Fatima K.
Baada ya Ripoti ya Osoro, ile ya matrilioni mengi TRA ikatoa assessment ya USD 190 bln dhidi ya Acacia:
1. WaTZ wakaanza kuhesabu kila mtu anapata gari ya Noah;
2. Assessment ikajadiliwa kimataifa;
3.watangazaji wa CNN walikuwa wanacheka kama wehu.
Serikali:
1.ikasema inataka kuhakikisha makanikia yote yasafishwe TZ ili tusiibiwe
2.ikapitisha SHERIA 3 bungeni na marekibisho ya Mining Act inayotaka mikataba ya madini ijadiliwe na kupitishwa na Bunge ili kuwe na UWAZI.
WaTZ wakashangilia huu UWAZI mpy kwenye madini.
Leo tunaambiwa:
1. Makanikia huru kusafirishwa
2.Hakuna smelter iliyojengwa TZ
3.Assessment ya USD 190 bln BASI kw sababu Serikali imepata 16% za hisia za Twiga.
4.Mkataba umesianiwa bila ya kujadiliwa au kuudhinishiwa na Bung wala hatujui details
Maswali yangu:
1. Kama Kamati za Mruma na Osoro walikuwa wa kweli, USD 190 bln ziko wapi?
2.Assessment ya TRA ya USD 190bln inafutwa vipi kisheria kama ni ya KWELI?
3.Kwanini Ripoti za Mruma na Osoro hazijawekwa wazi?
4.Tumepata barabara. Smelter iko wapi?
Mwisho:
Kuna WaTZ 3 waliyekuwa wanafanya kazi Acacia. Wako ndani kwa MONEY LAUNDERING tangu October 2018 na Biswalo anasema:UPELELEZI HAUJAKAMILIKA.
1. Hawa WaTZ 3 ni Collateral Damage
2.Ndio wameshasahauliwa sasa Mkataba umeshasainiwa?
Technocrats wameacha SIASA ifukie UKWELI
Sent using
Jamii Forums mobile app