Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,827
- 4,184
Uchaguzi wa mwaka 2010 umekuwa somo kubwa sana katika maisha yangu.
Baada ya kuishi miaka 30(umri wangu) katika maisha ya mazoea na kukata tamaa, sasa nina amini nchi hii kuna watu wanaoweza kuwaamsha Watanzania na kuleta mageuzi ya kisiasa na kiutawala yanayoweza kuleta uwiano wenye usawa kimaisha katika jamii.
Jamii nyingi za Watanzania hasa vijijini ni masikini, na wengi wanadhani kuwa Mungu aliwaumba kuwa masikini na hawajui kazi ya viongozi wa kisiasa.
Ki ufupi ni kwamba ninatangaza kupitia jamii forums kuwa Ninajiunga na Chadema Rasmi.
2005 nilikipigia kura nikiwa namtambua Mbowe(Freeman).
Zito kabwe nilianza kumsikia kwenye sakata la Amina Chifupa (marehemu) kupitia magazeti ya Udaku.
Nilishtuka pale nilipojua kuwa kumbe hata Professa Gwiji la Siasa za Kimataifa, Mwesiga Baregu naye pia ni mwanachama wa chama hiki makini.
Heshima kwa Mzee Mtei.
Heshima kwa Wibroa Slaa (PhD)
Heshima kwa mwana harakati Tundu Lisu
Heshima kwa Mpiganaji Rastafarai Chacha Zakayo Wangwe (Mungu Amlaze mahala pema)
Heshima kwa Damu ya Nyerere (Vincent Nyerere, Leticia).
Watanzania Wenzangu.
Hakuna haja ya kupigana. Hakuna haja ya kutamani kufa.
Ukombozi wa chi hii upo karibu.
Matokeo ya Mwaka 2010 nimeyavulia kofia.
Sasa Tuanze na Operation Nyangumi. Twende Vijijini. Tukawaamshe

Ninakuunga mkono, mimi nimeamua rasmi kujishughulisha na siasa tangu pale niliposoma quote hii maarufu ya gwiji Plato "The punishment which the wise suffer who refuse to take part in the government, is to live under the government of worse men."
Nilishajiunga na Chadema mapema kupitia sms lakini sikuwahi kujua ofisi zao zilipo, hivyo sikufika mbali. Ninaomba kama kuna kiongozi yeyote wa CHADEMA anayesoma thread hii, aitishe mkutano wa wapenzi na washabiki wa Chadema ili kuwasajiri rasmi kama wanachama na wanaharakati wa ukombozi wa kweli wa Tanzania. Harakati hizi zinatakiwa zianze mara moja, tunataka 2015 nchi hii iwe chini ya utawala mpya wa CHADEMA.