Sasa kutuonyesha tupu zenu ndio nini!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa kutuonyesha tupu zenu ndio nini!?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Nov 14, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Tafiti nyingi zinaonesha kwamba, mwanamke ambaye anavaa kwa njia yenye kuchokoza hisia, hawezi kutazamwa kama aliye na uwezo sawa na wengine mahali. Hii iko duniani kote, bila kujali kama ina ukweli au haina.

  Njia rahisi kwa wanawake wasiopenda kuwajibika kwa maisha yao ni kuwalaumu wanaume, na ndio maana mie hata sishangai ninaposhambuliwa pale ninapoweka mada kuwakosoa wanawake. Mtu anazungumzia kuhusu kuvaa vibaya kwa wanawake kwamba, kunachangia kuwafanya waonekane ni bidhaa, wanawake wengine wanabisha. Kubisha huku ni kukataa kuwajibika. Lakini hata wakibisha, bado jamii zote zinaushikilia huo wanaoukataa kuwa ndiyo ukweli.

  Mtu akijichukulia kwa udhati fulani, wengine nao watamchukulia kwa udhati huo. Akishindwa, wengine nao watashindwa kumchukulia kwa udhati unaostahili. Kama unataka kubishana na hao wengine, ni suala la kujaribu kuipinga hali halisi na kupinga kuwajibika kwa maisha yake. Hebu fikiria, hata kama ni mwanaume. Leo hii mwanasheria wa kiume amevaa 'pensi' huku akiwa ameteremsha mlegezo mpaka makalio yanaonekana na shati la 'ki-modo' na makobazi, unadhani ni nani atamkabidhi kesi yake. Hata kama ni mwanasheria mzuri vipi, labda tu kama mtu anamjua vizuri sana tangu hapo kabla.

  Mwanamke ambaye ni afisa mahali kama Mamndenyi, akienda ofisini na kimini na kitopu chenye kuonesha kitovu, hakuna atakayetilia maanani maneno yake. Mhuni hatiliwi maanani. Kwa jamii, hizo ni nguo za kihuni, iwe ni kweli au sio kweli, ndiyo tafsiri yake. Mwanamke anapovaa kama kifaa, wanaume wanapomzonga au kumchukulia kama kifaa, hilo sio suala la unyanyasaji kijinsia, bali ndiyo hali halisi. Mtu wa zima-moto tunamjua kwa mavazi, mcheza mpira tunamtambua kwa mavazi, mwanafunzi hivyohivyo. Ndiyo maana kuna wakati makahaba wa jijini Dar walikuwa wanavaa kama wanafunzi na mashugadadi wakawa wanawachangamkia sana. Mavazi husema sisi ni nani na ni jamii imepanga siyo wanaume.

  Huwa tunawaambia wengine sisi ni akina nani kwa lugha za ishara za aina mbalimbali, na ndio maana wengi hawashangazwi na majibu ya baadhi ya wana JF wanapojibu hoja humu jamvini, mfano mzuri kama, mzee mwenzangu Rejao, rafiki yangu Bujubuji, Ndyoko, au Washawasha. Hawa wamejijengea sifa moja kubwa humu jamvini, huwa hawamung'unyi maneno. Inawezekana wasichana wengi siku hizi hawajui kwamba huwa wanasema wao ni nani kupitia mavazi. Wanachojua wao ni fasheni ambayo wameiyona kwa wanawake fulani maarufu hususan wa nchi za Magharibi, lakini hawajui jamii inapokea ujumbe gani kwa mavazi yao.
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  MSG sent.
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hata wewe umeona eh! Leo huenda nitakiona cha mtema kuni, ngoja waje Wabeijing hapa!
   
 4. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Shikamoo baba,ujumbe umefika naona umezingatia genda umeongea kwa pande zote!
   
 5. bht

  bht JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  unajishtukia tu

  binafsi linapokuja suala la uvaaji kila mtu kuna anachoangalia (labda umbo lake na rangi ya ngozi yake) na najua pia kuwa kila vazi lina sehemu yake. na hili si kwa wanawake tu hata wanaume mbona wengi tunawaona wanaacha maungo yao wazi (na mnavyotisha sasa...yak)
   
 6. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  kuna uzi umeanziswa wa mapepo/majini/masabuli/masijui nn umeniboa jamani!! samahani babu kwa kuichakachua sledi yako !
   
 7. Akthoo

  Akthoo JF-Expert Member

  #7
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 585
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  Swadakta! Umenena kweli Mtambuzi.
   
 8. Sabry001

  Sabry001 JF-Expert Member

  #8
  Nov 14, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,064
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Leo ukishambuliwa wamekuonea cuz umesema ukweli mtupu!
   
 9. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #9
  Nov 14, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  dah! Mtambuzi..hii research yako uliifanya saa ngapi? kumbe ni hivi! ...nilikuwa sijui aisee!
   
 10. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #10
  Nov 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,091
  Likes Received: 6,557
  Trophy Points: 280
  '.............Mwanamke ambaye ni afisa mahali kama Mamndenyi, akienda ofisini na kimini na kitopu chenye kuonesha kitovu, hakuna atakayetilia maanani maneno yake. Mhuni hatiliwi maanani .................'

  Mkuu nimekukubali sana,
  mkono wako ukipona tu mkuu lazima nikakupe ile kitu roho yako itapenda,
  kwa sasa naendelea kukuombea tu.
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Bee umeongea

  Mwanamke na Mwanamme wote wanatakiwa kuvaa mavazi yanayoendana na matukio au mahala walipo.
   
 12. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #12
  Nov 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,091
  Likes Received: 6,557
  Trophy Points: 280
  mi sijaiona iko wapi,
  lakini babu atakuboa je,
  au umeisoma juu kwa juu.
   
 13. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #13
  Nov 14, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  kuna wengine wanakwenda nyumba za ibada wamevaa kituko utafikiri wanakwenda disco/shivas inaboa vaa kuendana na mahali husika
   
 14. bht

  bht JF-Expert Member

  #14
  Nov 14, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  sasa Mtambuzi asilete mambo za 'blame game' hapa ilhali hili liko wazi kabisa...
  kwa mwanamke au mwanaume linapokuja suala la mavazi, it is all about what, when and where to wear what u want to... (this should tell you how you should get dressed).
   
 15. Brine

  Brine JF-Expert Member

  #15
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 376
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  haswa maana siku hizi wanawake wenzangu wamechoka kujiheshimu
   
 16. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #16
  Nov 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,091
  Likes Received: 6,557
  Trophy Points: 280
  Started by: Teamo
   
 17. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #17
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,699
  Likes Received: 416
  Trophy Points: 180
  nimetuma wakusalimie,barua pia nimetuma,usooome........ Nalog off
   
 18. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #18
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  thatha kama joto limezidi, watafanyaje? inabidi tu wavae hivyo vimini, mgongo mgongo na naiti dress mchana! "Just jokin........"
   
 19. frank lujaju

  frank lujaju Member

  #19
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yaan umenena kila kitu kwa usahihi na wengi eti ujiita ni watu wanaokwenda na wakati jamani c kila kitu uigwa tamaduni nyingine c zetu tunakopi na kupesti,message sent
   
 20. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #20
  Nov 14, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Hahahahaa mtambuzi bana, naona leo umeanza na defence kwanza!! Mi naona issue hapo ni aina ya mavazi, wakati na sehemu uliyopo. Kwa sababu hata huyo mamndenyi mwenyewe hawezi kwenda ofisini juu kavaa mtishirt mkuubwaa, chini kajifunga kanga halafu miguuni kavaa raba mtoni, kisa tu ni nguo ya heshima!!!
   
Loading...