wakoloni waliaona ule Ukoloni Mkongwe haukuwa na faida kwao Kama ambavyo waliachana na Biashara ya Utumwa baada ya lndustrial Revolution.

Kinachoiponza Afrika ni pamoja na:-

Mosi; Ubeberu na Ukoloni mamboleo ambapo Mabeberu waliendelea kuzinyonya nchi zetu kwa njia ya mikopo na misaada ya masharti magumu, pamoja na kuhakikisha kwamba hakuna umoja wenye nguvu baina ya mataifa ya Afrika.

Pili; kukosa dira kwa mataifa ya Kiafrika. Baada ya kuondoa Ukoloni wengi wa Viongozi wa Afrika hawakuwa na road map na Visions ni kwa namna gani wataendesha nchi zao. Unaweza kuona hata hapa kwetu mtu akiuliza hivi kama Taifa tunaelekea wapi? Unaweza usipate jibu la moja kwa moja.

Tatu; Ulafi wa Watawala wa Kiafrika. Ambao walijigeuza Wakoloni wapya na kujali zaidi matumbo yao tofauti na maslahi mapana ya nchi zao. Watu wa kaliba ya Mobutu.

Nne; kutokuwa na taasisi imara, na Viongozi kujijengea himaya na mifumo ya kuhami mamlaka yao tu. Hata hapa kwetu mamlaka ya Rais ni makubwa sana.

Kwa hiyo kwa maoni yangu ni kwamba kwa miaka 60 ijayo Afrika itabaki kama ilivyo na hali inaweza kuwa mbaya zaidi tusipobadilika.
 
Future ya africa alikua nayo Gaddafi na mawazo yake yalikua makini ila wakamuita dicteta wakamuua. Sikuzote ukitaka kuwakomboa watu ki fikra lazma wajuba wa mambele wakuite dicteta.

Hakuna makaburi ya waoga ila kuna makaburi ya mashujaa .
 
Back
Top Bottom