Sarafu mpya yatolewa leo na BOT

Sarafu mpya yatolewa leo na BOT

Hapa tujiandae kuchanganyiwa 500 na 200, tusipokuwa makini, utajua umepewa elfu moja kumbe mia saba tu...
 
Nataman mtu,anieleze faida na hasara za kuwa na sarafu, na mapungufu yaliyopo kweny Noti, Nasubr jib

ngoja nijaribu kukudokeza! Hapo hasara yake tunaipima kwa hiyo note ambayo imekuwa replaced! Hasara zake ni kwamba tusitegemee tena kuiona 500 ktk sehemu kubwa za kufanya production na ktk taasisi za fedha! Pia, wana ua sifa ya pesa (portability) sarafu actually sio portability in comparison with notes!
 
Hii tathimini ya wapi kumbe sarafu mpya ikitoka ndiyo uchumi kushuka hiki nacho sijui ni kichwa gani cha huyu jamaa.

kutoka kwa sarafu kama sarafu sidhani kama kuna shida, lkn sarafu ku replace note mkuu hapo ndo kwenye shida na tatizo ki uchumi!
 
Poor Tanzania..Tunashuka n kuporomoka kwa kasi. Tumefuata nyayo za Uganda ila kwa sasa wao wamekuwa stable so tunaenda mbele zaidi kufuata nyayo za Zimbabwe. Hi ni htari. Pesa thamani imeshuka kiasi hiki? na bado tunafanya vitu not in our best interest? Uganda wao wana sarafu ya sh 500 tayari na unaona uchumi wao unavoshika mkia kati ya Tz, Kenya na Ug..Ila wao sasa hivi wanajiambatanisha na Kenya wanakuwa pulled up, in the same manner Namibia na Botswana katika SACU wanavokuwa pulled up na S.Africa. Sie Tz kwny EA tutakuwa kama Swaziland kwny SACU.
 
Gazeti la leo tarehe 08/09/2014 lina taarifa yenye kichwa cha habari kinachosomeka "sarafu ya sh 500 kuanza kutumika Oktoba".Ni Oktoba mwaka huu.

Je,nini maoni yako juu ya habari hii.
 
Ingekuwa sarafu ya TSh. 400 ingekuwa vizuri zaidi. Wangekuwa wametuepusha na usumbufu wa makonda kwenye daladala.
 
Ingekuwa sarafu ya TSh. 400 ingekuwa vizuri zaidi. Wangekuwa wametuepusha na usumbufu wa makonda kwenye daladala.

Hatari nyingine ni kuiangusha au kuipoteza.Ni bora ukapoteza mia au mia mbili na siyo mia tano itakuuma zaidi hasa ukiwa umepigika.
 
Unafikiri mi nne hiyo ya makonda itadumu? Sarafu itaharibu mifuko ya suriali zetu bure. Ni bora wangeiboresha hiyo hiyo 500 note kama madai yao ni kuchakaa haraka
 
Duh!! Hii dalili mbaya sana. Inaonyesha jinsi shilingi inavyoshuka thamani kila kukicha. Kesho itakuja sarafu ya shilingi elfu moja, mbili, kumi, elfu ishirini etc.
SARAFU MPYA YATOLEWA: BoT leo imetoa sarafu mpya ya Sh500 itakayoanza kutumika rasmi Oktoba 2014, noti za Sh500 zitatumika hadi mzunguko wake utakapoisha.

SARAFU_full.jpg
 
hata kama mi siyo mchumi, lakini naona hapo mmeporomosha uchumi , maana sarafu ya mia mbili na mia , na hamsini niyo kifo chake kimefika hivyo vitu vyote vidogo vidogo kama pipi, wembe, kipande cha sabuni n.k vitakuwa vinauzwa sh 500, kwa hiyo itaongeza mfumuko wa bei. japo kila siku mnatwambia uchumi wa bongo unakuwa sasa sijui unakuwa au unadumaa?? au unakuwa kwa kwenda chini? wachumi nisaidieni
 
Back
Top Bottom