Sasa hawaitaki tena Katiba ya Warioba, wanataka kama ile ya Marekani yenye mfumo wa utawala wa majimbo

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
3,614
2,000
Sasa wameweka wazi aina ya katiba mpya wanayoitaka. Wanakusudia kuufumua kabisa mfumo wa utawala wa nchi yetu na kuufanya uwe kama ule wa Marekani wa majimbo yanayojitegemea.

Nchi yetu itagawanywa kwenye majimbo (kanda) kama tisa hivi kama zilivyo kanda za chama hicho. Kila kanda itaongozwa na gavana ambaye atachaguliwa na wananchi wote wa kanda hiyo kwenye uchaguzi mkuu. Katika uchaguzi mkuu huo watachaguliwa pia wasaidizi wa gavana wa jimbo (magavana wa wilaya), watendaji wakuu (province and district chief executive officers) ambao ndiyo watakuwa maafisa masululi. Pia watachaguliwa wawakilishi wa wananchi (senators badala ya madiwani) kwenye bunge lao la jimbo (senate).

Gavana wa jimbo atakuwa na mamlaka kamili ya kiutawala katika jimbo lake na hatawajibika kwa rais wa JMT. Atakuwa na mamlaka ya kukusanya mapato yote (kodi) yanayozalizwa jimboni kwake na kuyatumia kwa maendeleo ya jimbo lake kwa idhini ya senate. Atakuwa mkuu wa majeshi ya usalama ya jimbo, atakuwa mwajri wa watumishi wote wa umma jimboni kwake na kadhalika.

Kwa ufupi serikali za majimbo/ kanda zitakuwa ni states kamili kama zilivyo huko Marekani. Kazi za rais wa JMT zitabaki tu zile za uhusiano wa kimataifa na uamiri mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania. Majeshi mengine kama ya polisi yatakuwa kwenye mamlaka ya magavana wa majimbo. Fedha za uendeshaji wa shughuli za rais wa JMT atazipata kutoka kwenye ruzuku ambayo atakuwa anapewa na magavana wa majimbo. Yaani tuta copy, paste and install the government adminstrative system of the United States of Amerika. Ndiyo maana bunge la USA limekuwa likiufatilia sana kwa karibu uchaguzi wetu huu.

Haya yatakuwa ni mabadiliko makubwa sana ya katiba yetu. Yale ya katiba ya Waryoba ni cha mtoto. Uzuri ni kuwa ile idadi ya theluthi mbili za wabunge wote inayohitajika kubadili katiba hawa jamaa hawataipata.

Tusipende kubadili katiba ya nchi kwa matakwa ya wanasiasa. Nchi nyingi za Afrika ikiwemo ya majirani wetu tumeshudia matatizo makubwa wanayoyapata. Katiba yetu ni kati ya katiba bora sana Afrika. Mfumo wetu wa utawala wa serikali unazingatia dhana muhimu ya demokrasia ya serikali ya watu wote kwa manufaa ya watu wote na inaendeshwa na watu wote kupitia wawakilishi wao (wabunge na madiwani). Madaraka yote ya serikali yanawekwa na watu wote.

Wananchi wote kupitia uchaguzi mkuu humukabidhi rais mamlaka (power) ya utawala wa nchi kwa mjibu wa katiba ya nchi iliyowekwa na wananchi wote. Yeye ndiye muajibikaji wa kila jambo linalotendeka nchini mwao. The back stops on him for every matter. Anawajibika moja kwa moja kwa wananchi wote kupitia wawakilishi wao bungeni ambao wana mamlaka kamili ya kumuondoa madarakani wakati wo wote kwa utaratibu waliouweka.

Huyu mgombea amekuwa akizunguka akidanganya wananchi kwenye kampeni zake kuwa eti kwa mjibu wa katiba yetu ya sasa rais wa JMT hawajibiki kwa yo yote. Ukweli ni kuwa anawajibika kwa wananchi waliomchagua na kumuweka madarakani kupitia wabunge wao bungeni. Nchi kama ya Afrika kusini, rais wao anawajibika kwa chama chake tu na si kwa wananchi wa Afrika kusini. Rais wa South Afrika hachaguliwi na wananchi wa South Africa. Wao katika uchaguzi mkuu huchagua vyama vya siasa tu. Chama kinakoshinda ndicho huchagua rais na wasaidizi wake.

Chama kilichoshinda kinaweza mbadilisha rais wakati wo wote kinavyopenda. Hata huko Amerika rais wao hachaguliwi na wananchi wote wa Amerika bali na kakikundi kadogo ka mabepari ambako kana watu mia tano tu - kinaitwa electrol voters. Kura za wananchi (popular votes) ni sawa na kura za wajumbe hapa kwetu. Mtu anaweza akaongoza kwa mbali kwenye popular votes (kama alivyoongoza Hillary Clinton mwaka 2016) lakini akakatwa na hao electoral voters. Hivyo rais wa Marekani anwajibika kwa hilo kundi la mabepari (captalists) lililomweka madarakani na siyo hao wajumbe! Sasa kwa akili ya kawaida nani ana katiba inayozingatia zaidi dhana ya demokrasia kati yetu na hao?

Haihitaji akili ya ziada kujua kuwa huo mfumo wa utawala wa serikali wa majimbo utakaoletwa na hawa jamaa zetu kimaendeleo na kwenye kila kitu utaigawa nchi yetu vipande vipande na kikabila. Kanda zenye neema za rasilimali zitakuwa kama ulaya na zingine zitakuwa kama jehenamu. Imagine likanda kama la wasukuma lenye madhahabu na maliasili zingine kedekede litakuwaje? Hizo SGR, Nyerere hydroelectic dam, bormbadier na miradi mikubwamikubwa yenye manufaa kwa nchi yote huyo rais wa JMT atapata wapi fedha za kufanya yote hayo ikiwa pesa yake itategemea ruzuku ya magavana wa majimbo? Yaani rais wetu tuliomchagua wote ndiye awe wa kupewa ruzuku na serikali za mitaa badala ya yeye kuzipatia ruzuku. Yaani wajemeni hii ni kitu gani? Hayo mafisadi na mabadhilifu wa mali za umma yakiwemo baadhi ya hayo magavana wa majimbo nani atayatumbua? Mahesabu yao nani atayakagua na kuuadhibiti? Hao watumishi hewa, wanafunzi hewa, miradi hewa, vyeti feki nk nani atalala nao mbele?

Tatizo la hiki chama hakina watu wenye weledi na uzoefu katika utumishi wa serikali. Hawajawahi kufanya kazi yo yote serikalini. Hawajui historia ya hii MacKenz government administrative system imeanzia wapi na imefikia wapi? Walichonacho uzoefu ni uongozi na utawala wa vi saccos. Wanataka kuofanya nchi yetu kuwa saccos yao. Tuamke, tuchukue hatua tarehe 28 Oct 2020.
 

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
5,975
2,000
Katiba ya Warioba inataka serikali tatu; ya Tanganyika, ya Zanzibar na ya Muungano. Chadema inataka kuwa na serikali ya majimbo huku Tanganyika na Zanzibar wataamuua wenyewe namna ya kujitawala. Usichoelewa ni nini wewe mburula?
 

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
13,140
2,000
Asili ya sera ya majimbo ni ubinafsi wa wale walioibuni. Wametazama rasilimali walizonazo wakajidanganya kwamba wanaweza kujitegemea, dead wrong.

Utajiri wa ardhini haulingani na moyo wa upendo wenye kumtanguliza mtu pasipo kutazama asili yake ni wapi.

Ukianzisha majimbo umeua kitu kinachoitwa a sense of belonging, ile hali ya umoja ambayo ndio msingi wa utaifa imara.
 

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
13,140
2,000
Nchi ina watu milioni 70 ila wanaofaidi nchi hawazidi kumi, serikali ya majimbo ndo mwarobaini wa hii Kero, haiwezekani mambo ya shinyanga yaamuliwe na bashite aliyeko dar!

Bunge linapaswa kuwa na wawakilishi wenye haki sawa za kuwasilisha maoni ya wananchi.

Huo ubinafsi wa majimbo ni kwa mataifa mengine sio Tanzania hii tunayoifahamu.
 

Nazgur

JF-Expert Member
Apr 19, 2020
1,908
2,000
..tumechoka kuwa ombaomba wa fedha za maendeleo kwa Raisi.

..tunataka baadhi ya makusanyo ya serikali yabaki ktk mikoa yalipokusanywa na kusaidia maendeleo.

..serikali kuu itaongezea pale ambapo majimbo au mikoa imepungukiwa.
Hata ukiwa na gavana bado mwananchi atakuwa ombaomba kwa gavana.
 

Blac kid

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
5,388
2,000
Bunge linapaswa kuwa na wawakilishi wenye haki sawa za kuwasilisha maoni ya wananchi.

Huo ubinafsi wa majimbo ni kwa mataifa mengine sio Tanzania hii tunayoifahamu.
Majimbo yakipewa mamlaka kamili maendeleo yatalipuka kwa kasi na kwa uwiano uliosawa, let us decentralise the country sio kila kitu cha nchi kiamuliwe dar na watu wawili tu.
 

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
3,614
2,000
..hiyo ni proposal tu.

..kama kuna jambo halitufai tunaweza kuliondoa.

..na kama kuna jambo zuri na halipo ktk hiyo proposal tunatakiwa kuliongeza.

..uzuri ni kwamba mwisho wa siku Katiba Mpya hupigiwa kura ya ndio au hapana na wananchi.
Kwenye hizi kampeni tunanadi ilani. Na ilani siyo proposal. Ni ahadi au mkataba kati ya wenye ilani na wananchi kwamba wakichaguliwa watayafanya yale yote yaliyo kwenye ilani yao. Kwenye hizi kampeni wagombea huwashawishi na kuwatongoza wapiga kura uzuri wa hizo ilani (ahadi) zao.

Kwa hiyo ndicho hawa jamaa watakachofanya tutakapowapa kura nyingi wagombea wao wa ubunge na urais na kuchukua mamlaka ya nchi. Wakuweza kupata theluthi mbili au zaidi za wabunge wote bungeni na kushinda urais lazima hiki ndicho watakachofanya. They are not joking or giving a proposal. Hata ukiwatazama kwenye macho yao na body language zao they are very serious about this na ndiyo maana bunge la Marekani (?lililowatuma) linafuatilia kwa karibu na kutuwekea mashinikizo ili hawa jamaa washinde!
 

Kashaija72

Senior Member
May 18, 2020
157
250
Nchi ina watu milioni 70 ila wanaofaidi nchi hawazidi kumi, serikali ya majimbo ndo mwarobaini wa hii Kero, haiwezekani mambo ya shinyanga yaamuliwe na bashite aliyeko dar!
Hizi data za idadi ya watu mnazipata wapi, nazihitaji tafadhari
 

Interested Observer

JF-Expert Member
Mar 27, 2006
1,869
2,000
Kwenye hizi kampeni tunanadi ilani. Na ilani siyo proposal. Ni ahadi au mkataba kati ya wenye ilani na wananchi kwamba wakichaguliwa watayafanya yale yote yaliyo kwenye ilani yao. Kwenye hizi kampeni wagombea huwashawishi na kuwatongoza wapiga kura uzuri wa hizo ilani (ahadi) zao. Kwa hiyo ndicho hawa jamaa watakachofanya tutakapowapa kura nyingi wagombea wao wa ubunge na urais na kuchukua mamlaka ya nchi. Wakuweza kupata theluthi mbili au zaidi za wabunge wote bungeni na kushinda urais lazima hiki ndicho watakachofanya. They are not joking or giving a proposal. Hata ukiwatazama kwenye macho yao na body language zao they are very serious about this na ndiyo maana bunge la Marekani (?lililowatuma) linafuatilia kwa karibu na kutuwekea mashinikizo ili hawa jamaa washinde!
Mr. Akili, I fail to call you a doctor(A PhD or MD). Uchaguzi hauna formula kama wewe unapotaka ku-propose au ku suggest. Kuna vitu ambavyo vipo wazi, you can use anything you want, according to your selected strategy. Ofcourse Lisu au Magu wote wameenda mbali wakafanya SWOT analysis. What are my strengths, weaknesses and opportunities ofcourse without forgetting threats from my opponent. Hamna formula zaidi ya hapo. Any strategy hupangwa na kutekelezwa kwa ku assess through that. Lisu anazo opening nyingi mno kwa Magufuli, let him use them. Lisu is Agile, Intelligent and enegetic (young); na anaweza kufanya hoja, flamboyantly and bombastically, and is workingg.

CCM mwaka 2015 walimtukana Lowasa matusi mabaya sana ohoo sijui anakojoa, hajiwezi ana ugonjwa sijui wa nini, hamkumbuki. Lisu wala haja tukana mnasema oohh hana sera. Hamsikii?? Siasa za majimbo, (though I was not aware), ni kweli Lisu ni right. Mkuu wa mkoa anayechaguliwa na Rais hana uwajibikaji kwa wananchi kama mkuu wa Jimbo ambaye tunamchagua sisi wananchi.

Halafu usifanye exaggeration ya siasa za Majimbo za Lisu ati ukaleta majimbo ya Marekani. Lisu anasema majimbo ya Tanzania yalikuwapo tangu zamani ni CCM ndiyo wamegawanya ili kuwapa madaraka makada wao, mfumo ambao umeongeza gharama za uendeshaji.
 

Larson

JF-Expert Member
Dec 9, 2015
253
250
Siku mkiacha UCHAMA hata akili zenu zitafanya kazi
Kwa matunda yao, mtawatambua. Chama hi reflect wenye chama. Chama saccos, Sera zao, akili zipo kipigaji tu. Hatuwezi kubali upuuzi tena.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom