Sasa Lowassa hakamatiki: Waraka kwa Jakaya Kikwete!

JK: Jibu ni ndiyo. Ni kweli tu kwa sababu, kwanza kwa maana tu ya uzoefu wangu katika utumishi wa umma, katika serikali. Lakini miaka 10 hii ambayo nimekuwa katika Wizara ya Mambo ya Nje, imenipa fursa kubwa na pana zaidi ya kuifahamu dunia na pia kufahamu hasa jinsi nchi zinavyoendeshwa.Nimepata uzoefu mkubwa wa kujifunza nchi zinazoendeshwa vizuri, na kwa nini wamefanikiwa. Nchi zinazoendeshwa vibaya, ni kwa nini wameshindwa.
Ikiwa leo JK hajui kwa nini Tanzania ni maskini, sasa ule uzoefu umetupeleka wapi?
 
Kweli mtandao umemsaidia sana hasa kwa mambo makuu mawili. Mosi kufanikisha wizi wa pesa za epa bot, pili kumumwakyembe JK original kwani angekuwa hai asingekubali wezi wapewa nchi

kama huma hoja ni bora ukakaa kimya,hv una fahamu pesa za epa zilikwapuliwa lini?
 
Kweli mtandao umemsaidia sana hasa kwa mambo makuu mawili. Mosi kufanikisha wizi wa pesa za epa bot, pili kumumwakyembe JK original kwani angekuwa hai asingekubali wezi wapewa nchi

kama huna hoja ni bora ukakaa kimya,hv una fahamu pesa za epa zilikwapuliwa lini?
 
Lowasa ni rais wa 2015, namsubiri kwa hamu, kura yangu anayo....na ya mke wangu, na ya housegirl, na ya dada zangu na ndugu zangu na wafanyakazi wenzangu wote wa karibu. period...tukitaka nchi(inji) hii iendelee tunahitaji watu wenye kufanya maamuzi mazito yenye manufaa kwa taifa, hatutaki watu walegevu.
 
Lowassa for President...jamaa mchapa kazi sana huyu na Richmond hakuiba yeye,kama aliiba mbona hamumpeleki mahakamani kumshtaki?
 
Mimi nimeshajiandaa kisaikolojia kwa ujio wa Rais mpya, sioni cockroch yeyote ndani ya CCM wa kuweza kumzuia mwanaume huyu wa Shoka, na kwa jinsi nijuavyo JK ni lazima ajisalimishe mapema kwa Lowasa ili visenti vyake vya uzeeni aweze kuvitumbuwa kwa amani.

Lowasa ni stering wa Kihindi, huwa anaanza kwa kupigwa na kuteswa lakini mwisho wa Sinema mtabaki vinywa wazi. na kwa wale wanaoamini kwenye maombi yule Nabii ambaye yupo duniani TB Joshuwa yeye tayari ameshamhakikishia Lowasa asubili kuapishwa tu.

****...
 
Lowasa ni rais wa 2015, namsubiri kwa hamu, kura yangu anayo....na ya mke wangu, na ya housegirl, na ya dada zangu na ndugu zangu na wafanyakazi wenzangu wote wa karibu. period...tukitaka nchi(inji) hii iendelee tunahitaji watu wenye kufanya maamuzi mazito yenye manufaa kwa taifa, hatutaki watu walegevu.

Hauwezi kua na hg wewe,wala hauwezi kua mfanyakazi kwa iq yako hiyo!
 
Wazazi huo uchaguzi sio december 2012 ni 2015 bado bajeti nne kamili, mzee zima EDO katoka mkuku mapema sana nafikiri atajikwaa avungike shingo Lowasa! Lowasa! Lowasa! Lowasa! ngoma imevuma sana kaka haichelei kupasua;ila mungu amuweke hai maana atoa mpunga si kitoto watu makanisani KKKT washajinoma sana ,kwa kadinali Pengo ndo wanagoja kesho kutwa Ifakara mapadre washanawa, Mashehe round yao iko mbioni.Hakuna mtanzania aliyewahii kuutolea mcho uraisi kama huyu kuanzania 1995 mtu mzima anaumendea kipaka shume;akiingia ikulu anaweza akaanguka akafa kwa kihoro, taama ilimuua fisi chunga sana mzazi misifa ya wapambe hao watakuua wale ubeche wa mwisho,Mi nduguyo nakuonea imani sijui unalala vipi mzazi maana kusema za kweli kila kona gumzo ni wewe mzazi hata afya yako haiko mukide
 
Lowasa ni rais wa 2015, namsubiri kwa hamu, kura yangu anayo....na ya mke wangu, na ya housegirl, na ya dada zangu na ndugu zangu na wafanyakazi wenzangu wote wa karibu. period...tukitaka nchi(inji) hii iendelee tunahitaji watu wenye kufanya maamuzi mazito yenye manufaa kwa taifa, hatutaki watu walegevu.

wewe lazima utakuwa dikteta dizaini ya baba ubaya
 
Waandishi muoneeni imani EDO mtaamuua walahi tukose lakusema ukimuona mzee ameshaanza kunyong'onyea nyie mnaonge ya 2015 wakati december hii parefu msijesema optimus mwanga
 
amini nawaammbieni kikwete ndio wa mwisho ccm kimsingi ilo lichama limesha kufa tunasubiri kuzika 2015

"slaa 4 presidency 2015"
 
Najiuliza maswali ya kijinga......
1) U-rais ni nini hasa?
2) Je kwa nini Lowassa (au kambi yake) wanaona kuwa ni lazima yeye na yeye pekee ndiye (lazima) awe rais wa Tz 2015?
3) Kwa nini hawazioni nyufa lukuki ktk hoja zao nyepesi na mantiki zao tata juu ya mtu wao huyo?
4) Je Lowassa ana ushawishi gani kiuwezo na maadili hata kujaribu kufikiria nafasi ya Urais?
5) Ikiwa yeye anataka Urais kwa mbinde namna hiyo na wananchi hawamtaki......atatumia nini kutimiza azma yake hiyo?

In short what can he offer which ccm and Kikwete could not offer?

Lipumba ukimuuliza kwa nini kila siku unagombea Urais wewe na kwa nini usiwaachie wengine, kana kwamba vile neno mgombea Urais ini sehemu ya ubini wa jina lako!!?? jibu atakalokupa ni hili hapa;
Mimi ni muumini wa Falsafa ya Abdoulaye Wade Rais wa Senegal ambaye amegombea urais mara nne tangu 1978 mpaka mwaka 2000 alipoupata Urais.

Lakini ni Wade huyo huyo leo hii amebadilisha katiba ili abaki madarakani licha kwamba umri wake ni miaka 85, huyu ni babu wa kutulia na wajukuu, sasa hapa wa kuulizwa swali ni Lipumba je bado anaishi katika Falsafa za Wade?
 
Heshima kwanu wanajamvi.

Mheshimiwa Lowassa alishawekwa pembeni siku nyingi muanzisha mada anataka kutuaminisha bado mtu wake ana nguvu kubwa lakini ukweli utabaki ukweli.Lowassa aliondoka serekalini kwa aibu Kikwete angeweza kumrejesha ndani ya safu za uongozi wa chama eg nafasi ya katibu mkuu,Makamu wa mwenyekiti hii ingemsaidia zaidi kujijenga ndani ya chama

Ukitazama mchakato wa uchaguzi ndani ya CCM uliompitisha Kikwete mwaka 2005 na michakato ya uchaguzi ujao wa mwaka 2015 utabaini wazi nafasi ya Lowassa imezidi kuwa ndogo kadri siku zinavyosonga mbele.

Lowassa ataingia kwenye mpambano bila nafasi nzito serekalini na ndani ya chama.Ikumbukwe utaratibu mpya wa chama nafasi za uNEC zitagombewa wilayani kwakuwa Lowassa tayari ni mbunge itabidi abakie na nafasi yake ya ubunge hataruhusiwa kugombea nafasi ya nec labda kwa kibali maalumu cha CC ya CCM taifa kitu ambacho sikioni kikitokea.

Lowassa ataingia kwenye mpambano akiwa na kashfa nzito ya Richmond iliyomlazimisha kuachia nafasi ya uwaziri mkuu kwa aibu na fedhea kubwa.Hili ni doa kubwa sana ambalo ameshindwa kulisafisha mbela ya umma wa waTanzania na jumuiya ya kimataifa.

Lowassa amedhibitiwa mkoani Arusha,Uteuzi wa Mkuu wa mkoa mpya wa Arusha Bwana Magesa Mulongo na Katibu wa CCM mkoa wa Arusha Bi Mary Chatanda ni kigingi kingine ambacho Lowassa atapaswa kukishinda ingawa tayari wameshalidhibiti kundi la Ngoyai kuanzia Mwenyekiti wa UVCCM Arusha na wajumbe wa Halmashauri ya mkoa wa Arusha.Lowassa ameachwa atambe wilaya ya Monduli pekee yake.Uteuzi wa mgombea ubunge Arumeru Mashariki Bwana Summari umekataliwa kwa nguvu kubwa na wajumbe wa Halmashauri ya Mkoa wa Arusha wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa na Katibu wa Mkoa.Sababu kubwa ya pingamizi la mkoa ni ukaribu alionao Bwana Summari na Mheshimiwa Lowassa [Mkwe].

Sakata la Dr Mwakyembe litaendelea kumtesa Lowassa na pengine yaweza kuwa msumari wa mwisho katika jeneza lake la kisiasa.Dr Mwakyembe ana turufu kubwa Laigwani anajua hilo wafuasi wake wanajua katia mikakati yao hawakutarajia kukumbana na changamoto hizi walitarajia Dr angejifia kama alivyojifia Salome Mbatia.

Mwisho msisahau wajumbe wa NEC watakao chagua wagombea wa CCM si hawa wa sasa watachaguliwa wapya kutoka wilayani hakika katika mfumo mpya wa chama waliojiwekea hawa hawatakuwa na nafasi za uwaziri wala ubunge watakuwa ni wajumbe wa NEC watakaokuwa wanafanyakazi za kudumu wilayani tofauti na sasa utamkuta mtu mmoja ni mjumbe wa NEC ni waziri na ni mbunge.Ukitaka kusema Lowassa ana nguvu wakati bado wajumbe wa NEC na mkutano mkuu hawajachaguliwa lazima tukuite mwehu.

Tanzania ni mali ya waTanzania lini Tanzania ilibinafsishwa kwa mafisadi.

Karata pekee iliyobaki kwa Lowassa ni kukimbilia makanisani.
 
amini nawaammbieni kikwete ndio wa mwisho ccm kimsingi ilo lichama limesha kufa tunasubiri kuzika 2015

"slaa 4 presidency 2015"
Achana na Habari za Dr Slaa kwenye thread hii kuchaguliwa ni kitu kingine na kutangazwa mshindi ni kitu kingine tofauti, Dr Slaa tulimchaguwa kuwa Rais wetu lakini hakuapishwa kuwa Rais wala hakutangazwa kuwa mshindi, sasa huyu Lowasa vile vyombo vinavyopinduaga maamuzi ya wananchi vyote viko chini yake hasa Usalama wa Taifa ni nani wa kumzuia huyu!!??
Mnachopaswa kukizingatia kabla hamjatokwa na mapovu ni kwamba currently tuna ceremonial President tu, lakini Lowasa ndie mwenye CCM, nadhani mtakumbuka vizuri Samuel Sitta alivyoshikishwa adabu kwenye uspika.
 
Mwisho msisahau wajumbe wa NEC watakao chagua wagombea wa CCM si hawa wa sasa watachaguliwa wapya kutoka wilayani hakika katika mfumo mpya wa chama waliojiwekea hawa hawatakuwa na nafasi za uwaziri wala ubunge watakuwa ni wajumbe wa NEC watakaokuwa wanafanyakazi za kudumu wilayani tofauti na sasa utamkuta mtu mmoja ni mjumbe wa NEC ni waziri na ni mbunge.Ukitaka kusema Lowassa ana nguvu wakati bado wajumbe wa NEC na mkutano mkuu hawajachaguliwa lazima tukuite mwehu.

Tanzania ni mali ya waTanzania lini Tanzania ilibinafsishwa kwa mafisadi.

Karata pekee iliyobaki kwa Lowassa ni kukimbilia makanisani.
1.JPG

Sasa mkuu ngongo naona unajichanganya mwenyewe kwa maelezo marefu yasiokuwa na tija, sasa kama unasema Sioi Sumari ni mtandao wa Lowasa, je alieshinda kwa kura za wana CCM hapo Arumeru ni nani!!?? bado una underestimate nguvu za Lowasa CCM? Pole sana huwajui vizuri wana CMM.
 
Back
Top Bottom