Sasa kama kumbe Kutokukoma kwa Teuzi ni Agenda ya Siri ya CCM kuwa kila mwana CCM lazima ale Keki ya nchi kwanini msiseme tu?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,738
109,177
Nasikia umeshauriwa na Mtu unayemuamini na kumsikiliza mno kuwa ili mwaka 2025 upate Uungwaji mkono na wana CCM wote hakikisha kila mara unawapa Ulaji ili Waibe na Wajitosheleze kisha unawapa na Fursa hiyo hiyo na Wengine ili wapige na hadi hiyo 2025 wasije Kukulaumu.

Nimedokezwa kuwa kati ya Mwezi August na October 2023 kutafanyika Mabadiliko mengine ili huu Utamaduni wa Kula kwa pamoja Keki tamu ya Taifa kwa wana CCM uendelee huku Watanzania wengi wakiendelea tu Kutaabika na Msoto wa Kimaisha.

Ngoja tuendelee Kunywa Mtori taratibu na huenda Nyama tutazikuta chini zikiwa tamu.
 
Kuna mmoja huko kwao nchi jirani, yeye aliita nchi hiyo ....... limited company, wananchi wa huko wakamjia juu. Aliwajibu kuwa kwenye kampuni kuna hisa, na wenye hisa ndio hao waliowachagua kuingia madarakani, na ndio watakaofaidi matunda ya nchi. Kuhusu kila mwana ccm kuonja keki ya nchi hii ni kawaida, na ndio sababu kuu kila mwanachi kujiunga na chama hicho ili ikifika wasaa wake wa kulamba asali naye alambe. Hao wengine wataambulia kama zile chengachenga zinazoanguka chini sisimizi wanazifaidi
 
Back
Top Bottom