Sasa Kiingereza kitakuwa na kazi gani?

Sasa Kiingereza kitakuwa na kazi gani?

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2020
Posts
279
Reaction score
480
Naona tayari michakato ya sheria iko jikoni mahakama kuanza kutumia Kiswahili mwanzo mwisho tofauti na sasa ambapo dokomenti zote huwa za kiingereza sasa baada ya sheria hii hakimu au mwanasheria yeyote itamlazimu atumie lugha ya kiswahili ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa upande wa BOT nao pia sheria iko jikoni hatua za mwisho mwisho zimefika kuwa mikataba yote ya kifedha itafanyika kwa lugha hadhim ya Kiswahili. Hii inamaana kuwa hadi risiti za mashine hazitakuwa za kizungu bali kwa lugha ya Kiswahili, haya ni pamoja na Pro foma, Delivari note, bili of ladingi na dokomenti zote unazozijuwa wewe ikiwamo za benki zitalazimika kutumia lugha ya Kiswahili.

Swali la msingi je hizi shule za inglishi midia zitakuwa na kazi gani au wataenda kukitumia kiingereza chao huko Uganda na Zambia.
Na kwanini serikali isipige jiwe katikati na kutunga sheria kuwa kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu lugha ya kufundishia iwe Kiswahili na lugha zingine kama Kiingereza na lugha zingine za kigeni ziwe kama masomo.

Hii italeta maana zaidi kuliko hivi sasa taifa lina dobo standadi kwani wengine wanasoma kwa kizungu na wengine kwa Kiswahili hii haileti usawa hata kidogo.

Mbona mataifa mengi nje ya bara la Afrika yanatumia lugha zao kama Korea Kaskazini, Uchina, Urusi, Cuba na mataifa mengi madogo madogo yanatumia lugha zao kama Falme za kiarabu nyingi wanatumia Kiarabu kwani lugha ya mababu zao. Kwanini sisi bara kubwa kuzidi yote duniani hata kanchi kamoja kasiwepo ka kutumia lugha yake, ukiangalia kuna wakati inatia hadi aibu kuona nchi nyingi za kiafrika zinatumia hadi kiingereza na kifaransa kuimba nyimbo yao ya taifa kanakwamba hilo taifa halina lugha yoyote zaidi ya Kiingereza au kifaransa. Huu ni utumwa mbaya uliopitiliza naamini hata Mungu mwenyewe anachanganyikiwa kwani anaangalia eneo ambalo aliliumba mwenyewe na kuweka watu wake pale na lugha yao baadaye wanamwomba kwa lugha nyingine kwana hawezi kuwa sikiliza.

Naona kuna haja ya kujikomboa kutoka katika utumwa wa kifikra.

Na kanisa ndilo limekuwa mstari wa mbele sana kuhakikisha lugha za asili zinapotea kwani ukija huku kwetu kanisani unaweza kushangaa maana utakuta wote tunajua kiswahili na tunajuana na hakuna mgeni wote ni wandengereko lakini anawekwa mkalimani au mchungaji au nabii au mtume anaongea kizungu utazani yupo ulaya au Amerika, nikama sifa hivi kuwa mzungu.. kwa waislam pia hivyo hivyo yaani mpaka ujilaze katika rahaja za kiarabu ndiyo uonekane sasa safi kwa Mungu.

Mimi pamoja na kulelewa na kusoma kwa sadaka huwa sielewi huyu Mungu wetu wa kikristu na wa waislam kwanini huyu Mungu anashida gani na lugha zetu? kwani hizi lugha zina najisi? maana kanisani bila kizungu ibada haiendi kama zamani bila Kilatini ndani ya kanisa la Roma misa hakuna. Msikitini bila kiarabu tena kile cha kikureshi hakuna ibada hii inamaana gani mbona kama utumwa. Nakama Kiswahili kinanajisi basi hawa watu wa dini waseme tukiache kabisa.

Naipongeza serikali ya awamu ya tano ila msipige pembeni pigeni katikati kieleweke ndiyo maana huwa mnasema huku kwenu ndani ya chama kuwa serikali inapewa Jembe na Nyundo basi kama mmepewa msiwe waoga tumieni hizo zana wengine walishindwa. Sehemu ya kutumia Jembe litumike kama lote na sehemu ya kutumia nyundo itumike sisi watu wa roho tunaelewa hizi mithali.

Nimeshuhudia kwa mara ya kwanza mwalimu wa kiswahili Mkenya akiwa darasani shule ya msingi huko Afrika ya Kusini akifundisha kiswahili na watoto wa kisauzi wakionyesha kufurahia na wakitoa komenti kuwa maneno mengi Kiswahili kimeiba maneno kutoka katika lugha ya Kizulu, Shona, sesoto, Kosa na kiswana huku wakiwa wanasahau kuwa kiswahili ni kibantu.
Hii ni kazi ya awamu ya tano.

Mtoto wa Mchungaji,
Nawasilisha.
 
Kwa kifupi UN kila wakitangaza kazi za East Africa ni Wakenya na Waganda wanapeleka maombi kwa wingi. Uwakilishi wetu kwanye kazi za UN ni mdogo mpaka tunapata nafasi za upendeleo lakini zinajazwa na majirani zetu.
 
Sio Kiswahili wala kingerza ambacho kinaweza kutupa faida kama mfumo wa nchi kwenye Elimu haueleweki kila siku Magufuli anaeleza kuhusu lugha lakini naona kama unatoa hela mfuko wa kushoto na kuweka kulia.

Yani Nonsense kabisa
 
Mdogo mdogo, wacha kwanza makali yaonekane! Hatimaye Taifa litatumia lugha tukufu na adhimu ya Kiswahili.
 
Kwa kifupi UN kila wakitangaza kazi za East Africa ni Wakenya na Waganda wanapeleka maombi kwa wingi. Uwakilishi wetu kwanye kazi za UN ni mdogo mpaka tunapata nafasi za upendeleo lakini zinajazwa na majirani zetu.

Naona TATIZO Ni KINGE as far as UN Jobs concerned.
 
Suala la kingereza halina ubish kwamba ndio lugha ya biashara, wengi wanasahau kwamba lugha rasmi Tz ni Eng na Kiswahili.

Hata waseme nini waweke nini kingereza bado ndio lugha pendwa ya kupeleka Ugali nyumbani.

Kulikuwa na wazir flani aliunganisha chemistry na physics na kufuta masomo yote ya kilimo na biashara, sijui aliishia wap
Muda ni mwamlim mzur sana
 
Kwahyo kiongozi wa taifa kuwa na PhD au prof na kushindwa kingereza basi ndo wanahalalisha watoto wasome kiswahili KWA lazima. English ni international language na ndo inatumika kote na kifaransa tuache kujifariji na kiswahili ambayo imelack vocabularies mbaya zaidi wanaokuja na hizi sera ni wazee ambao miaka yao ya kuishi duniani imebaki michache. Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa
 
Kwani kumetokea nini huko kwenye sheria zilizoandikwa kwa kingereza mpaka zibadilishwe kuwa za kiswahili, isije ikawa tunapinga vitu hapa kumbe wenye Nchi kuna kitu wameona.......ila kama ni mtu mmoja kaamua tu kwa matwaka yake basi hilo nalo ni tatizo lingine.
 
wanasiasa wa Tanzania wanavuka mipaka yao. Unaamua kitu cha kusomwa mwashuleni bila utafiti, bila consultation ya kitaalam, bila mijadala ya kitaifa? Just bin vuu jukwaani unaamua watoto wetu wasome nini? Kwanini lakini?
 
Sisi watanzania ni sitaki nataka na mimi nikiwemo, kuna kipindi tulitaka elimu iwe kwa kiswahili ngazi zote ila sasa tunaona mzee kaanzia mbali sana. Ni kweli lakini

Sasa nirudi kwenye ukigeugeu

Mfumo wa sheria kutawaliwa na kiswahili ni kosa kwa ninavyoona mimi, tukumbuke kuna mawakili kutoka nchi za jumuiya ya madola wanaweza kufanya petition kwa CJ wakawakilisha wateja wao mahakama za Tz sasa itakuwaje??

Tukumbuke Tz kuna makampuni ya kigeni na ya ndani yanayotumia mawakili kutoka nchi nyingine nao watafanyajee?

Ila bora maana na sisi tutapata wateja kwa kiswahili chetu maana hadi wandugu wakijue kiswahili sio leo wala kesho. Ahsante Magu japo sio poa pia.
 
Ahahahahaaaaa hii ndio bongo bana,yenye watu wenye dharau na majigambo wakati hawana kitu, nikitazama na kufikili naona kuna ujinga mwingi sana, hao hao wanategemea kila kitu kutoka kwa wazungu,ndege ,magar ,treni ,mawasiliano,silaha yaani kila kitu ambavyo ili kuvielewa matumizi yake lazima ujue kiinglish na kuna vingine ili uvijue ni lazima uende training kwa hao hao wainglish, wanaowadanganya wengine wao watoto wao wanasoma international schools zenye mitaala ya wainglish,
Kweli wanyonye lazima waendelee kuwa wanyonge tu mpaka kiama
 
Hatutaweza kwa Kiswahili. Hatuna uchumi wa kuweza kuinfluence Lugha ya Kiswahili. Na ukweli ni kwamba tutaanzisha kipindi hiki tu akiwa madarakani. Akiondoka tunaipiga chini kama tulivyoipiga chini Physics with Chemistry ya Mungai. Anatumia rasilimali za nchi vibaya. Zitakuwa lost resources.
 
Back
Top Bottom