Sarakasi za CT Scanner, MRI na vipaumbele vyetu

Sarakasi za CT Scanner, MRI na vipaumbele vyetu

gollocko

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
2,945
Reaction score
2,283
Baada ya kutoa sifa nyingi kwa raisi wetu kwa kufanya ziara za kushtukiza pale muhimbili ambazo ni kama zimezaa matunda kwa kipimo cha MRI kuanza kufanya kazi, hebu sasa na tujiulize juu ya viapaumbele vya serikali yetu kama vipo sawa.

Hebu tuangalie kuhusu vipimo hivi viwili vya ct scanner na mri. Kwa mujibu wa wizara ya afya vipimo hivi vilisuswa kufanyiwa matengenezo baada ya kampuni ya Phillips kutolipwa deni lake kuvifanyia ukarabati vipimo hivyo ambalo limefikia bil. 7. Na juzi wamelipwa bil. 3 ndio kikafanyiwa matengenezo. Kwa maana hiyo serikali bado inadaiwa bil.4.

Tanzania tunavipimo hivyi katika hospitali moja tu ya muhimbili kati ya hospitali zote za serikali hapa nchini, hiki ni kichekesho na tena ni aibu!

Kwa mujibu wa kampuni ya Phillips, moja ya makampuni yanayotengeza hivi vipimo, bei ya hivi vipimo ni kati ya USD 150,000 - 250,000 yaani sh. Mil 300 _ 500 za kitanzania kwa ct scanner ya slice 16 na USD 250,000 - 300,000 yaani Tsh. Mil. 500 - mil 600. Kwa ct scanner ya slice 64. Na gharama za kuifunga pamoja na mafunzo ni tsh mil. 200.

Kipimo cha MRI chenyewe huuzwa kwa USD 400,000 ambazo ni sawa na tsh mil. 840. Na gharama za mafunzo na kuifunga ni tsh. Mil. 300.

Kwa mujibu wa deni wanalotudai hao Phillips la matengenezo tu tungeweza kununua mashine mbili za mri na ct scanner tatu.

Tarehe 20 october kabla ya uchaguzi aliyekua raisi wetu alipokea magari mapya ya washawasha 399, ambayo ni miongoni mwa magari 777 ambayo serikali imeyaagiza kwa ajili ya uchaguzi, ambayo hayakutumika hata magari 50. Hapa ndio pakujiuliza magari yote 777 yalikuwa ma umuhimu gani!

Kwa mujibu wa mtandao wa alibaba, gari moja la washawasha(Riot control vehicle) lenye uwezo wa kubeba little 11500 za cinamon water(maji ya kuwasha), linauzwa kwa USD 250,000 - 400,000. Ambazo ni sawa na tsh mil 500 - 800!

Kwa maana hiyo gari ya washawasha moja na mashine ya mri moja bei hazitofautiani. Kwa maana hiyo yangepunguzwa magari 50 tu, serikali ingeweza kuzifunga mashine za mri na ct scanner katika hospitali zote za mikoa.

Hii inaonyesha serikalini kuna hela, tatizo ni vipaumbele vyetu ambavyo ni vibovu. Chekecha bongo ujue ni kwanini gari la washawasha ni bora kuliko vipimo muhimu kama hivi!
 
Nimesoma ulichokiandika nikajikuta machozi yananitoka! Na tutegemee majibu ya uongo ya CT Scanner na MRI kwa sababu kila mtu ataogopa kusema kuwa ni mbovu! Hahahaa tutapewa report za ajabu sana, ngoja si tupo hapa! Maamuzi ya kukurupuka ndio tunaisoma namba
 
Asante kwa elimu ya Uraia uliotupatia yote haya ni madhara ya kukosekana kwa Uwazi

Haswaa, uwazi ni vigumu kuwepo hasa kwa watu wasiopenda kuwajibika. Iweje kipimo cha bei kama hiyo, seikali ishindwe kuvinunua halafu inatuambiwa moja ya vipaumbele vyake ni afya.
 
Ndugu edit ulichoandika $400 sio million 840 za tanzania $300 sio million 600 au unatumia rate gani
 
Aisee kama ulichoongea kina ukweli ndani yake basi hili litakuwa ni tatizo kubwa sana ktk serikali iliyopita. Yaani wanapeleka magharama yasiyo ya msingi ktk vitu ambavyo ni none sense.
 
Yiiiiiiii.....aaaaaaa.....yalaaaa...nalia mie kwa ucunhu mkubwa
kuona kipaumbele kinawekwa kwa magari ya washa washa
kisa babu white hair kawatia amsha amsha....wakati kuna huduma
nyingi sana za msingi zinahitaji msaada wao.

Arough budget ya haya magari 7-7-7
gari moja tufanye kwa wiki lina hitaji lita za ujazo
zipatao 50 , ambapo kwa mwaka wenye wiki 52 gari moja
litahitaji jumla ya lita 2,600. Hivyo basi kwa magari yote 7-7-7
kwa mwaka mzima yahitaji lita 2,020,200 ( 2M -litters za mafuta)
ambapo kwa gharama ya lita moja ya Tsh.2,000 ina maana kwa mwaka
yanahitaji mafuta yenye thamani ya Th 4,040,400,000 (zaidi ya bilioni 4)
kuyapa mafuta tu,
hapo bad matengenezo yake na gharama za vipuri pia.

kwa leo naishia hapo tu.

Baada ya kutoa sifa nyingi kwa raisi wetu kwa kufanya ziara za kushtukiza pale muhimbili ambazo ni kama zimezaa matunda kwa kipimo cha MRI kuanza kufanya kazi, hebu sasa na tujiulize juu ya viapaumbele vya serikali yetu kama vipo sawa.
Hebu tuangalie kuhusu vipimo hivi viwili vya ct scanner na mri. Kwa mujibu wa wizara ya afya vipimo hivi vilisuswa kufanyiwa matengenezo baada ya kampuni ya Phillips kutolipwa deni lake kuvifanyia ukarabati vipimo hivyo ambalo limefikia bil. 7. Na juzi wamelipwa bil. 3 ndio kikafanyiwa matengenezo. Kwa maana hiyo serikali bado inadaiwa bil.4.

Tanzania tunavipimo hivyi katika hospitali moja tu ya muhimbili kati ya hospitali zote za serikali hapa nchini, hiki ni kichekesho na tena ni aibu!

Kwa mujibu wa kampuni ya Phillips, moja ya makampuni yanayotengeza hivi vipimo, bei ya hivi vipimo ni kati ya USD 150 _ 250 yaani sh. Mil 300 _ 500 za kitanzania kwa ct scanner ya slice 16 na USD 250 _ 300 yaani Tsh. Mil. 500 _ mil 600. Kwa ct scanner ya slice 64. Na gharama za kuifunga pamoja na mafunzo ni tsh mil. 200.

Kipimo cha MRI chenyewe huuzwa kwa USD 400 ambazo ni sawa na tsh mil. 840. Na gharama za mafunzo na kuifunga ni tsh. Mil. 300.

Kwa mujibu wa deni wanalotudai hao Phillips la matengenezo tu tungeweza kununua mashine mbili za mri na ct scanner tatu.

Tarehe 20 october kabla ya uchaguzi aliyekua raisi wetu alipokea magari mapya ya washawasha 399, ambayo ni miongoni mwa magari 777 ambayo serikali imeyaagiza kwa ajili ya uchaguzi, ambayo hayakutumika hata magari 50. Hapa ndio pakujiuliza magari yote 777 yalikuwa ma umuhimu gani!

Kwa mujibu wa mtandao wa alibaba, gari moja la washawasha(Riot control vehicle) lenye uwezo wa kubeba little 11500 za cinamon water(maji ya kuwasha), linauzwa kwa USD 250 - 400. Ambazo ni sawa na tsh mil 500 - 800!

Kwa maana hiyo gari ya washawasha moja na mashine ya mri moja bei hazitofautiani. Kwa maana hiyo yangepunguzwa magari 50 tu, serikali ingeweza kuzifunga mashine za mri na ct scanner katika hospitali zote za mikoa.

Hii inaonyesha serikalini kuna hela, tatizo ni vipaumbele vyetu ambavyo ni vibovu. Chekecha bongo ujue ni kwanini gari la washawasha ni bora kuliko vipimo muhimu kama hivi!
 
Raisi akipiga marufuku viongozi kutibiwa nje ya nchi isipokua kwa kesi stahiki na akazuia watoto wa viongozi kusoma shule za binafsi huenda nikatubu kosa la kumnyima kura yangu.

Bila kufanya hivyo, sarakasi hazitaisha!
 
Ndugu edit ulichoandika $400 sio million 840 za tanzania $300 sio million 600 au unatumia rate gani

Kuku87, sikutaka kuweka figure exactly, ila kwa exchange rate ya leo dollar moja ya marekani ni tsh. 2150.
 
acha uongo Ct scan zipo kibao huku arudha ipo aga khan ipo seliani ipo Kcmc pia. iyo MRI ipo ocen road. wala hujui kilicho tokea. wala hujui gatama za izo machine kulingana na kampuni zinazo install na slices ya picha inazo weza fanya. na mikataba ya kampuni na hospitali inayo ingia nao nimigumu hairuhusiwi kampuni nyengine kufanya service. sasa ulizia OC itakuja lini hospitali?
 
Hivi ni chama gani ambacho kimekuwa madarakani nchi hii?

Ni kosa la nani kutokuwepo kwa hizo mashine kwenye hospitali zote za serikali nchini?

Ni kosa la UKAWA? CHADEMA? CUF? TLP?
 
Hivi ni chama gani ambacho kimekuwa madarakani nchi hii?

Ni kosa la nani kutokuwepo kwa hizo mashine kwenye hospitali zote za serikali nchini?

Ni kosa la UKAWA? CHADEMA? CUF? TLP?



Ngabu uliona ile ishu ya Ethiopia ku intruduce train za umeme Addis Ababa?
dola milion 480 tu kilometa 32....
imagine that.....huku Tanzania inatumia dollar milion 800 kwa hospitality wizarani kila mwaka
 
Hivi mgombea wa UKAWA Lowasa alikuwa waziri na mtumishi wa serikali gani ukiondoa miezi miwili ya kampeni ? Analipwa pensheni kama mstaafu wa serikali ipi? Tuliomchagua JPM tulilinganisha kubwa kuliko na ndogo kuliko. Hapakuwa na CCM vs UKAWA bali A na B. Tumechagua A. Mgombea mnayemlinganisha na yanayosahihishwa alikuwa Mtendaji Mkuu wa serikali miaka 2, hakuyaona kama hao mnaowakosoa.
 
acha uongo Ct scan zipo kibao huku arudha ipo aga khan ipo seliani ipo Kcmc pia. iyo MRI ipo ocen road. wala hujui kilicho tokea. wala hujui gatama za izo machine kulingana na kampuni zinazo install na slices ya picha inazo weza fanya. na mikataba ya kampuni na hospitali inayo ingia nao nimigumu hairuhusiwi kampuni nyengine kufanya service. sasa ulizia OC itakuja lini hospitali?

Kwanza andika kama mtu anayejali wasomaji wake. Unaandika makosa meeengi. Mambo ya CT na MRI siyo mambo ya kitaalamu tena! Hizi ni enzi za intaneti na taarifa kiganjani.

Bei za CTscanner ni hizo alizoandika. kuna scanner hata za dola 95,000.
Rais aliyeondoka aliwahi pewa mfano kama huo yeye akasema ni uongo. sasa fungua ukurasa ufuatao

CT Scanner Price Guide

Utakuta taarifa hii:
Whether you're looking for marketability or to meet a Physician's or clinical demands, this is when good ol' Woody just won't cut it. If you're looking to do cardiac studies then you'll want the Buzz Lightyear of CT scanners.

64 slice CT ranges between $150,000-$250,000 installed with a "first scan" warranty. While site planning and applications training costs may remain the same, the service agreements will cost more (ranging between $100,000-$125,000). After all, the CT Tube alone can cost as much as $220,000 to replace.


And as the slice counts keep going up (128, 256 and even 320 with the Toshiba Aquilion One) the costs and clinical capabilities go up too.


If you have more CT scanner questions, let us know. We're here to serve you in navigating all the little green aliens of CT scanner project planning.
 
acha uongo Ct scan zipo kibao huku arudha ipo aga khan ipo seliani ipo Kcmc pia. iyo MRI ipo ocen road. wala hujui kilicho tokea. wala hujui gatama za izo machine kulingana na kampuni zinazo install na slices ya picha inazo weza fanya. na mikataba ya kampuni na hospitali inayo ingia nao nimigumu hairuhusiwi kampuni nyengine kufanya service. sasa ulizia OC itakuja lini hospitali?

Umenielewa nimeandika nini? Hivi aga khan, celian na kcmc ni hospitali za serikali? Pale muhimbili, philips ndio wanatender ya kukarabati hizi mashine, hebu ingia kwenye website yao uangalie wanaziuzaje! Soma mada yote uielewe.
 
Back
Top Bottom