Sasa hawaitaki tena Katiba ya Warioba, wanataka kama ile ya Marekani yenye mfumo wa utawala wa majimbo

Dr Akili,

Hao wajasiriamali, hata saccos yao imewashinda ndio iwe nchi. Sioni kiongozi kule anayeweza, tuvusha kwenda uchumi wa juu zaidi. Ukisikia Rais Magufuli anasema uongozi haujaribiwi, wengi wanadhani anatania. Lissu na saccos yao hawana pa kutupeleka watanzania, huo ndio ukweli.
 
Ukitaka kuwaelewa hawa makamanda yakupasa kuwa mwendawazimu kidogo. Leo mgombea wao atasema tutaanzia pale alipoishia Warioba. Kesho utasikia tutaweka majimbo. Tatizo hawako madubuti na sera zao. Wanadandia chochote kinacholetwa na upepo (wa kisulisuli?).
 
Muamke mchukue hatua, kumbuka siku zote hizo mko madarakani, sasa sijui muamkeje , Amka kwa kukitoa chama dhalimu madarakani.

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Majimbo yakipewa mamlaka kamili maendeleo yatalipuka kwa kasi na kwa uwiano uliosawa, let us decentralise the country sio kila kitu cha nchi kiamuliwe dar na watu wawili tu.
Hulka ni zile zile, watu ni wale wale, ni kisingizio tu cha umaskini.
 
Tundu lissu ametumwa kuja kusambaratisha nchi, sheria ya majimbo ni hatari sana kwa umoja wetu
 
..Kweli.

..wananchi watakuwa ombaomba kwa Raisi, na akiwa mchoyo watakwenda kwa Gavana, ikishindikana kwa mkuu wa mkoa.

..sasa hivi Raisi akiamua kuwanyima wananchi maendeleo, basi imekula kwao, hawana mwingine wa kuwaletea maendeleo.

Sio kweli. Wewe kama mwananchi unaweza kumpa wazo lako mbunge wako nae akalipeleka bungeni kama muswada na likatungiwa sheria.

Na hiyo sheria ikaifaidisha nchi nzima kuanzia hapo ulipozaliwa.

Tatizo letu ni kupenda kulalamika na kutafuta mtu wa kumtupia mzigo wa lawama. Wakati tunao uhuru wa kuyafanya tulionayo vichwani mwetu yakawa na tija kwa taifa letu.
 
Hadi vyoo tunamwomba Rais..

Rais ana shughlikia hadi madarasa.. vyoo, street lights .. aibu kabisa..

Rais wa nchi alitakiwa kushughlikia mambo makubwa..
..tumechoka kuwa ombaomba wa fedha za maendeleo kwa Raisi.

..tunataka baadhi ya makusanyo ya serikali yabaki ktk mikoa yalipokusanywa na kusaidia maendeleo.

..serikali kuu itaongezea pale ambapo majimbo au mikoa imepungukiwa.
 
Kamanda mnataka katiba ya Warioba au mnataka mtengeneze yenu ya majimbo?
..tumechoka kuwa ombaomba wa fedha za maendeleo kwa Raisi.

..tunataka baadhi ya makusanyo ya serikali yabaki ktk mikoa yalipokusanywa na kusaidia maendeleo.

..serikali kuu itaongezea pale ambapo majimbo au mikoa imepungukiwa.
 
Hao wajasiriamali, hata saccos yao imewashinda ndio iwe nchi. Sioni kiongozi kule anayeweza, tuvusha kwenda uchumi wa juu zaidi. Ukisikia Rais Magufuli anasema uongozi haujaribiwi, wengi wanadhani anatania. Lissu na saccos yao hawana pa kutupeleka watanzania, huo ndio ukweli.
Nauliza je nani alizaliwa kuwa kiongozi au kujua kama atakuwa kiongozi?
 
Majimbo na states ni vitu tofauti. Mfumo anayoizungumzia Lissu uko kwenye nchi nyingi including South Afica
Hata katiba ya Warioba ilizungumzia kwa urefu devolution na ndicho wanachokilenga chadema.

Tatizo la hawa wenzetu huwa hawajishughulishi walau kusoma kidogo
 
Asili ya sera ya majimbo ni ubinafsi wa wale walioibuni. Wametazama rasilimali walizonazo wakajidanganya kwamba wanaweza kujitegemea, dead wrong.

Utajiri wa ardhini haulingani na moyo wa upendo wenye kumtanguliza mtu pasipo kutazama asili yake ni wapi.

Ukianzisha majimbo umeua kitu kinachoitwa a sense of belonging, ile hali ya umoja ambayo ndio msingi wa utaifa imara.
Hivi umoja wa kitaifa wa nchi yetu unaweza kulinganisha na Marekani?Hapa kwetu tukipata adui tu kuna Watanzania wengi tu watakuwa upande wa adui!Hiyo ni tofauti na Marekani,wataparuana wenyewe kwenye siasa zao ila akitokea adui basi utashangaa wanavyokuwa wamoja!

Tanzania jambo kubwa linaloleta utengano ni siasa za kishamba na zilizopitwa na wakati!
 
Tukikubaliana na sera ya majimbo hata huu umoja wetu ambao haulingani na ule wa Marekani itabidi tuusahau!.

Siasa za kishamba ni tafsiri binafsi ya mtu mmoja mmoja. Sera ya majimbo haitafuta hizo siasa za ushamba na zilizopitwa na wakati kwani utaibuka ushamba mwingine huko huko majimboni.
 
Hujaelewa,hapa nakuelemisha kuwa sera ya kuanzisha majimbo iwapo itatengenezewa utaratibu mzuri inaweza kuwa na tija na isilete huo mgawanyiko unaouhubiri hapa!Ndio nikakupa na mfano!Lakini nimekueleza,Tanzania hatuna huo mfumo lakini siasa zetu za majitaka zimetugawa sana!Tanzania ya leo si ile ya Nyerere yenye uzalendo na umoja!Huwezi kunitesea ndugu zangu bila sababu wala misingi ya kisheria halafu utegemee upendo na ushirikiano kutoka kwangu!Huwezi kudharau maamuzi yangu katika sanduku la kura halafu utegemee ushirikiano wangu kwako!
Haki siku zote huinua taifa!Bado tunasurvive kwa sababu ya misingi imara ya amani na umoja aliyoiweka Nyerere!Na watawala wanalichukulia hilo kama advantage kwao kuendelea kutenda watakavyo!Wanasahau hata plastic ikivutwa sana kuna hatua itafikia stage inaitwa permanent deformation na hapo sasa its just a matter of time kabla haijakatika!
 
Dr Akili,

Hao wajasiriamali, hata saccos yao imewashinda ndio iwe nchi. Sioni kiongozi kule anayeweza, tuvusha kwenda uchumi wa juu zaidi. Ukisikia Rais Magufuli anasema uongozi haujaribiwi, wengi wanadhani anatania. Lissu na saccos yao hawana pa kutupeleka watanzania, huo ndio ukweli.
Sasa yeye alipokuwa anabeep anakuwa hajaribu .....!!?
 
Back
Top Bottom