Sasa imegusa Ikulu, imechafuka... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa imegusa Ikulu, imechafuka...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ngoshwe, Nov 20, 2011.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Haya yapo katika mfumo wa Uongozi wetu sasa (Mhe. Tundu Lissu mlimsikia aliponukuu maneno ya Hayati Baba wa Taifa Kuhusu Uongozi wetu na tulipofikia): Mamlaka ya Uteuzi ya Katibu Mkuu Kiongozi: Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania (kwa sasa ni Bw. Philemon Luhanjo ambae alitoka na Mhe. Rais Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiana wa Kimataifa) Mamlaka ya Uteuzi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini: Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Mamlaka ya Uteuzi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Mamlaka ya Uteuzi ya Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru (PCCB): Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Mamlaka ya Uteuzi ya Mdhibiti wa Hesabu za Serikali: Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania. Mtakumbuka kuwa wakati wa kujadili ripoti ya Kamati Teule ya Bunge ya Richmond, kamati ilibanisha wazi kuwa Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru imehusika kwa karibu sana kuupotosha Umma pale ilipobainisha kuwa hakukuwa na ukiukwaji wa Sheria.Kamati ilibaini pia kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa wakati huo akiwa Bw. Johnson Mwanyika (rtd) imeishauri vibaya Serikali na kujikuta ikiingia katika mkataba ambao kama Mwanasheria Mkuu angekuwa makini, basi Taifa lisingeingizwa mkeknge hiuo ambao sasa unaligharibu kwa kutakiwa kulipa takriban Bilioni 110 kwa kampuni ya hewa ya Dowans.Kamati Teule chini ya Uongozi wa Mhe, Mwakyembe ilitoa Mapendekezo yafuatayo:Kamati Teule ya Bunge ya Kuchunguza suala la Bw. David Kitundu Jairo (Katibu Mkuu aliyesimamishwa wa Wizara ya Nishati na Madini) ilibainisha mapungufu makubwa katika Serikali ya JK kusimamia mambo mazito hasa yanayohusu fedha za Umma. Mapungufu haya yameanzia IKULU kwenyewe, ambapo Katibu Mkuu Kiongozi ni kama yupo juu ya Waziri Mkuu na ametumia Ofisi yake Vibaya kupoitosha Umma kuwa Jairo hana hatia ya kufuja fedha za umma (alifanya hivyo kwa sababau binafsi za Kumsafisha kwa staili ile ile iliyowsafisha akina Patrick Rutabanzibwa, Arthur Gwanaloli K. Mwakapugi., Johnson Mwanyika, Edward Hosea, Donald Chidowu na wenzake kwa hofu kuwa wakicvhukuliwa hatua Serikali itajikuta ikiingia katika mzigo mwnigine Mkubwa wa kulipa deni iwapo itashindwa Mahakamani kama watumishi hao wangefungua kesi kutokana na kutoridhika na hatua za Nidhamu zilizochukuliwa. Wakati ule, Ofisi ya Waziri Mkuu ndio iliyotoa taarifa Bungezi za Kuwasafisha watendaji hao wa Umma, hivyo kwenda Kinyume na Mapendekezo ya Kamati Teule ya Bunge (somahttp://lukwangule.blogspot.com/2008/08/taarifa-ya-waziri-mkuu-kuhusu-richmond.html).
   
 2. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  tunasubiri tuone nini kitafuatia. Nalog off
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Nov 20, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kha! yaani Mkuu hujui nini kitafuata? Hii inapotezewa kiaina kwa kutafuta mbyuzi wa kafara wawili watatu, halafu wakubwa wataendelea kupeta kama kawa kwa kisingizio kuwa hatua zimeshachukuliwa na nyingine zinazohitaji mabadiliko ya sheria zinafanyiwa kazi. Naamini kwa dhati kabisa kuwa hakuna mabadiliko makubwa yatakayotokea kwa sababu hakuna kati ya haya yaliyosemwa na kamati teule ya Bunge ambayo serikali ilikuwa haiyafahamu, kama kuchukua hatua wangeshachukua miaka mingi iliyopita. Watzanzania tumeshageuzwa kuwa Mbuzi wa shughuli
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Nov 20, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Sitashangaa Luhanjo akisema Jk anaijua vizuri hii issue
   
 5. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #5
  Nov 20, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mkuu usi log off tafadhali,komaa hapa hapa mpaka tuone hatma!ikibidi kupigana ngumi tupigane tu, itafika mahala waziri anavurunda wananchi mnatanda barabara mnamshusha kwenye gari "yenu"shangingi mnampa kichapo mpaka atapike hela alizoiba
   
 6. V

  Vonix JF-Expert Member

  #6
  Nov 20, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 1,987
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Umeandika mada yako safi sana ila labda kama ungekuwa utawala mwingine na sio huu wa jk sawa ila kwa huyu ****** hapo hamna kitu,sanasana saa hizi akina salva wako bize kusuka mikakati ya kuipotezea.issue iko hot ila ni sawa tu ilivyokuwa ile ya richmond maazimio ya bunge 23 yalitoka uliona hata moja limetekelezwa????wanaishia kusema serikali inashughulikia.Yetu macho kweli utawala huu ni hamnazo.
   
 7. M

  MWANAKASULU Senior Member

  #7
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Imechafuka zaidi ya maelezo na aliyeichafua ni huyo jk mwenye madaraka makubwa kupindukia zaidi hata yale aliyokuwanayo mfalme **** sasa wanamagamba wenzake wamerubuniwa aendelee kuwa na madaraka makubwa tena kwenye uundaji wa tume ya kupata katiba mpya hii jamani ni hatari.LAANA ITAWAANGUKIA WANAMAGAMBA waliopitisha mswaada bungeni.
   
 8. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #8
  Nov 20, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mkuu mapendekezo yataishia kabatini kama ripoti zilizotangulia
   
 9. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  Halafu mbuzi wenyewe wanakuwa wale waliokonda/wagonjwa ndio wanawatoa kafara,dah! Híì serikali ni kama vile mchezo wa kuigiza. Nalog off
   
 10. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #10
  Nov 20, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  Hawa dawa yao ni kuwaonesha dhahiri kuwa hatuwakubali viongozi wa namna yao,kwa kuwafanyia vurugu. Nalog off
   
 11. kirumonjeta

  kirumonjeta JF-Expert Member

  #11
  Nov 20, 2011
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 3,072
  Likes Received: 484
  Trophy Points: 180
  Hapa tunazidi kuyajua MAGAMBA zaidi,itashangaza 2015 watu wakapokea vitenge na vyandarua wakayarudisha tena magamba haya bungeni
   
 12. D

  Deo JF-Expert Member

  #12
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,190
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ikulu siku zote chafu, hata richmondi na hata sasa.

  Kwani mkuu hakuona?

  pida alistahili kudharauliwa kwa matendo na kazi zake, ona utendaji wake. Subiri hata hii atakavyofanya kama ile ya richmond. Jairo atafukuzwa baada ya kustaafu. Hii serekali bana!

  Subiri mchezo wa kuigiza na suala litachukuliwa personal si ya kamati kama Mwakyembe.
   
 13. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #13
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  47. Offences and penalties:
  (2) Any staff of the National Audit Office, an auditor and an expert acting on behalf of the Controller and Auditor-General commits an offence if he-
  (a) demands or takes bribe, recompense or reward for the neglect or non-performance of duty;
  (b) willfully fails to report to the Controller and Auditor-General any abuse or irregularity that comes to his notice in the course of auditing duties;
  (c) makes any report to the Controller and Auditor-General which he knows to be false or has no reason to believe it to be true;
  (d) abuses his powers, engages in malpractices for personal gains, neglects duties or divulge State's or auditee's business secrets; or
  (e) any other matter as the Controller and Auditor-General may consider an offense.
  (3) When the Controller and Auditor-General has reason to believe that an offence has occurred, he shall refer the matter to the Director of Public Prosecutions for appropriate action.
   
 14. p

  politiki JF-Expert Member

  #14
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
   
 15. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #15
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Laiti tungalijua tuendako!!! Yaliyomkumba Masha, yatamkuta Ngeleja na wale wote ambao wanalazimisha madaraka akiwemo Januari Makamba!!,wataumbuka wote!!
   
 16. l

  limited JF-Expert Member

  #16
  Nov 21, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  rais ana madaraka mengi sana na sasa yanatusumbua kwenye mfumo wetu wa uongozi. hii ni mbaya kwa bahati mbaya siku tunapata raisi kichaaa tumekwisha.
   
 17. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #17
  Nov 22, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Tatizo letu watanzania ni kusahau haraka! Likizuka jambo kidogo (mfano watu wasikie kuna babu kimbiji anatibu magonjwa kwa kutumia fanta) tu kila mtu keshasahau madudu ya nishati na madini anakimbilia kimbiji maisha yanaendelea ufisadi unaota mizizi na 2015 magamba yanarudishwa madarakani!
   
 18. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #18
  Nov 22, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hivi kumbe bado hatujampata eh?
   
 19. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #19
  Nov 22, 2011
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,610
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mh yetu macho, tusubiri tuone mwisho wake.
   
 20. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #20
  Nov 22, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  sitashangaa JAIRO akisema kuwa hawakujuna na kikwete kwenye siasa!!!!
   
Loading...