Sasa Lowassa hakamatiki: Waraka kwa Jakaya Kikwete!

Ni analysis nzuri yakuonyesha namna ambavyo CCM imeoza...lakini naona unafanya jitihada za dhati kumpigia promo white hair...mimi nadhani tuache kuwafanya watanzania ni wajinga,kwa maovu aliyoyafanya white hair watanzania hatuwezi kumsamehe..anaweza akawa mchapa kazi kwelikweli nakubali,lakini doa la kutuibia mali zetu sisi wanyonge ni kama damu iliyomwagikia kwenye shati nyeupe..hata kwa omo haitakasiki..white hair hatumtaki tafadhali!!
 
Lowasa ni stering wa Kihindi, huwa anaanza kwa kupigwa na kuteswa lakini mwisho wa Sinema mtabaki vinywa wazi. na kwa wale wanaoamini kwenye maombi yule Nabii ambaye yupo duniani TB Joshuwa yeye tayari ameshamhakikishia Lowasa asubili kuapishwa tu.

nashukuru sana kwa kulitambua hili
 
edward ngoyay lowassa!!!alishakamatika siku nyingi!!!muulize samwel 6 alimkuta angle gani!!!mbona hata alipokutwa ghadafi pana uafadhali!!!!!!amini hilo!!!!

ongea kama unaongea sio utuletee mambo ya redio mbao . Usiwe kama huyo mnafiki 6.
 
Ni analysis nzuri yakuonyesha namna ambavyo CCM imeoza...lakini naona unafanya jitihada za dhati kumpigia promo white hair...mimi nadhani tuache kuwafanya watanzania ni wajinga,kwa maovu aliyoyafanya white hair watanzania hatuwezi kumsamehe..anaweza akawa mchapa kazi kwelikweli nakubali,lakini doa la kutuibia mali zetu sisi wanyonge ni kama damu iliyomwagikia kwenye shati nyeupe..hata kwa omo haitakasiki..white hair hatumtaki tafadhali!!
Wenzako kila siku wakiulizwa walete ushahidi wa tuhuma za huyu bwana ndio huwa wanakimbia kimoja na hawarudi tena kwenye thread. Mbaya wa Watanzania si Lowasa kamwe bali ni:

1. Harisson Mwakyembe Huyu na kamati yake walitumia mamilioni ya pesa za walipa kodi kwa kazi ya kuutafuta ukweli matokeo yake wakaja na ukweli nusu, je ule ukweli nusu mwingine walikuwa wanamficha nani na kwa faida ya nani?
2. Samuel Sitta Huyu ni mzee wa hovyo sana na tena anazeeka vibaya mno, hatuwezi kumsamehe kwa kuumaliza mjadala wa Richmond kihuni namna ile, kwangu mimi hawa watu wawili ndio maadui wetu wakuu kwenye hili!!
 
Huyu Jamaa Lowasa inaonekana amejipanga vilivyo, maana waandishi wote wenye njaa kali ambao walitumika kama vuvuzela la JK sasa wameingia kazini rasmi kuhakikisha hakuna anaeleta kiwingu cha kumzuia Lowasa.
Jionee mwenyewe!!


Waraka kwa Rais Jakaya Kikwete (3)



*Tujikumbushe alivyotoboa siri ya mtandao 2005

Makosa yetu mengine hutokana na woga; woga unaotuzuia kumlaumu mkubwa japo tunajua kuwa kakosa, au kumtetea mdogo anayelaumiwa na wakubwa japo tunajua kuwa hana makosa. Na msingi wa woga ni unafsi. Pengine huwa tunaogopa sisi wenyewe kulaumiwa au kupata hasara fulani. Pengine twaweza kuwa hatuna cheo chochote ambacho tunaogopa kupoteza; pengine huwa hatuna wala tamaa yoyote ya kupata cheo fulani. Lakini woga unaweza kutokana na tamaa ya kila binadamu kupendwa na binadamu wenzake. Sisi wote tunayo tamaa hii, au sivyo tusingekuwa binadamu. Woga huu huweza ukamfanya mtu kuvumilia maovu, hasa kama maovu yale yanatendwa na walio wengi kwa walio wachache, au yanatendwa na wakubwa kwa wadogo. Kwa kuogopa kuwaudhi wengi tunawaacha watende makosa bila kuwasahihisha, wasije wakatuchukia. Huu ni unafsi mbaya sana.

Tujisahihishe
Julius K. Nyerere
Mei, 1962

Nimeanza na nukuu hii ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili kuwajibu wasomaji kadhaa ambao wamediriki kusema nina chuki binafsi dhidi ya Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete. Hao hawanijui. Wapo wanaosema tayari kazi ya 2015 imeanza! Sijui ni nani mwenye mawazo finyu anayeweza kupambana na mtu anayeng’atuka! Anapambana ili iweje? Haya ninayoyaandika, yanatokana na msukumo wa kuwasaidia viongozi wetu, akiwamo Mheshimiwa Kikwete.
Isitoshe, Oktoba, 2005 Mheshimiwa Kikwete mwenyewe akiwa mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), alifanya mahojiano maalumu na aliyekuwa Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Tido Mhando. Katika mahojiano hayo yaliyofanyika London, Uingereza, Mheshimiwa Kikwete alieleza bayana msimamo wake wa kutumia vyanzo mbalimbali kupata kile kilichokuwa kikiendelea mitaani. Alisema:
“…Kuwa rahisi kuyasikia ya watu, hili ndilo jambo kubwa katika uongozi, ili uweze kuwa unayasikia mambo mbalimbali ya watu badala ya kuwa na njia moja ya kusikia wanavyosema wananchi wako. Kwa hiyo, lazima utengeneze namna ya kukutana na watu wengi…unajua tatizo la kusikia mambo ya huku duniani kupitia njia moja, wakati mwingine wanaweza kuwa wanakuletea yale tu ya kukufurahisha…oh, unajua mzee mambo huku ni mazuri, huko mitaani huko kila mtoto anayezaliwa anapewa jina la Jakaya…eh, Jumamosi hii mzee, watoto wote wa kiume waliozaliwa Muhimbili wanaitwa Jakaya…unaendelea hivyo mpaka mambo yanaharibika. Ni lazima pia uwe na namna zako nyingine za kupata habari zako. Nina watu wengi nawafahamu mitaani, kuna mabaraza ya wazee na kadhalika.”
Haya ni maneno yake Mheshimiwa Kikwete mwenyewe aliyoyazungumza Oktoba, 2005. Wengine tuliyazingatia haya na ndiyo maana tumejipachika dhima ya kumweleza kinachoendelea mitaani. Naamini yeye mwenyewe hawezi kushangaa kuona nimeamua kuitumia njia hii ya waraka kumfikishia yale yanayosemwa mitaani. Kama alivyosema mwenyewe, kutegemea njia moja kufikishiwa mambo muhimu, kuna walakini. Wapo wanaolalamika kwamba huenda Usalama wa Taifa hawampi haya, au kama wanampa, basi amekuwa mbishi na mpuziaji. Hata pale alipoamua kuwatumia wazee, amekuwa “akiwahutubia”, huku tukiambiwa kwamba “anazungumza na wazee!”. Wazee anaochangua kuzungumza nao ni mabubu? Mazungumzo gani yasiyoruhusu hoja kutoka upande wa pili?
Nirejee kidogo kwenye mada. Yeyote aliyemsikia Rais Kikwete wakati akihutubia wafuasi wa CCM wana wananchi wakati wa Maadhimisho ya Miaka 35 ya Kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza, atakubali kuwa maneno anayozungumza Nape Nnauye, huwa ni yake. Ni kawaida ya Rais Kikwete kujaribu kukwepa lawama kila inapowezekana. Amekuwa wakiwatumia kina Nape kufikisha ujumbe, lakini amekuwa mwepesi wa kusema si yeye aliyewatuma. Inaiwia vigumu kuamini kuwa mwajiriwa anaweza kuwa jeuri mbele ya mwajiri. Nape ni mwajiriwa. Haiwezekani akawa anatoa kauli zisizomfurahisha mwajiri wake-Rais Kikwete-halafu akaachwa hivi hivi. Akili ya kawaida inakubali kuwa Rais amekuwa akimtuma Nape kuyasema anayosema, ingawa inawezekana si yote.
Kama hivyuo ndivyo, ebu tujikumbushe hili la kuwazuia wanaotaka urais wasijitokeze sasa. Huko nyuma nimepata kusema kwamba kitendo cha kuwazuia wana CCM na Watanzania wenye sifa zinazostahili kujitokeza sasa kutangaza nia, au kuanza maandalizi, ni kuwaonea. Haiwezekani jambo hilo likawa limehalalishwa kwa Mheshimiwa Kikwete tangu mwaka 1995, lakini sasa likawa haramu kwa wengine.
Kuna faida nyingi kwa mtu anayeutaka urais kujitokeza mapema. Ukiacha faida wanayopata wananchi ya kumtambua, ipo faida nyingine kubwa na muhimu kwake. Nayo ni ya kuupata urais. Kuwekeana vizingiti hakuna maana.
Katika kuthibitisha hilo, ebu turejee tena kwenye maneno ya Mheshimiwa Kikwete aliyoyazungumza alipohojiwa na Tido Mhando na yakarushwa kupitia BBC mnamo Oktoba, 2005.


TIDO: Wakati wa uteuzi wa chama, Rais Mkapa alitoa hotuba ambayo wengi walidhani alikuwa anakupigia debe wewe. Je, hili lilikushangaza hata wewe binafsi?


JK: Yaani wewe kweli mimi nitashinda kwa hotuba ya jukwaani pale. Ndugu yangu, nilishinda kwa jitihada kubwa ambazo niliziweka mimi na marafiki zangu. Ukweli ni kwamba ilituchukua muda kujijenga. Tulitengeneza mtandao wa watu nchi nzima wa watu wanaotuunga mkono. Tulifanya juhudi kubwa ya kuzungumza na wana-CCM.


TIDO: Lakini wakati kiongozi mkubwa kabisa, anapokuja mbele ya wajumbe na kutoa matamshi ambayo yanaonyesha dhahiri yanaelekeza kwamba yeye anamuunga mkono fulani, na ilijihidhirisha hata katika mkutano ule pale watu walipoanza heka heka za Kikwete…Kikwete moja kwa moja.


JK: Mimi sijui ni kupigiwa debe kwa vipi hasa. Hotuba ya Rais, yeye alichokuwa akizungumza tu ni kwamba... Mimi nadhani hotuba yake ilikuwa inasisitiza kwamba; kwanza alichokisema kwamba moja; CCM kama CCM, tuchague watu, lakini tusisahau huyu tunayemchagua sasa, hatimaye tutampeleka kwa watu.Na huko kwa watu, ni lazima sisi kama chama, kama tunataka kushinda, ni lazima tutambue matarajio ya watu. Kwa sababu haiwezekani muwe mmekaa tu pale kwenye mkutano, mkajifanya kama vile mmefunga masikio, yaani mmeziba masikio, na macho mmeyaziba, hamuoni na wala hamsikii huko mnakotoka wanasema nini.Lakini pia, hata wale wanakuja kwenye Mkutano Mkuu wanatoka katika kila wilaya ya nchi yetu. Ni vizuri kwao wakaangalia matumaini ya watu, na muangalie matumaini ya wale mnaowategemea watakwenda kupiga kura. Sasa, sina hakika kama kwa kusema hivyo alikuwa na maana yangu mimi!


TIDO: Kulikuwa na vitu vingi pale. Oh, mchague mtu ambaye amekulia kwenye chama hiki, anayekifahamu vizuri sana. Ukiangalia kwa undani, ukilinganisha na wagombea wenzako uliokuwa nao pale, sifa zote hizo zilikuwa zimeiva kwako.


JK: Lakini, niseme. Hivi, hivi ni mwana-CCM gani, atateua mtu ambaye hana historia na hicho chama. Hata kama utataka kunilaumu kwa hilo, bado nitaendelea kusema si kweli.


TIDO: Hapana si kwamba tunakulaumu, lakini tunasema alionyesha wazi kwamba chama kimchague Kikwete.


JK: Mimi sijui Bwana, sijui. Mimi ningependa kuamini kwamba nilifanya jitihada kubwa kushinda, na wasije wakafika mahali wakarahisisha mitihani niliyoipitia. Nilifanya jitihada kubwa sana. Sisi ni katika wale tunaoamini kwamba mwisho wa uchaguzi mmoja, ni mwanzo wa uchaguzi mwingine. Sisi tulianza mwaka 1995, tukaweka mkakati wa mwaka 2005.Nilifanya kazi kubwa kujenga mtandao. Nilifika mahali, kila mahali ukinitajia Ngara yuko nani, nakwambia yuko fulani. Nikawa nawajua watu kwa majina. Nimefanya kazi kubwa sana. Ndiyo, nakiri kwamba uzoefu wangu nao katika chama ulinirahisishia. Kwamba hawa watu ninawafahamu, nimeshaishi nao, ndiyo msingi ambao mimi ninadhani umesaidia.
Lakini wanaodhani nilishinda kwa hotuba ya Rais wanatafuta kurahisisha tu ili ionekane kwamba kama isingekuwa hotuba ile watu wasingenichagua. Hata kidogo! Mimi nilianza zamani. Ninaamini tu kwamba nilifanya jitihada mimi mwenyewe ya kuwaomba wana-CCM waniunge mkono, na ninashukuru walinikubali baada ya kuwaeleza nia yangu ni nini.


TIDO: Eh, uliwaomba wakupe kijiti ili nawe uweze kuliongoza taifa la Tanzania, na wao wamekupa, unafikiri sasa hivi uko imara zaidi kuliko miaka 10 iliyopita?


JK: Jibu ni ndiyo. Ni kweli tu kwa sababu, kwanza kwa maana tu ya uzoefu wangu katika utumishi wa umma, katika serikali. Lakini miaka 10 hii ambayo nimekuwa katika Wizara ya Mambo ya Nje, imenipa fursa kubwa na pana zaidi ya kuifahamu dunia na pia kufahamu hasa jinsi nchi zinavyoendeshwa.Nimepata uzoefu mkubwa wa kujifunza nchi zinazoendeshwa vizuri, na kwa nini wamefanikiwa. Nchi zinazoendeshwa vibaya, ni kwa nini wameshindwa.


TIDO: Kwa hiyo, unaweza ukasema labda unashukuru kwamba miaka 10 iliyopita ulikosa, na umepata mwaka huu sasa?


JK: Nilisema hivyo mkutanoni pale. Nilisema Mwenyezi Mungu, maana sisi Waswahili, ukishindwa unasema kila jambo ni kwa kheri ya Mwenyezi Mungu, eh kwamba pengine Mungu hakutaka, na alipokataa wakati ule alijua kwamba kuna ka-kipande haka ka-uzoefu ambako nilikuwa sijakapata, nami nikajitahidi kukapata. Nami nasema kwamba sasa nikifanikiwa kuchaguliwa nitakuwa Rais mzuri zaidi.


TIDO: Wengine wanasema hata hayati Mwalimu alikueleza hivyo siku ile hasa baada ya kushindwa, akisema nafasi yako inakuja, subiri. Je, hii ni kweli?


JK: Hayo yaacheni, tuzungumze mambo ya sasa.


Mwisho wa kunukuu
Je, kwa maelezo haya ya Mheshimiwa Kikwete, ya kujiandaa kwa miaka 10 kuupata urais, yanampa ujasiri gani wa kuwazuia wengine kwa miaka hii mitatu iliyosalia nao kujiandaa kuipata nafasi hiyo? Je, kama kwake ilikuwa halali kujiandaa kwa muda wote huo, tena kwa kuwa na mtandao imara, kwanini wengine nao ‘wasimuenzi; kwa njia hiyo? Tutafakari. Itaendelea.


Manyerere J. N
0759 488 955
manyerere@hotmail.com

Jackton Manyerere kumbe ndie alieandika mi nilidhani mwandishi gani sijui makini,manyerere mbona kawekwa kiganjani na lowassa yeye pamoja na balile lowassa anawamilik,anaweza kuwafanya lolote atakalo na hii atakua kaiandika lowassa kampa manyerere aipachike kwenye magazet yao mafisadi.

Anasema jk anamzuia lowassa kivipi?au anataka kusema jk ambebe lowassa labda kwa kuwa yeye alibebwa na mkapa.Lakini uchaguzi si bado?ukifika wakati wa kuchukua fomu lowassa atakataliwa fomu???au manyerere anataka kutumabia nini ?

N a kitu kingine manyerere aache kulitumia jina la mwalimu nyerere kujinufaisha,kwanza yeye sio mtoto wa nyerere kama anvyotaka watu waamini,familia yote ya nyerere haimuungi mkono lowassa huyu mtu wa mbali na familia iweje atumie jina la nyerere kumbeba lowassa??ameahidiwa nini na lowassa,ukrugenzi wa habari na mwasiliano ikulu au?
 
Siasa za CCM zimejaa fitna unaoambatana na uhuni, EL anazijua fitna hizo kuliko ilivyo kwa JK.

Maelezo ya JK yana kila chembe yenye kuonyesha nguvu ya watu wengine (sio yake) ndiyo ilimpa ticket ya CCM, ndio maana kaendelea kutawala kwa hofu na woga.

Tatizo kubwa ni kwamba EL naye anapita njia hiyo hiyo jambo ambalo linamwondolea sifa ya kuwa rais BORA. Tanzania inahitaji rais anayekubalika kwa hoja na misimamo yake, sio kuwa na mtandao from Ikwiriri to Ngara!........ Ni nani atacheza nafasi ya 'Daudi' (iwe CCM au CDM) kumwangusha 'Goliati'?????
 
Wenzako kila siku wakiulizwa walete ushahidi wa tuhuma za huyu bwana ndio huwa wanakimbia kimoja na hawarudi tena kwenye thread. Mbaya wa Watanzania si Lowasa kamwe bali ni:

1. Harisson Mwakyembe Huyu na kamati yake walitumia mamilioni ya pesa za walipa kodi kwa kazi ya kuutafuta ukweli matokeo yake wakaja na ukweli nusu, je ule ukweli nusu mwingine walikuwa wanamficha nani na kwa faida ya nani?
2. Samuel Sitta Huyu ni mzee wa hovyo sana na tena anazeeka vibaya mno, hatuwezi kumsamehe kwa kuumaliza mjadala wa Richmond kihuni namna ile, kwangu mimi hawa watu wawili ndio maadui wetu wakuu kwenye hili!!

ushahidi ni kura chache ilizopata ccm kutoka na kashfa iligharimu uwaziri mkuu wa lowassa.Pia huyu alishiriki katika kasfa ya ununuzi wa magari ya wabunge,ushahidi zaidi ni mahakamani chamani hatuna hayo mambo yenu ya ushahidi,chama kinatumia zaidi taarifa za kiintelijensia,toka enzi hizo za kina kambona chama kikitaka kumshughulikia kiongozi muovu hakitafuti ushahidi wa mahakamani kina njia zake na lowassa anazijua,nyie endeleeni kulilia ushahidi,lakini nec ile mliokuwa mkidai mzee ana nguvu imeshaamua juzi mwambie mzee achague ubunge ama u nec...nasikia anataka kujiunga na kina Hamad Rashid na cuf yao mpya,tunamtakia kila la kheri atupunguzie mzigo wa matatizo yake!
 
vipi kuhusu maamuzi ya nec ya juzi yanayompa mwenyekiti mamlaka ya kukudhibiti chama kuelekea uchaguzi wa ccm na baadae jina la mgombea urais?
Unapoteza muda wako bure, CCM yote iko chini ya mikono ya Lowasa akiwemo JK. WEWE JIDANGANYE NA MAIGIZO YA KINA NAPE.
 
EL nimekusoma.... wee jipangee kisawasawa, atakayekuja kichwa kichwa kukuzuia pigaaaa....
 
he he he he he he aisee da kweli ndo maana Tido Muhando alifukuzwa TBC maswali ya kumchoma mtu hayo aisee du...he he he
 
kweli kazi ipo na hii ndiyo maana ya siasa... kila lakheri wagombea watarajiwa wa uraisi 2015.. fuateni nyayo za Baba Mwanaasha... "...Sisi ni katika wale tunaoamini kwamba mwisho wa uchaguzi mmoja, ni mwanzo wa uchaguzi mwingine." acheni kuzubaa
 
William alisema yuko tayari kuingia msituni kuliko kuona EL anaingia magogoni, sijui atakuwa amebadii mawazo?
 
Iwapo Edward Lowassa atakuwa rais hii itaonyesha jambo kuu moja, kwamba watanzania si watu wa kuhurumiwa. Ukipata chance tu iba, iba na endelea kuiba na watakuzawadia urais kama shukrani ya kuwaibia na kuwagawia umaskini.

Edward Lowassa hatakuwa rais, na bado hiyo haitoshi kuwa ushindi dhidi ya ufisadi. Kuushinda ufisadi si kumtosa Lowassa ili kumweka Membe, au Sitta, au Migiro, au Magufuli au Pinda au Bilali au....nilisikia eti na Emmanuel Nchimbi nae yumo. Kuchunguza chunguza ndani ya genge lililowakumbatia mafisadi kumtafuta mtu msafi ni sawa na kumtafuta aliye hai katika makaburi.
 
Najiuliza maswali ya kijinga......
1) U-rais ni nini hasa?
2) Je kwa nini Lowassa (au kambi yake) wanaona kuwa ni lazima yeye na yeye pekee ndiye (lazima) awe rais wa Tz 2015?
3) Kwa nini hawazioni nyufa lukuki ktk hoja zao nyepesi na mantiki zao tata juu ya mtu wao huyo?
4) Je Lowassa ana ushawishi gani kiuwezo na maadili hata kujaribu kufikiria nafasi ya Urais?
5) Ikiwa yeye anataka Urais kwa mbinde namna hiyo na wananchi hawamtaki......atatumia nini kutimiza azma yake hiyo?

In short what can he offer which ccm and Kikwete could not offer?
 
Back
Top Bottom